Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Apo ulitamani uwe na gari umkimbize hospital chap
 
Nilipofikia "yule dereva aliyekuwa anapitwa akafanya kumuovateki mwenzake bila kuangalia nyuma" basi nami sikutaka kuendelea kusoma nikijua hizi ni kamba.
Wikiendi njema.
 
kwenye wahudumu
ona hiki kisa

kuna mtoto akiwa anaongea na kutembea aliletwa na bibi yake hospital X, doctor akamuangalia mtoto akaandika diazepam inj lakin dose akasaau kuandika, nurse akachukua cheti akenda famasi akachukua diazepam 10mg, mkuu hiyo diazepam na anapewa mtoto chini ya miaka 4, nurse kavuta dawa kamdunga mtoto 10mg ya diazepam, kumbuka mtoto alikuja hospital anongea anatembea na alikuwa na uwezo wa kucheza.. baada ya mtoto kupewa hiyo dawa dakika chache tu mtoto akaanza kutetemeka nurse akaitwa, nurse akaangalia akaulizwa na wenzake umempa kiasi gan cha dawa? nurse kuangalia vizuri cheti akaanza kuogopa na yeye, baada ya kumuita doctor amsaidie nurse akaenda famasi eti kutafuta antdote ya diazepam, baada ya dakika chache zingine mtoto akaanza kutoa povu na badae akafariki. bibi wa watu alikuja na mjukuu wake akiwa mzima lakini akaondoka na msiba, kifo cha kizembe kabisaa

haya hapo huyo nurse na doctor kuna kazi gani kubwa waliifanya kwenye mazingira magumu yakupewa pongezi zaidi ya kuleta kifo cha bure bure.

kuna kesi kama hizo za kijingajinga watu wanakufaa kizembe kwa sababu ya uzembe tu.

mimi sio muandikaji sana, lakin nina vingi tu vya aina hiyoo. hospital uzembee mwingi tu, watoa huduma hawana utu, wapo waluwalu (sijui ni ujana) hawana pride na kazi zao.
 
Doooh, mkuu pole sana aisee, i cant even imagine, Baba mzazi aisee dooh, poleni sana.
 
Chai. Kuna viashiria vingi kuwa hii ni chai. Kwa wale wataalam wanaojua makosa wanaofanya wasimulizi wa ''story chai'' wa Bongo watakubaliana na mimi.
Dogo acha ujinga, hakuna mtu wa kupoteza muda wake hapa, kwani tunalipwa? yaani niandike hayo yote ili nipate nini? Hili ni darsa huru uenda likawa msaada kwa watu wengine, by the way haujafa haujaumbika what if the next person ukawa ni wewe na tena ukasuswa mapokezi tu? si utaukumbuka huu uzi huku unatubu dhambi zako zote.
 
Doooh huyo bibi angefungua kesi ya madai, na hapo kuna pure jinai ya malpractice kabisa. So sorry aisee.
 
Watu wa daladala wa hovyo sana kuna siku hivyohivyo tupo kwenye gari wanashindana karibu na victoria tushafika kabisa safari yetu morroco jamaa mwengine akahama kaja kwetu ilibaki al manusura tupinduke dereva wetu alijitahidi akapeleka kwenye zile sehemu zakati zinazotenganisha upande yani tuliyumba mara 6 Mungu amuweke yule dereva ..Cha ajabu Magari yote kampuni moja πŸ˜‚
 
Fafanua hili, unataka kumpita aliyeko mbele yako lakini anaamua kukupita bila kuangalia nyuma! Mimi nilipofikia hapo sikutaka kuendelea kusoma.
 
Pole sn mkuu
 
Fafanua hili, unataka kumpita aliyeko mbele yako lakini anaamua kukupita bila kuangalia nyuma! Mimi nilipofikia hapo sikutaka kuendelea kusoma.

Hapa mleta mada amechanganya kidogo maelezo sijui labda sabab ya ajali…..

Kwanza kabsa gari zilkua znaenda one direction ile single phase sasa kilichotokea ni hiki……..huyu dereva aliokuwa nyuma kipindi ana overtake tayari alikua ameingiza gari kwenye line ya pili(upande ambao bro alikua anakuja na gari yake hapa wangekutana uso kwa uso)…

Ilibid busara itumike ambayo ni dereva wa gari ilyokua kushoto amuachie jamaa apite kiroho safi maana yeye tayari anakua mtu ambaye kwanza ajali anaiona kabsa hii hapa lakin pia alkua na uwezo wa kuizuia isitokee(nidhamu ya barabara) kibaya zaid na yeye akaamua kukaza ubongo…

Pia inategemea na hali ya barabara ilkuaje na watumiaji wengine wako vip,hapo ilibid bro(aliepata ajal) aweke gari pemben yaan atoke barabaran kabsa huku akiangalia usalama(udereva wa kujihami)…

Yote kwa yote pole sana bro kwa ajali naelewa nn maana ya ajal na huwa inatokea within seconds tu inahitaji akili ya haraka kuzuia unachokiona mbele
 
Afrika ni kama njia panda ya kuzimu...kuna mambo ya kipumbavu sana huwezi imagine kabisa

Watu wengi sana wamepoteza uhai kwa makosa ya makusudi ya wenye walau kuweza okoa maisha ya watu...
 
pole sana sana
 
Pole sana kiongozi
 
Chai. Kuna viashiria vingi kuwa hii ni chai. Kwa wale wataalam wanaojua makosa wanaofanya wasimulizi wa ''story chai'' wa Bongo watakubaliana na mimi.
Hatuwezi kukubaliana na wewe hadi utoe uchambuzi wako wa Uzi huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…