Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Sawa muhudumu wa Afya tumekuelewa
 
Afrika ni kama njia panda ya kuzimu...kuna mambo ya kipumbavu sana huwezi imagine kabisa

Watu wengi sana wamepoteza uhai kwa makosa ya makusudi ya wenye walau kuweza okoa maisha ya watu...
Ni vile Kuna watu wamezaliwa familia za kimasikini sana na watoto wengi sana kiasi cha kuoneana wivu na kukosa utu kwenye mioyo yao Sasa huko nje familia inawatoto wachache na wote wanapendana hivyo wakiona familia zingine zinashida wanaonyesha Upendo wao na kama ni huduma wanatoa huduma nzuri za kuokoa uhai kwa moyo wa Upendo.
 
Pole kwa madhira hayo yaliyokukuta!
In short kwa nchi yetu ugonjwa wenye uhakika wa kupona ni UTI ! A little complication unaaga dunia!
Pia gharama za matibabu ni kubwa nimewahi kuishi nchi moja ya kiafrika kwa kweli huduma zao za afya ni sawa na bure unalipa Sh. 50 kumuona na daktar na 250 kununua dawa (dawa aina yoyote) na dawa zinapatikana.kwa gharama hizi zinawavutia wananchi kuwahi mapema pind tu tatizo linapoanza na sio kusubiri hatua za mwisho. Thus why I don’t wonder why they have low mortality rate!
Nilishangaa kwenda muhimbili na kuambiwa kama hauna Bima kumuona daktari tu ni elfu 30 mbali na vipimo na dawa! How many can can afford ?
 
Unaimani thabiti sana kwa Mungu wetu,na naamini ndio imekuponya. "Nyanyuka uende zako,imani yako imekuponya". Ukawe shuhuda kwa mataifa juu yake. Kamwe usiiache kwani Mungu anakusudi kwa kila mmoja wetu.Pole sana mkuu,umesisima imara na sasa songa mbele tena
 
Poleni sana. Shemeji yako alipata kitu imaitwa "Retrodgrade amnesia". Ni complication ambayo ni common baada ya ajali inayohusisha kichwa.
Hope sasa hivi anaendelea poa.
 
Pale Muhimbili emergence ni ushubwada sana pale wale watoto sijui ni intern wale.
Na kweli wengi ni Samsung na infinix. Zile za zamani.
Kwangu Mimi, nilikula Mzinga mwaka 2017, nikalala Bochi Mwaka na miezi nane? Aisee nilipitia Mengi ila nilipona kwa uwezo wa Mungu. Sikutoka kitandani mwaka na miezi miwili, miezi sita ilikua yakujitoa muhanga.
Nimewahi kutaka kutoroka kitandani, nakutwa nimedondoka chini siwezi rudi kitamdani, nimefanya physical workouts nilinunua vyuma vya gym nikawa napiga kitandani. Mpaka siku niliwezi kuinuka,
Na nilifanikiwa kupiga show in the same 6 months zakujiweka sawa kashori kangu kamoja. Aisee. Hizi ajari, acha tu.
 
Umeweka emoj ya kucheka itafikia wakati utashindwa kuwe emoj ,Kama abiria mlishindwa nini kushuka kwenda kumtia mbata huyo dereva mpumbavu?
 
Pole sana..bongo kifo nje nje..usipo fia kwenye tukio unaweza fia hospitali kwa kuchelewa kupata huduma.

#MaendeleoHayanaChama
 
Doooh mkuu pole sana, story yako nusu inachekesha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nusu ina ujumbe mzito sana, ilikuaje hio siku ya mzinga na uliumia uti wa mgongo au kichwa maana mwaka na miezi nane sio mchezo mzee.
 
Pole sana..bongo kifo nje nje..usipo fia kwenye tukio unaweza fia hospitali kwa kuchelewa kupata huduma.

#MaendeleoHayanaChama
Very true, ndo mtu mmoja hapo juu akasema "sasa iv bongo tulipaswa kua milion 90 sema hospitali zetu tu ndo zimetuyeyusha".
 
Poleni sana. Shemeji yako alipata kitu imaitwa "Retrodgrade amnesia". Ni complication ambayo ni common baada ya ajali inayohusisha kichwa.
Hope sasa hivi anaendelea poa.
Sorry mkuu, hali hio hua inadumu kwa kipindi cha muda gani?
 
Hii ya kusema kung'ang'ania brake ndio imekuvunja mguu ni kweli. Jamaa yangu mmoja nae hivyo hivyo ule mguu ulioshikilia brake baada ya kishindo ukasukumwa juu ukapachuka kwenye hip hapo sema mambo ya hela yakasaidia akaenda India wakamuweka sawa
Tatizo ile hali hutokea kama tendo automatic kwani tukio ni la ghafla....kila kwenye ajali akili hukimbilia kwenye beki.
 
Pole son.

Na vipi kuhusu gari na vitu vyako ulikuwa navyo kwenye gari.

Hosp wapo wenye roho mmbaya acha tu
 
Pole sana mkuu 800 kama 800 dah maisha haya yani
 
Pole Mkuu.Ila story yako haijasaidia chochote. Hukutakiwa kuficha jina la hiyo hospitali uliyoanzia. Laiti kama ungeitaja hapa hakika ungekuwa umesaidia wengi sana. Naamimi wahusika wangejiona hapa wangeshikwa na mshipa wa aibu wangejirekebisha, aidha mamlaka za juu zingewakemea. Ungekuwa umeokoa uhai wa watu wengiHukutakiwa kuficha. Unaogopa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…