Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Doooh mkuu pole sana, story yako nusu inachekesha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nusu ina ujumbe mzito sana, ilikuaje hio siku ya mzinga na uliumia uti wa mgongo au kichwa maana mwaka na miezi nane sio mchezo mzee.
Uti wa mgongo mzee wangu.
 
Umemuomba mungu afya njema yeye akakujalia ajali halafu kwa uwezo mshangavu akakuponya na wadau wanamshukuru hapa.
 
Hii ya kusema kung'ang'ania brake ndio imekuvunja mguu ni kweli. Jamaa yangu mmoja nae hivyo hivyo ule mguu ulioshikilia brake baada ya kishindo ukasukumwa juu ukapachuka kwenye hip hapo sema mambo ya hela yakasaidia akaenda India wakamuweka sawa
Bora angeacha asukumiziwe mbele au sio? Ukigongwa tokea nyuma lazma utengeneze opposing force nahisi ndio ilimuumiza zaidi jamaa
 
Hii nchi kwenye huduma bado saaaaana tena sana, hospitali na polisi ni mtihani hasa ukiwa masikini Mungu atusaidie.Pole sana stori yako imenihuzunisha sana japo am happy u r ok
Na awamu hii ndo itakuwa NECTA kabisa maana ni zaidi ya mtihani!
 
Inauma sana yani
 
Pol

Pole ndugu Kwa masaibu.. unashangaa ungetembea speed kubwa Wala usingpata ajali. Maisha ni fumbooo
Eeh mambo ya kuzubaa zubaa barabarani hayo sio mazuri mkuu! Katika kuendesha gari nimejifunza mambo makuu matatu.

1.Kutokukaa nyuma ya boda boda, bajaji wala lorry ama kwa mda mrefu. Huwa nazikimbia kwa namna yeyote ile.

2.Naepuka kuongozana mtu ambaye hana maamuzi katika uendeshaji aidha anafunga funga breki hovyo, hawashi indicators. Huwa nampita kisha nanyoosha kibati mpaka nifike mita kadhaa mbali toka alipo ambapo nakuwa mwenyewe njia nyeupe mbele na nyuma.

3.Kuchukua hatua haraka napoona mbele kuna upumbavu umefanyika ghafla ambao ungenihatarishia kupata ajali. Aidha mtu kachomeka kijinga, au daladala inasimama ghafla mbele yangu n.k au mtu anazubaa wakati taa zimeruhusu!
 
Ukiingia barabarani utagundua kuna wenzetu huu uhai hawaupi thamani sana.
 
Pole sana mkuu.
Hii story yako inasikitisha sana. Kwa bahati mbaya sana, story kama hii watu wengi sana huwa wanapitia, na wengine huishia kufariki. Naiangalia story yako kwa upana zaidi, imeibua mambo kadhaa kwenye fikra zangu...
1.Mfumo wetu wa afya uko vibaya sana kwenye ku "respond" katika ajali... Yaani pale ajali inapotokea; Watanzania wengi hawajui nini cha kufanya baada ya ajali kutokea, na ucheleweshaji huanzia pale. Pia, lingine linaloendana na hili ni watu wengi kutokua na basics za huduma ya kwanza (first aid) vitu kama nini cha kufanya kuzuia au kupunguza damu kuvuja kwa majeruhi, nini cha kufanya kwa majeruhi, na kadhalika. Kuna tafiti nyingi ambazo zimeonyesha karibu asilimia 50 ya vifo vinavyotokana na ajali kwenye nchi za dunia ya tatu,vingeweza kuepukika kama wangepatiwa huduma ya kwanza kwa haraka.
2.Mfumo wetu wa afya una mapungufu makubwa pia kwenye namna ya kuwapokea, na kuwahudumia majeruhi wa ajali kwa uharaka unaostahili... Huu utaratibu unaitwa triaging... Yaani kuweza kujua mgonjwa huyu anahitaji huduma ya haraka, huyu anaweza akasubiri kidogo, yule anatakiwa apate huduma ndani ya lisaa limoja la sivyo atafariki. Hapa ni stage ya pili ambapo ucheleweshaji wa huduma kwa majeruhi wa ajali unatokea, na kupelekea pia vifo zaidi vya majeruhi hata baada ya kufikishwa hospitali; Hili linakwenda sambamba pia na mfumo mbovu wa rufaa ambao pia umeonekana wazi kwenye huu mkasa wako, ambao ulipelekea ucheleweshwaji wa masaa kadhaa kutoka hospitali ya wilaya hadi kufikishwa hospitali ya taifa. Yote haya yanasababisha idadi kubwa ya vifo kutokana na ajali ambavyo vingeweza kabisa kuzuiwa.
3.Uelewa na umahiri wa watoa huduma kwa majeruhi wa ajali-Hili pia limekua wazi kabisa katika mkasa wako, watoa huduma kutojua nini cha kufanya eidha kwa makusudi kabisa (kwa sababu ya kukosa motisha, au kutokujali tu au kutaka rushwa), au saa zingine ni kweli kabisa wanakua hawajui nini wanatakiwa kufanya kwa mgonjwa gani... Kama ambavyo umeshuhudia kuwa ulikuta interns/wanafunzi hapo emergency ambao hawakuonyesha kujali sana, labda kwa sababu ya kukosa muongozo kutoka kwa senior anayeelewa. Je, ni kwa nini emergence pajae wanafunzi/interns bila kuwepo seniors wa kutosha kuwaongoza? Ni kwa sababu ya upungufu wa watoa huduma? Au ni kutokujali tu?

Hizo changamoto tatu hapo juu zinasababisha vifo vingi sana vya majeruhi wa ajali ambao wangeweza kupona. Na hii hali haitabadilika hadi zitakapofanyiwa kazi ipasavyo.
 
Ila umezengua bana, sasa umeshindwa nini
Kutaja jina la hiyo hospitali ndogo na kubwa
ili wenye mamlaka wafahamu uozo uliopo, ingekua imesaidia kiasi fulani. Ila pole sana mzee na Ahimidiwe Mungu aliyekuponya.
Then like kitu kilichokwambia uchukue tahadhari huyo ni Roho Mtakatifu. Siku nyingine usimwite kitu ama machale yakanicheza kama wengine wanavyosema. Sio machale wala kitu ila ni Roho Mtakatifu ambaye hutuongoza.
 
HOSPITALI KUBWA YA TAIFA NI IPI KAMA SIO MUHI-2 NA MLOGANZIRLA?
 
Unajiita 666 halafu unasema upo karibu na Mungu.
 
Pole sana chifu
 
Acheni kujitetea! Kama ni hvyo kwann sasa mkipewa hela mnachangamka?, Si mngekuwa mnakataa..ni wachache ndo wapo committed na kazi. Hujiulizi kwann wasisingiziwe wengne ..
 
Huko kwenye wodi za wazazi ni balaa tupu, rushwa nje nje na wala hawaogopi!
 
Boda ni waseng* Sana,hili tusi siwezi kulitoa imelazimika niliandike hapa, baada ya kusoma mwanao aligongwa na boda,
Kuna siku boda boda mmoja alikuwa amebeba madumu mawili ya petrol Lita 20 alafu Yuko speed,wakati Ana over take bila kuangalia mbele yake akagonga gari yetu na ile pikipiki yake ikaanza kuwaka Moto hapo hapo
 
Hyo namba ya ID yako ndo inakupa mikosi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…