G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,505
- 40,002
Huu ni ushuhuda wa kweli na jinsi nilivyowaona Polisi wakiua raia hizo siku.
October 29 kuanzia saa moja usiku.
Polisi walikuwa wamejificha kwenye makutano ya barabara fulani juu ya ghorofa na hapo kila mpita njia aliyekuwa anapita kuanzia saa moja usiku alikuwa anakula shaba. Wengi hawakujua kama kulikuwa na mtu au watu aliyekuwa akiwalenga kutokea juu ghorofani.
Mbaya zaidi maiti zilikuwa zikifika kadhaa inakuja gari nyingine inachukua na kutokomea nazo. Nilishuhudia dereva boda bda kadhaa wakiwa wanaweweseka punde tu baada ya kufika eneo lile na muda mfupi baadae unaona mtu kaanguka.
Octoba 30 kuanzia saa sita usiku wa manane.
Nikiwa ndani kwangu karibu kabisa na makutano ya barabara kuu, nilisikia milio ya risasi tena siyo zile risasi za kutoka kwa ku-koki. Ni zile risasi unasikia bunduki inapiga mfululizo. Zilikuwa zinapiga mfululizo mara tatu kisha unasikia kimya kimetanda, baada ya dakika kadhaa unasikia tena.
Kuamkia Octoba 30
Hapa ndipo niliposhuhudia maiti mbili zikiwa zimetelekezwa karibu kabisa na eneo la kwangu huku moja ikiwa imepigwa risasi kutokea upande wa mbele wa kifua na kupita mgongoni na maiti nyingine ikiwa risasi imepita ubavu mmoja wa tumbo kutokea ubavu mwingine.
Asubuhi hiyo tukiwa tunahamaki kutazama zile maiti ikaja gari ya polisi haraka sana na kufyatua risasi ambapo pale pale walijeruhiwa watu wawili (Sijui kama bado wapo hai ingawa siku ile mpaka jioni bado walikuwa hospitali)
Cha ajabu hii gari ya polisi baada ya kufyatua zile risasi wakatokomea na kuacha zile maiti ambazo baadae zilikaa eneo lile kwa zaidi ya masaa 36 bila kuchukuliwa.
Hali hii ya kusikia milio ya risasi iliendelea hadi kufikia usiku wa kuamkia jumatatu ya juzi. Sijui walikufa wangapi ila mtaani kwetu tulipata kazi ya kuishi na maiti kama ndugu!