Namna nilivyopambana na Kampuni Binafsi ya Bima Ya Afya na kuwapiga Knock Out kwa msaada wa Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO)

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Igweeee wananzengo,

Leo napenda ku-share uzoefu wangu na moja ya kampuni binafsi za bima ya afya hapa Tanzania ambayo walikataa kabisa kulipia matibabu ya mke wangu, ikiwemo upasuaji, huku wakitoa sababu ambazo zipo kinyume kabisa na mkataba wangu kati yao.

Pia, nilipojaribu kuwasiliana nao kwa simu, awali, maongezi na kampuni ya bima yalikuwa mazuri lakini ghafla walianza kunizungusha na mwishowe wakapotezea kabisa simu zangu. Hawakutaka hata kusikia shida niliyokuwa nayo, jambo lililoniacha njia panda.

Kutokana na hali hii, nililazimika kulipia gharama zote za matibabu kutoka mfukoni mwangu, jambo lililoniathiri kifedha na kihisia. Baada ya kupona kwa mke wangu, nilianza kutafakari njia za kudai haki yangu. Nilikaribia kwenda mahakamani lakini gharama na muda vinavyohusika viliniogopesha.

Nikiwa sina la kufanya, baada ya kuongea na watu wawili watatu, niligundua kuhusu ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima. Nilijaribu bahati yangu na kuwasiliana na msuluhishi mkuu, ambae alinipa maelekezo ya nini cha kufanya, ikiwa ni pamoja na nyaraka zinazohitajika ili waanze kushughulikia mgogoro huo, na namna ya kuzituma.

Kwa kweli, walichukua hatua haraka kuliko nilivyotarajia. Mikutano yote ilifanyika kwa njia ya mtandao, na sikuhitaji kusafiri kwenda Dar es Salaam, kwa sababu mimi naishi mkoani, nje ya Dar.

Baada ya majadiliano na mikutano kadhaa ya usuluhishi, na kuonekana wazi kuwa kampuni ya bima walichemka na hawakunitendea haki, walikubali walifanya makosa na wakanipa pole. Pia, walirejesha gharama zote nilizolipa na tukafikia makubaliano ya fidia kwa usumbufu na stress waliyonisababishia mimi na familia yangu.

Tukio hili linaonyesha ni jinsi gani kampuni nyingi za bima hapa nchini hazina utu wala hazijali wateja wao. Kila kitu kinachukuliwa kimazoea tu mpaka pale mtu anapopiga kelele. Kwa yeyote aliye na mgogoro na kampuni yoyote ile ya bima (bima ya aina yoyote ile-ya afya, ya chombo cha moto, ya maisha, na kadhalika), usikubali kunyanyasika.

Msuluhishi wa Bima yupo kwa ajili yetu. Anaweza kusaidia kupata haki yako bila stress za mahakamani. Pia, hawa jamaa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa sana, nilikua na wasiwasi kama naweza kuipata haki yangu kupitia ofisi hii, lakini kiukweli wamekua na weledi mkubwa sana.

Kwa taarifa zaidi au msaada, unaweza kuwasiliana na ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima kwa barua pepe msuluhishi@tio.go.tz au kutembelea tovuti yao www.tio.go.tz.

Tujilinde, tujisaidie. Haki ya mtu haiendi chini ya ulimi. Asanteni kwa kusoma, na kumbuka kudai haki yako kila wakati!

View: https://www.youtube.com/watch?v=03SoFse1TYc
 
Safi sana mkuu!! Umejua kuwanyoosha kweli kweli matapeli hao!
 
Naku PM, na mimi kuna kampuni moja ya bima nawadai, wananizungusha tu tangu mwaka 2023.
 
Dokta huwa nakubali michango na hoja zako ila siku hizi hutumii sana JF.
Kwanza, nashukuru sana mkuu kwa kukubali hoja zangu humu, asante sana.
Pili, ni kweli kabisa, uwepo wangu JF umepungua sana siku za karibuni, ni kwa sababu siku za hivi karibuni nimekua busy sana. Lakini, nitajitahidi nirudishe uwepo wangu kwa wingi humu hasa siku za weekend!
 
Back
Top Bottom