Alexander von Humbolt
Member
- Sep 18, 2022
- 10
- 2
Nawasalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania........
Naamini wengi wetu tuko salama na tunaendelea kupambana na maisha. Karibuni kwenye mada tusaidiane mawazo ikiwa ni elimu kwangu mleta mada, lakini pia fundisho kwa wengi wetu tunaopenda kujishugulisha na siasa na uongozi.
Mimi ni kijana mwenye miaka 30+. Elimu yangu ni shahada ya uzamili, nimesoma nje ya nchi degree ya kwanza na ya pili. Familia yangu ni familia zile za kawaida sana. Nilisoma kwa udhamini (Scholarship). Tangu nimalize elimu yangu sijafanikiwa kupata kazi ya kueleweka. Napambana hapa na pale kujikimu na maisha. Kitaaluma ni Muikolojia (Ecologist), mwenye machapisho kadhaa ya kitaama.
Ninapenda sana siasa na naamini ninao uwezo wa kuongoza. Kwa sasa sina direct affiliation na Chama cha siasa moja kwa moja. Lakini ni "active and concerned citizen" kwa maana nafuatilia kwa karibu siasa za nchi yetu. Nahisi muda umefika niingie moja kwa moja kuhudumia watu kwa njia hii.
Nimeleta mada hii hapa ili tusaidiane yafuatayo;
1. Sina network wala mtu yeyote nayemfahamu anajihusisha na siasa moja kwa moja kwenye vyama vya siasa. Naanzia wapi kufanikisha malengo yangu?
2. Je nianze kwa kujiunga na chama kimojawapo cha siasa au nianze kama mwanaharakati?
3. Namna gani naweza kujuana na wanasiasa wakubwa na nikapata mentor (kiongozi mwelekezi) kwenye siasa akanielekeza njia na kunishika mkono kuelekea kufikia malengo yangu?
4. Kama kuna marafiki humu ndani wenye network ya kisiasa naomba sana njooni PM mnishike mkono mwenzenu nipate pakuanzia.
5. Naweza kujitolea kufanya kazi either kwenye chama cha siasa au/na mwanasiasa mzoefu/mkongwe ili kujifunza siasa za field bila malipo. Hivyo kama kuna msamalia mwema wakufanikisha hili na yupo hapa au unamfahamu asisite kuja PM.
N:B. Uzoefu wangu mdogo kwenye siasa nimefanya nje ya nchi kama kiongozi kwenye serikali za wanafunzi. Siasa za nje ya nchi vyuoni hazina nguvu kama Tanzania.
Karibuni kwa mawazo na namna yoyoye nzuri kufanikisha hili.
Asante.