Namna nzuri ya kuwa Winga na Pointa wa biashara ya mitumba

Namna nzuri ya kuwa Winga na Pointa wa biashara ya mitumba

Kalaga Baho Nongwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
9,953
Reaction score
23,150
Na Mwalim M. A, Mkombozi (Kalaga baho)

Kanusho : Hakuna mgogoro wowote wa kimaslahi utakaojiyokeza kwenye darasa hili endelevu. Ushauri utatolewa bure kabisa na hakuna nia ya moja kwa moja ya kuumiza hisia ya mtu.

Asee niaje? Wazee mpo??
Ni vyema kwa kias chake kuendelea kumwaga nondo na kushea uzoefu katika mapambano kwa vijana wenzetu. Kuendelea kupeana maujanja na michongo ili tuendeshe gurudum la maisha. Ni katika harakati tu za kujikwamua na kujitegemea, juhudi za kuusaka utajiri badobado!.. Ofkoooz ni jambo linalotia moyo, na kupendeza sana!

Leo, kalaga baho ninazungumzia machache sana, japo mengi kwa kadiri ya uchache utakaofikirika. Yote yatahusu kona mbili tu yani 1. "Uwinga kariakoo", 2. "Pointa Ilala boma" na yote mawili yatabeba dhima ya kumsaidia kijana walau kuanza kuthubutu kufanya jambo.

Niliwahi kuzungumzia kuhusu mitumba- uzoefu wa ilala boma 2018-2021, na nina uzoefu wa uwinga kariakoo. Vyote kwa pamoja nitashea humuhumu.

1. WINGA
Winga ni mtu kati, dalali anayeuza kitu cha mwingine kwa bei juu ili apate chochote "ganji". Winga huwepo masoko yote makubwa yanayouza nguo, simu au bidhaa ambazo si chakula kilichopikwa. Hata chakula katika mfumo wa nafaka winga huwepo. Madalali hawa wanakabidhiwa mizigo wauze ili wapeleke hesabu.. wengine hupeleka wateja na kupewa ganji na muuza duka. Ni wazuri sana kwa wauzaji mana wachangamfu na wanauza kweli, wabaya kwa mteja mana huwa na bei juu sana. Huwa na sifa ya kubambikia wateja vitu vibovu. Mawinga ni wengi sna Kariakoo, Ilala, Manzese, Tandika,Mbagala na karume. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia mawinga wanatumia mitandao ya kufanya biashara zao. Wanaunda magroup wasap na kubust matangazo Instagram. Uwinga ni pesa, kazi na fursa kama zilivyo nyingine.

Shida ya mawinga
1. Ulevi na anasa, wengi huwa hawaon cha maana cha kufanyia pesa wanayopata. Ilala yote ile mawinga ni walevi walevi na vijana wasioleweka tu.
2. Dhulma na ujanja ujanja
Hakuna watu ambao hawafai kuaminiwa kama hawa jamaa. Mkiuza kitu mgawane hapohapo mana ukitoa kisogo umekwisha. Pia wajanja sana, huwez kutoa gepu hata kidogo mana waharibifu
3. Winga wanauza kila kitu kwa bei juu.
4. Ugumu ulipotiliza kukua kibiashara kama mfanyabiashara. Yani winga wote wanasafa kukuza biashara zao mana hawana uwezo wa kupeleka wateja dukan.. wanapoteza wateja kila leo kwa sabab ya kufika dukani tu

Uzuri wake
1. Exposure ya biashara, kujua bei na machimbo
2. Haihitaji mtaji, hupati hasara wala hulipi kodi.
3. Networking na kukua kiujuzi
 
Unawezje kuwa winga?
Namna ya kuwa winga#...
1. Chagua bidhaa ya kuifanyia uwinga/kudalalia
2. Fanyia utafiti kwanza bidhaa hiyo yani kujua bei, original na feki kwa kutofautisha/quality arrangement, machimbo yalipo na bei ya machimbo versus faida inayopatikana kwa mtu akiuza nje ya machimbo hayo
3. Fika machimbo ujionee uhalisia
4. Tengeneza network ya wauzaji wengine nje ya machimbo
5. Anza kutafuta wateja wa bidhaa hiyo kwa mitandao kwa bei YAKO (Weka status, bust matangazo instagram au post jf, fb)

Darasa hili pia nitashea na machimbo na bei ya bidhaa zinazopatikana kwa kadiri muda utakavyoniruhusu.
 
Mfano 1.
1. Unataka kuuza mashuka, tafiti ya awali itakuambia mashuka yanaenda sambamba sana na Taulo, neti, for onyo, mito, pazia na duvet..
2. Mashuka pia yamepangwa kwa majina, chapa na lebo kama chapa ya HIS (uganda) kuna shuka za Thailand (H&F na HM) ambayo yana quality tofauti na bei yanatofautiana. Uganda ni elf 31 na Thailand ni elf 20 kwa chapa ya H &F na elf 19 kw H&M chapa
3. Tembelea machimbo y shuka hizi ambayo yako kariakoo mtaa wa Aggrey na Swahili, mchikichi na swahili, livingstone na Aggrey na Sikkuu na Aggrey uone utofaut wa bei kati ya bei ya kuuza jumla na muuza really mfan. Shuka za Thailand bei ya jumla ni elf 16 (kwa mchina) na bei ya reja ni elf 20 (kwa wauzaji). Lakini pia winga na pointa wanauza elfu 25. Hapo utaona faida yako inatokeaje
4. Anza kujihusisha na uuzaji kwa watu walioaribu na wewe (yaani Wanalipia unawapelekea)
5. Tumia lugha ya kibiashara mfano (imebakia hii tu, wahi sasa ni chache.., shuka nzuri na quality! Etcetera) na hakikisha unasisitiza kuwa hutaki wateja wapate usumbufu wa kukufata. Yani wewe ndo utapeleka ili umtoe tamaa ya kutaka kujua duk lako liko wapi au alike dukani
6. Hakikisha kila unayemhudumia humpeleki kokote kumuaminisha kuwa duka hilo mlilopo ni lako
 
ZINGATIO
1.Winga lazima uwe mchangamfu
2. Winga lazima ujue machimbo
3. Winga lazima ujue badiliko la ghafla la bei ya unachokiuza au bei halisi
4. Winga lazima uwe na uelewa wa quality ya bidhaa na utofauti wa bei kati ya maduka ya kariakok na sehemu wanapochuku bidhaa hizo.
5. Winga lazima ukutane na wateja wapya kila siku.. kama haufanyi B2B hili ni muhimu kwan wateja hawana guarantee akijua bei yako iko juu atakukimbia tu. So lazima upate mteja mpya na uwe na sifa extra yani UAMINIFU, DELIVER au KUSAIDIA KUBEBA MZIGO BURE HADI STENDI ama KUmsindikiza mteja kwenye mitaa au machimbo ya bidhaa ambazo wewe umekiri kuwa hauuzi.

JITAHIDI SANA, kupata wateja wengi wa mikoani na nje ya nchi ili kuepousha usumbufu wa nteja yule kutaka kufika dukani kwako
 
MACHIMBO
1. Simu, vifaa vya elekitroniki kama chaji, eafoni, adopter na TV nenda mtaa wa aggrey na Likoma/Msimbazi. Duka maarufu pale linaitwa Mashariki. Ingawq simu kwq zanzibar ni nafuu sana.. last time nimenunua A25 Samsung kwa 450 tu wqkati kariakoo yote ni 600+

2. Nguo za kike nenda mtaa wa mchikichi na nyamwezi, na mtaa wa muhonda na raha. Tafuta maduka kama ya baba d (mchikichi na Congo) nenda duka la Amos mtaa wa Raha na Muhonda. Tafuta duka la Dar kitonga pale wanyama hotel
 
3. Tafuta jengo linaitwa Colombia liko aggrey na Congo ufike duka la braga kwa pochi
 

Attachments

  • IMG-20240715-WA0095.jpeg
    IMG-20240715-WA0095.jpeg
    1 MB · Views: 33
  • IMG-20240715-WA0105.jpeg
    IMG-20240715-WA0105.jpeg
    1,003 KB · Views: 32
  • IMG-20240715-WA0084.jpg
    IMG-20240715-WA0084.jpg
    168.7 KB · Views: 30
  • IMG-20240715-WA0060.jpeg
    IMG-20240715-WA0060.jpeg
    1.4 MB · Views: 28
  • IMG-20240715-WA0037.jpg
    IMG-20240715-WA0037.jpg
    54.4 KB · Views: 37
  • IMG-20240715-WA0029.jpeg
    IMG-20240715-WA0029.jpeg
    1 MB · Views: 32
  • IMG-20240713-WA0051.jpg
    IMG-20240713-WA0051.jpg
    93.2 KB · Views: 29
  • IMG-20240713-WA0049.jpg
    IMG-20240713-WA0049.jpg
    164.7 KB · Views: 30
  • IMG-20240713-WA0048.jpg
    IMG-20240713-WA0048.jpg
    104.9 KB · Views: 28
  • IMG-20240713-WA0044.jpg
    IMG-20240713-WA0044.jpg
    116.1 KB · Views: 29
  • IMG-20240713-WA0042.jpg
    IMG-20240713-WA0042.jpg
    130.1 KB · Views: 33
  • IMG-20240713-WA0035.jpg
    IMG-20240713-WA0035.jpg
    64.6 KB · Views: 37
Mtaa wa Kongo na aggrey huwa kuna maduka mengi sana pale ya pochi, kuna maduka ya ndakilawe, chuwa na kadhalika. Huu mtaa uko karibu sana/nyuma ya jengo la kariakoo la infinix . Wamachinga wote huchukua pochi hapo mana mtaa huu unasifika kuwa ni "UCHOCHORO WA POCHI"
 
Winga kuwa na kama network of trustees, watu watakaokulinda kuchukua mali ya tajiri. Kama wewe ni Sudi basi Jose akiwa mwaminifu na mzoefu anakupeleka kwa tajiri wake na anamwambia "Sudi amenyooka hana shida" basi wewe njia nyeupe kuchukua mali kwa tajiri wa Jose. Ni kama kujiunga na kilinge cha wachawi, huna mdhamini itaonekana we mlokole tu.
 
Ukitaka kuuza vitu kama shuka, neti, taulo chupi, sidiria, vikoi, Bahamas nk hapo unacheza na mitaa ya aggrey na livingstone, nenda pia MCHIKICHI NA SWAHILI hapo kuna jengo jeupe flani hivi lina underground floor. Hili jengo linauza mazurka, duvet, taulo na nguo za ndani. Pia floor ya kwanza wanauza pazia kwa mchina flani hivi.. bei nzuri piga picha uza mtandaoni

Njoo mtaa wa livingstone na Aggrey huku karibu na kituo cha BAHRESA, fika dukani kwa MWANGALA anauza shuka za Pakistan na Thailand, taulo pia anauza mito na foronya. Mito mikubwa ya kitanda 25 kwa laki moja tu.

7. Ukitaka kuuza bidhaa zinahoshuiana na kufungashia. Njoo Tandamti na Nyamwezi karibu na kariakok shimoni. Nenda mtaa wa pemba kwa mkongwe.. huko utapata chupa, dumu, mifuko, box za pizza na take away plates... nk (sitoi namba naheshim privacy)

8. Unataka kuuza tisheti, shati au jinzi za quality nzuri kutoka India na uturuki nenda jengo la Raha restaurants underground. Huko utafika duka la Ylb na maduka mengine kibao yanauza tisheti kali kwa eld 12, elf 15 au 16 nyingine elf 10 kwa bei ya jumla. Jengo hili liko karibu sana na stendi ya mwemdokas ya msimbaz B
 
Winga kuwa na kama network of trustees, watu watakaokulinda kuchukua mali ya tajiri. Kama wewe ni Sudi basi Jose akiwa mwaminifu na mzoefu anakupeleka kwa tajiri wake na anamwambia "Sudi amenyooka hana shida" basi wewe njia nyeupe kuchukua mali kwa tajiri wa Jose. Ni kama kujiunga na kilinge cha wachawi, huna mdhamini itaonekana we mlokole tu.
Kuna njia nyingi, sana mkuu... hili la kupelekwa ubebe mzigo ukauze ni steji nyingine kabisa. Hapa tunatka yule anayejitoa mwemyew kwenda kuanza. Mm nikupeleke nikakukabidhi kwa watu wanaoniamin wakuamin kama sikujui unadhan suala dogo?
 
Unataka kuuza madira/vijora.. haya ni mavitambaa tu. Haya ndio Tanzania ya viwanda mana wengi wanayashona palepale kariakoo mtaa wa tandamti na Nyamwezi. Wanayabeba na kuyapeleka mtaa wa raha na muhonda kuyauza. Bei yao ni common sana elf 5, 6 mengine 11, 12 mpaka elfu 9. Hapa si sana kukuta mawinga mana bei yake inaeleweka na maua yanatoka mapya kila wiki

10. Unatak kuuza tishti kali pia, jitadi kutofautisha brands.. kwa kariakoo brand kali zaidi ni Unkut, na Converse mana hazina ujinga ujinga sana. Ingawa balenciaga, Nike na jezi zinajitahid kusimamisja ubora. Unkut grade 1 ni elf 16 mpaka 15 mawinga wanauzaga 20 ni tishet kali sana.. ukifika kariakoo mtafte "mkombozi store" mchikichi na Congo

Unkut nafuu ni elf 9 bei ya jumla ambayo ni grade 2, pia kuna Converse wanauza 12 mpka 13. Sports na twist kwa ajili ya kuprint ni elf 6 mpaka 7500. Mawinga kwa mizigo mikubwa wanaongezaga bukubuku tu. Mtej akichukua nguo 100 unakula laki moja chap tunakukuta kidimbwi
 
Back
Top Bottom