Namna 'Royal Tour' ilivyoikoa sekta ya utalii kutoka ICU

Namna 'Royal Tour' ilivyoikoa sekta ya utalii kutoka ICU

Md Gertrude unayosema ni kweli tupu, ila kuna kitu kidogo naomba lukusaidia.

Si wewe tu, wengi hawajui kwamba Mlima Kilimanjaro is the highest FREESTANDING mountain IN THE WORLD.

Ni kwamba mlima unaanzia huku chini Rundgai huku chini kupitia Kinong'oto hadi Lukani, hapo ndiyo unaanza kuupanda hadi Uhuru Peak. Hii ni njia iitwayo Lukani Route, kuna zingine za Marangu au Kiruru au YMCA pale mjini, ila best ni hii ya kwetu Lukani Route kwa Mbunge Mbowe.

Habari ya Mlima huu imekaa vizuri kwenye wimbo wa TYL:

SISI TUNATAKA KUWASHA MWENGE, TUNATAKA KUWASHA MWENGE. NA KUUWEKA JUU YA MLIMA, MLIMA KILIMANJARO*

Twende polepole, kuna wanaharakati huku ndani, Activists, watakwambia eti Mlima Everest ndiyo mrefu kuliko yote, ukifuatiwa na K2 na Qongrong za Tibet.

Hii si kweli. Mount Evarist is a series ofsmallsmall hills from Saudi Arabia and Afghanistan through Pakistan and Indian Kashmir, each on top of the other, hadi kileleni. Ndiyo maana the second and third highest (hiyo K2 na Qonrong, actually ni vilima vinatizamana kama sisi huku tuba Kibo na Mawenzi, eti kila kimoja ujitegemee.

Ni hayo tu.

Changamoto moja tunapata wapandamlima ni vyoo (loos, (toilets) As you know, njia nyepesi kwa Kitanzania ni kuchimba dawa, hawa tunafanya hivyo kwetu Meatu ukitoka nje ya mji, Tanganyika Bus husimama pembeni mnapewa dakika tano.

Mlima Kilimanjaro huwezi kuchimba dawa kwa sababu haitokauka, if you see what I mean. Any suggestions? Hapo ndiyo ndugu zetu diaspora wangetusaidia (badala ya kuomba passport waliyoikana): wangetufanyia utafiti huko Ulaya na Marekani wao hujimbaje dawa zao? Huwa zinakaugaga? How? Tukipata jibu itaokoa Mlima wetu ubaki kuwa the highest and cleanest reestandi mountain in the world.

UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI. PALE AMBAPO HAKUNA MATUMAINI, UPENDO MAHALA AMBAPO PANA CHUKI, HESHIMA AMBAPO PAMEJA DHARAU.

Mama karuhusu maandamano napendekekeza pawe na sharti la kila chama kuimba huu wimbo katikati ya hutuba, baada ya kuanza lakini kabla ya kumaliza

ZFZMWCCM
Hiyo elevetion ya mlima ndivyo inavyopatikana ndg msomi?

Elimu ya shule gani hii?
 
Kitu kama hujui unyamaze
Swiss wanatangaza Alps mountain
South Africa wanatumia mamilioni kuutangaza "Table Mountain"...
Leo hii watalii wanaoenda Table Mountain ni Wengi kuliko wanaoenda mount Kilimanjaro....

Muachage ujujaji Kwa vitu hamna uelewa navyo
Bajeti yao kutangaza mlima ni kiasi gani kwa mwaka?

Na wana tqngazia wapi ndugu mtaalamu?
 
[emoji23] Africa bwana. Utalii wa asili unajitangaza wenyewe ila leo mtu anajitokeza kuforce hapa.
Nakuuliza maswali haya !
Mlima mkubwa hupo wapi africa!
ina maana dunia nzima kwa karne hii atangaze mtu mmoja ndio utalii unaongezeka
Acha wivu, watangulizi wote hawakuweza hili alilofanya Dr Samia, "mlima everest upo katika safu ya milima himalaya, lakini juhudi zinatakiwa ili kunivutia niende" unabakia kusema, utalii wa ashili unajitangasha wenyewe, watu wengine mnastahiki kupigiwa mambata ili akili ziamke.
 
Kenya ambao hawajafanya ROYAL tuwa kasi ya ukuaji wa utalii wao ikoje, Vipi kuhusu ukuaji wa utalii wa EGYPT ambao hawajafanya ROYAL tuwa?

GUINEA je, utalii wao umekuwaje. Kweli wewe ndugu umefanya comparison analysis katika kujadili hoja yako?
Kwa kile nilichokusudia kuandika, sikuwa na ulazima wa kufanya comparison analysis. Lengo langu liko wazi kabisa, kuonesha tu Royal Tour imeleta mafanikio gani kwenye sekta ya utalii nchini.

Kuonesha comparison ni study mpya kabisa ambayo naweza kufanya hivyo siku nyingine, ila kwa hilo ambalo mimi nimeandika, ni kuonesha tu impact ya Royal Tour basi.

Naamini tumeelewana, kutokakufanya comparison analyisis haifanyi taarifa yangu kuwa invalid. Kukiwa na ufafanuzi zaidi niite, sitochoka.
 
Mwaka 2022 sekta ya utalii nchi iliimarika zaidi baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kucheza na kuzindua filamu ya Tanzania: Royal Tour.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Taifa letu, ambapo Rais anacheza filamu nzima, tena kama muhusika mkuu katika harakati za kuendeleza sekta ya utalii.

Katika ya utalii ni sekta ni muhimu sana kwenye uchumi wa Taifa letu, ni sekta ya kuvalia njuga hasa kwani ni sekta ambayo inaliingizia Taifa dola bilioni 2 za kimarekani kwa mwaka, sawa ni Tsh trilioni 4.6 za kitanzania.

Kupitia filamu hii, Tanzania itazamia kupokea watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025 kutoka watalii takribani milioni mbili kwa sasa. Pia Tanzania inategemea kuingia USD bilioni 6 kwa mwaka, sawa na Tsh 13.8 za kitanzania kwa mwaka, kutoka trilioni 4.6 kwa sasa.

Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonesha kati ya Jan - Oct 2022 watalii 1,175,697 wameingia nchini, tofauti na watalii 716,741 wa kipindi kama hicho mwaka 2021, ambapo ongezeko hilo ni sawa na 64%.

NBS inasadiki ya kwamba ongezeko la watalii nchini ni matokeo ya filamu ya Royal Tour, mfano kwa mwezi Octoba 2022 tu, walii walioingia nchini walikuwa ni 141,517 tofauti na 92,345 kipindi kama hicho 2021, ambapo ni sawa na 53.2%.

Kutoka Ulaya, Tanzania imepokea watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa (12,553), Marekani (9,097), Germany 98,874), UK (6,614) na Italy (4,557).

Watalii hao katika mahojiano mbalimbali wakisadiki ya kwamba wao ni mara ya kwanza kuingia Tanzania, na wamevutiwa zaidi kutembelea Tanzania baada ya kutazama filamu ya Royal Tour.

Filamu ya Royal Tour bado inazidi kuoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mataifa mbalimbali, huko mabalozi wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha hilo. Sept 2022 ilioneshwa Sweden, na inazidi kuoneshwa zaidi kwenye nchi za Scandinavia.

Pia inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye nchi kama Latvia, Finland, Denmark, Iceland, Lithuania, Estonia na nyingine nyingi za bara la Ulaya.

Filamu ya Royal Tour ni legacy ya Rais Samia Suluhu itakayoishi milele, faida zake hazitoishia kwakwe tu, bali hata kwa viongozi wajao, watakuwa na wepesi katika kuutangaza utalii wetu, kwani barabara imara itakuwa tayari imeshachongwa mtangulizi wao, Mh Rais Samia Suluhu.
Wewe ndiyo juzi ulikuwa unasema vijana wanasiasa uwezo wao wa kujenga hoja ni mdogo,sasa wewe hapa unafanya nini?

Unasema inasadikika ongezeko la watalii walimechangiwa na filamu ya royal tour!!how?

Ni lini ilifanyika assessment ya filamu ya Royal Tour ili tujue kuwa watalii wamepata taarifa ya vivutio vyetu kutokana na filamu husika?

Mtaalamu wa kujenga hoja unaleta hadithi za kusadikika jukwaani[emoji1787][emoji1787]
 
Kama umetazama Royal Tour kwenye Amazon+ ukasoma na reviews, ndio utajua namna gani watu wamevutika kuja Tanzania baada ya Royal Tour. Bila kificho tena kwa facts kabisa, Royal Tour imesaidia sana kuongeza idadi ya watalii, kuna ongezeko la asilimia zaidi ya 60% kati ya Jan - Oct 2022, sasa hapo unataka kusema wote hao wali book kabla?
Weka assessment report ya impact ya Royal Tour Film tuione.
 
Kama mambo yote ni bam bam kwanini bado tulia na kutoka machozi ya damu ?

Royal Tour haikuwa kutangaza nchi bali mtawala..., Just a Promo like any other Promo hilo ni moja mbaya zaidi tunaendelea kutumia rasilimali kuintangaza hiyo Royal Tour badala ya Utalii wenyewe....

Tangazo la Tangazo linatangazwa zaidi ya Tangazo Lenyewe....
 
Research? We unajua kweli maana ya research. Takwimu zinatolewa kila mara na mamlaka halali za serikali research gani tena wakati data tunapewa. Hata we ukihitaji ku-prove nenda kwenye maeneo yenye circuit za utalii ujionee yaani hiyo itakuwa mojawapo ya data collectio tool. ubishi usio na msingi ni sifa mbaya sana get rid of it.
Sijui anatuonaje,yaani kukusanya secondary data za NBS,eti ndiyo kafanya utafiti[emoji1787][emoji1787][emoji1787].Sasa yeye na NBS nani kafanya utafiti!!
Makada wa mbogamboga wana matatizo sana!
 
National Bureau of Statistics hawana fact kamili za vyanzo vya wageni.
Wao wanakokotoa kutoka kwenye entry points za wageni kama airports na border points.

Hawawezi kujua rasmi nini chanzo cha connection ya hao wageni.

Mtu anayefanya kwenye sekta husika anao uelewa mkubwa wa haya mambo kuliko hao NBS wako,ambao hata Zitto alikwisha waumbua.

Issue hapa sio Wingi wa wageni,bali chanzo cha wageni.

Haiwezekani nchi imejaa waisrael,wajerumani,wafaransa na waingereza kiduchu na hao Americans.
Wewe ukimbilie kuiunganisha na Royal Tour yenu.

Kwanza Royal Tour ili fail ku- perform sababu mama yenu aliacha wataalamu nyuma akajaza kina Abbas,Msigwa na Yunus.
Badala ya watu wa "Mweka College of African Wildlife Management" na "TATO"

Badala ya kwenda na wadau wenyewe wamsaidie kwenye Interview za Royal Tour kwenye zinduzi zake.

Punguzeni U-chawa jamani.

Wakati mnaisifia Royal Tour,unajua hali ya miundombinu ya barabara ilivyoharibika huko mbugani huku serikali ikikaa kimya.

Unajua hata idadi ya watalii waliopoteza maisha yao mpaka sasa kutokana na ajali za Barabarani kutokana na ubovu wake.
Hasa Serengeti?
Hii hoja yako imeweka uchi kabisa itikadi yako na pia hisia zako juu ya Rais Samia Suluhu. Ila tukiachana na hayo, naomba niende moja kwa moja kwenye kutoa majibu kwenye hoja zako pasi na kutaka kuingia ndani kwenye itikadi wala hisia zako, hayo yako nje ya uwezo wangu, ila kwa baadhi ya hoja zako, nakujibu kama ifuatavyo.

1. NBS ndio taasisi ya juu zaidi nchi mwetu inayohusika na masuala ya takwimu, na NBS ina uwezo wa kuomba data kutoka entry points zote za migrations nchini kwa minajili ya kuchakata taarifa zake. Wageni waingiapo nchi huja kwa sababu mbalimbali, hii inabainishwa hasa kwenye VISA zao. Yaani, wapo wanoomba VISA za biashara, matembezi na kazi, na wapo wanaosema wanakuja kwa ajili ya utalii. Hapa NBS inapata taarifa za watu hawa kirahisi kabisa. Sasa kama unataka kupingana na data za NBS itakupasa uje na data zako, ufanye utafiti wako ili uweze kuwa objective, otherwise itakuwa unapiga tu kelele kama ulivyofanya hapo juu.

2. Royal Tour haikufeli, Royal Tour imefanya vizuri sana. Kutokuwaweka hao Mweka na taasisi zingine za utalii haifanyi Royal Tour kutofanya vizuri, ndani ya mwezi mmoja, tayari ilishatazamwa mara milioni zaidi ya 50 pekee kwenye mtandao wa Amazon. Niseme tu, Royal Tour ilikwenda kama ilivyopangwa, na kama mpango ulienda sahihi, basi hayo ni mafanikio. Sasa kama imefeli kwa mtazamo wako, tuanza kuangalia tasfiri yako ya mafanikio, pengine haikufanikiwa, ila kwa mawazo yako, ila sio ya kwao.

3. Mbuga kuwa na barabara mbovu sio shida, of couse mbuga zinapaswa kuwa katika hali yake ya uhalisia, unataka serikali iweke lami mbugani au? Haya, kama barabara zetu ni mbovu, why bado Tanzania inangia kati ya nchi bora za kutembea duniani kila mwaka na inapata tuzo kwa kuwa na vivutio bora vya utalii kila mwaka.

4. Watalii hufa kila sehemu, nikisoma wanaopanda Mlima Evarest wanakufa wengine, ukiangalia wanaotembelea victoria falls wanakufa wengine, ukitazama wanaotembelea Kruger Afrika Kusinia wanakufa wengine. Kufa kwa watalii sio suala la Serikali, serikali inajitahidi kadiri iwezavyo kulinda maisha ya watalii, ila suala la kifo liko nje ya uwezo wa serikali yoyote. So I suggest tafuta namna nyingine ya kukosa, au suggest njia ya kuzuia vifo kama unayo.
 
Bora ungetafuta cha kuandika badala ya huu uchawa usio na ukweli hata 25%!

Sekta ya utalii ilifunguka baada ya Covid19 kupunguza makali yake!

Na hapo awali wageni wengi walikwishalipia safari zao,kabla ya katizo la covid19.

Hivyo ilipofunguka wote walimiminika kuja nchini wakiwa katika makundi mawili.ambayo ni..
Wale waliokuwa wamelipa awali bila kuchukuwa pesa zao.
Na wale waliokuwa wanakuja kurekebisha akili zao baada ya quarantine ya muda mrefu huko makwao.

Mataifa yaliyoongoza kwa kuja nchini ikuwa ni Russia na Ukraine kabla ya vita kuanza.

Na hata ushahidi ni pale baadhi yao walipokwama Zanzibar kwa miezi kadhaa baada ya vita kuanza huko Ukraine.

Mpaka Royal tour inazinduliwa na Peter huko USA. Warusi na wa Ukraine walikuwa wakiendelea kumwagika.

Kundi la pili ni la Waisrael wa kundi la "Shromo" almaarufu kama "Another World" wao mpaka sasa wanaendelea kuja na madege yao yakiwasubiri pale KIA.

Hiyo Impact yako ya Royal Tour sijui umeitolea wapi?

TTB wao wanatoa rekodi bila kutaja vyanzo vya wageni hao,ukiwa ni mtindo endelevu wa uchawa uliokomaa nchi hii.

Mpaka sasa mataifa yanayoongoza kwa kuingiza wageni nchi sio Marekani.

Ni wajerumani, waspanniola,na mataifa mengineyo.

Ukitaka Data za ukweli nenda kwa Tour Operators watakueleza na kukusaidia ili ukamilishe azna yako.

Getrude Mollel Njoo tukutane kule Ngoitoktok Picnic Site nikupe Data vizuriView attachment 2472024
Nimeisoma hoja yako imejaa hisia tu, haina fact hata moja. Mimi nimeandika baada ya kusoma ripoti ya NBS, itafute kwenye website yao uisome na wewe next time uache kuandika kwa mihemko. Tuambie kati ya watalii milioni 1.1 walioingia Tanzania kati ya Jan - Oct 2022, ni wangapi walibook kabla ya Kovid-19? Wengi humu kwa sababu tu wanafanya kazi kwenye kampuni ya utalii wamejipa mamlaka ya kuzungumzia sekta ya utalii hata kama hawa facts za msingi za kutetea hoja zao. Ujinga sana.
 
Akili za watu kama wewe ndo hatari sana...Dubai wanatumia dollars milioni zaidi ya 50 kila mwaka kuitangaza nchi .. unafikiri wao wajinga? Si kila mtu anaijua Dubai?

unakosea sana.Dubai wanatumia pesa nyingi kuijenga na kuvutia wawekezaji sababu ni jangwa.
hapa kwako kuna jangwa mpaka kuforce
 
Nimeisoma hoja yako imejaa hisia tu, haina fact hata moja. Mimi nimeandika baada ya kusoma ripoti ya NBS, itafute kwenye website yao uisome na wewe next time uache kuandika kwa mihemko. Tuambie kati ya watalii milioni 1.1 walioingia Tanzania kati ya Jan - Oct 2022, ni wangapi walibook kabla ya Kovid-19? Wengi humu kwa sababu tu wanafanya kazi kwenye kampuni ya utalii wamejipa mamlaka ya kuzungumzia sekta ya utalii hata kama hawa facts za msingi za kutetea hoja zao. Ujinga sana.

NBS wanaangalia border za kuingilia watalii, fact zao zinatoka huko

ila sasa kuna watu ambao wao ndio wanakaa na wageni au wageni wanafanya reservation kupitia wao, so wanajua in details hao wageni walipanga lini kuja so hapo usiwe mbishi

royo tour movies ingefanya vizuri then wageni kutoka US wangekuwa ni wengi zaid coz hata tuliamua kuizindua US ni kupata so la Marekani

but angalia wageni wengi ambao wamekuja ni wa wapi?

Ulaya, Russia, Israel na US kidogo sasa una fact gani ya Uhalisia kusema Royo Tour Documentary imefanya vizuri?

nilishiriki kwenye Royo Tour so najua naongea nn
 
Mwaka 2022 sekta ya utalii nchi iliimarika zaidi baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kucheza na kuzindua filamu ya Tanzania: Royal Tour.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Taifa letu, ambapo Rais anacheza filamu nzima, tena kama muhusika mkuu katika harakati za kuendeleza sekta ya utalii.

Katika ya utalii ni sekta ni muhimu sana kwenye uchumi wa Taifa letu, ni sekta ya kuvalia njuga hasa kwani ni sekta ambayo inaliingizia Taifa dola bilioni 2 za kimarekani kwa mwaka, sawa ni Tsh trilioni 4.6 za kitanzania.

Kupitia filamu hii, Tanzania itazamia kupokea watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025 kutoka watalii takribani milioni mbili kwa sasa. Pia Tanzania inategemea kuingia USD bilioni 6 kwa mwaka, sawa na Tsh 13.8 za kitanzania kwa mwaka, kutoka trilioni 4.6 kwa sasa.

Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonesha kati ya Jan - Oct 2022 watalii 1,175,697 wameingia nchini, tofauti na watalii 716,741 wa kipindi kama hicho mwaka 2021, ambapo ongezeko hilo ni sawa na 64%.

NBS inasadiki ya kwamba ongezeko la watalii nchini ni matokeo ya filamu ya Royal Tour, mfano kwa mwezi Octoba 2022 tu, walii walioingia nchini walikuwa ni 141,517 tofauti na 92,345 kipindi kama hicho 2021, ambapo ni sawa na 53.2%.

Kutoka Ulaya, Tanzania imepokea watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa (12,553), Marekani (9,097), Germany 98,874), UK (6,614) na Italy (4,557).

Watalii hao katika mahojiano mbalimbali wakisadiki ya kwamba wao ni mara ya kwanza kuingia Tanzania, na wamevutiwa zaidi kutembelea Tanzania baada ya kutazama filamu ya Royal Tour.

Filamu ya Royal Tour bado inazidi kuoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mataifa mbalimbali, huko mabalozi wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha hilo. Sept 2022 ilioneshwa Sweden, na inazidi kuoneshwa zaidi kwenye nchi za Scandinavia.

Pia inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye nchi kama Latvia, Finland, Denmark, Iceland, Lithuania, Estonia na nyingine nyingi za bara la Ulaya.

Filamu ya Royal Tour ni legacy ya Rais Samia Suluhu itakayoishi milele, faida zake hazitoishia kwakwe tu, bali hata kwa viongozi wajao, watakuwa na wepesi katika kuutangaza utalii wetu, kwani barabara imara itakuwa tayari imeshachongwa mtangulizi wao, Mh Rais Samia Suluhu.
2019 kulikuwa na Idadi kubwa ya Watalii
 
unakosea sana.Dubai wanatumia pesa nyingi kuijenga na kuvutia wawekezaji sababu ni jangwa.
hapa kwako kuna jangwa mpaka kuforce
Kwenye mambo ambayo hamna utaalam nayo muwe mnanyamaza kimya na kujifunza...
Hiko kipindi cha Royal tour ndo kimesababisha Rwanda wapate watalii Wengi kuliko Zanzibar..

Mnafikiri Rwanda wapumbavu kulipa hela PSG na Arsenal kuitangaza nchi Yao?...
Rais wa Tz Samia Hakukurupuka kuandaa hiko kipindi ..kashauriwa na wataalam wanaojua biashara ya utalii...muwe mnapinga vitu ambavyo mna uelewa navyo
 
Back
Top Bottom