Namna 'Royal Tour' ilivyoikoa sekta ya utalii kutoka ICU

kaka hapa ni africa tena africa ya tanzania, achana na hizo taasisi za data kama una jambo lako serious,

nenda site, fanya mwenyewe kwa sample zako,

taasisi nyingi zinafanya kazi kwa kufurahisha viongozi na sio uhalisia

rudi kwenye hizi mambo za research wakati wa magufuli je kulikuwa na uhalisia?

watu wanakaa na wageni, watu wana connection na wageni watu wanajua mambo meeeeeeengi na changamoto nyingi kuliko hao watu wa data
Wewe mpuuzi
 
Kwa kile nilichokusudia kuandika, sikuwa na ulazima wa kufanya comparison analysis. Lengo langu liko wazi kabisa, kuonesha tu Royal Tour imeleta mafanikio gani kwenye sekta ya utalii nchini.

Kuonesha comparison ni study mpya kabisa ambayo naweza kufanya hivyo siku nyingine, ila kwa hilo ambalo mimi nimeandika, ni kuonesha tu impact ya Royal Tour basi.

Naamini tumeelewana, kutokakufanya comparison analyisis haifanyi taarifa yangu kuwa invalid. Kukiwa na ufafanuzi zaidi niite, sitochoka.
Kenya na Egypt, walishajitangaza kwa nguvu kubwa wakati huo Tanzania ikiwa imelala fofofo, Kiongozi wa Tanzania ambaye amesimama seriously kunyanyua sector hii kwa dhati ni Dr. Samia.
 
..mpaka sasa hivi Royal Tour Tanzania imeangaliwa na watu wangapi?

..pia umesema hivi tunavyozungumza Royal Tour inaonyeshwa ktk kumbi za senema.

..Je mapato kiasi gani yamepatikana kwa kuonyesha senema hiyo?

..Senema yoyote ile lazima ijulikane imeangaliwa na watu wangapi, na imeingiza mapato kiasi gani.
Mara nyingi documentary huwa ni kama aina fulani ya ufundishaji, au uonyeshaji aidha utangazaji wa jambo lililokuwa pengine haijulikani kwa mapana.
 
Jambo gani pale lilikuwa halijulikani Kwa mapana?
 
Mwaka 2022 sekta ya utalii nchi iliimarika zaidi baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kucheza na kuzindua filamu ya Tanzania: Royal Tour.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Taifa letu, ambapo Rais anacheza filamu nzima, tena kama muhusika mkuu katika harakati za kuendeleza sekta ya utalii.

Katika ya utalii ni sekta ni muhimu sana kwenye uchumi wa Taifa letu, ni sekta ya kuvalia njuga hasa kwani ni sekta ambayo inaliingizia Taifa dola bilioni 2 za kimarekani kwa mwaka, sawa ni Tsh trilioni 4.6 za kitanzania.

Kupitia filamu hii, Tanzania itazamia kupokea watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025 kutoka watalii takribani milioni mbili kwa sasa. Pia Tanzania inategemea kuingia USD bilioni 6 kwa mwaka, sawa na Tsh 13.8 za kitanzania kwa mwaka, kutoka trilioni 4.6 kwa sasa.

Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonesha kati ya Jan - Oct 2022 watalii 1,175,697 wameingia nchini, tofauti na watalii 716,741 wa kipindi kama hicho mwaka 2021, ambapo ongezeko hilo ni sawa na 64%.

NBS inasadiki ya kwamba ongezeko la watalii nchini ni matokeo ya filamu ya Royal Tour, mfano kwa mwezi Octoba 2022 tu, walii walioingia nchini walikuwa ni 141,517 tofauti na 92,345 kipindi kama hicho 2021, ambapo ni sawa na 53.2%.

Kutoka Ulaya, Tanzania imepokea watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa (12,553), Marekani (9,097), Germany 98,874), UK (6,614) na Italy (4,557).

Watalii hao katika mahojiano mbalimbali wakisadiki ya kwamba wao ni mara ya kwanza kuingia Tanzania, na wamevutiwa zaidi kutembelea Tanzania baada ya kutazama filamu ya Royal Tour.

Filamu ya Royal Tour bado inazidi kuoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mataifa mbalimbali, huko mabalozi wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha hilo. Sept 2022 ilioneshwa Sweden, na inazidi kuoneshwa zaidi kwenye nchi za Scandinavia.

Pia inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye nchi kama Latvia, Finland, Denmark, Iceland, Lithuania, Estonia na nyingine nyingi za bara la Ulaya.

Filamu ya Royal Tour ni legacy ya Rais Samia Suluhu itakayoishi milele, faida zake hazitoishia kwakwe tu, bali hata kwa viongozi wajao, watakuwa na wepesi katika kuutangaza utalii wetu, kwani barabara imara itakuwa tayari imeshachongwa mtangulizi wao, Mh Rais Samia Suluhu.
Si bezi Juhudi za Mh. Rais kutangaza utalii. Inawezekana Royal tour imechangia au itachingia ujio wa watalii siku zijazo, ila ongezeka la watalii mwaka 2022 ni kutokana na kiwa watu wengi walikuwa wamejifungia ndani kutokana na janga la COVID na pia wengine walikuwa wame cancell safari zao. Hivyo baada ya kufunguliwa wengi waliona wanahitaji kutoka na wale bao walikuwa wame cancel safari zao walikuja maana wengine walisha lipia.

Ni hayo tu
 
Mara nyingi documentary huwa ni kama aina fulani ya ufundishaji, au uonyeshaji aidha utangazaji wa jambo lililokuwa pengine haijulikani kwa mapana.

..mtoa mada amesema Royal Tour inaonyeshwa ktk majumba ya senema ktk nchi mbalimbali.

..kama ni hivyo anatakiwa atueleze senema hiyo imeangaliwa na watu wangapi.

..pia atueleze senema hiyo imeingiza mapato kiasi gani. Na Tanzania tumepata kiasi gani.
 
Africa bwana. Utalii wa asili unajitangaza wenyewe ila leo mtu anajitokeza kuforce hapa.
siyo kweli kabisa kabisa. Ingekuwa ni hivyo Kenya wasingetupita kimapato ya utalii wakati sisi ndiyo wenye vivutio vingi vya asili.

Hata huo mlima unaojisifia wazungu walikuwa wanajua uko Kenya na siyo Tanzania.
 
Mwaka 2022 sekta ya utalii nchi iliimarika zaidi baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kucheza na kuzindua filamu ya Tanzania: Royal Tour.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Taifa letu, ambapo Rais anacheza filamu nzima, tena kama muhusika mkuu katika harakati za kuendeleza sekta ya utalii.

Katika ya utalii ni sekta ni muhimu sana kwenye uchumi wa Taifa letu, ni sekta ya kuvalia njuga hasa kwani ni sekta ambayo inaliingizia Taifa dola bilioni 2 za kimarekani kwa mwaka, sawa ni Tsh trilioni 4.6 za kitanzania.

Kupitia filamu hii, Tanzania itazamia kupokea watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025 kutoka watalii takribani milioni mbili kwa sasa. Pia Tanzania inategemea kuingia USD bilioni 6 kwa mwaka, sawa na Tsh 13.8 za kitanzania kwa mwaka, kutoka trilioni 4.6 kwa sasa.

Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonesha kati ya Jan - Oct 2022 watalii 1,175,697 wameingia nchini, tofauti na watalii 716,741 wa kipindi kama hicho mwaka 2021, ambapo ongezeko hilo ni sawa na 64%.

NBS inasadiki ya kwamba ongezeko la watalii nchini ni matokeo ya filamu ya Royal Tour, mfano kwa mwezi Octoba 2022 tu, walii walioingia nchini walikuwa ni 141,517 tofauti na 92,345 kipindi kama hicho 2021, ambapo ni sawa na 53.2%.

Kutoka Ulaya, Tanzania imepokea watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa (12,553), Marekani (9,097), Germany 98,874), UK (6,614) na Italy (4,557).

Watalii hao katika mahojiano mbalimbali wakisadiki ya kwamba wao ni mara ya kwanza kuingia Tanzania, na wamevutiwa zaidi kutembelea Tanzania baada ya kutazama filamu ya Royal Tour.

Filamu ya Royal Tour bado inazidi kuoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mataifa mbalimbali, huko mabalozi wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha hilo. Sept 2022 ilioneshwa Sweden, na inazidi kuoneshwa zaidi kwenye nchi za Scandinavia.

Pia inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye nchi kama Latvia, Finland, Denmark, Iceland, Lithuania, Estonia na nyingine nyingi za bara la Ulaya.

Filamu ya Royal Tour ni legacy ya Rais Samia Suluhu itakayoishi milele, faida zake hazitoishia kwakwe tu, bali hata kwa viongozi wajao, watakuwa na wepesi katika kuutangaza utalii wetu, kwani barabara imara itakuwa tayari imeshachongwa mtangulizi wao, Mh Rais Samia Suluhu.
Kwenye hili hata wale wanaobisha wanakubali kuwa mama ameupiga mwingi! HONGERA SANA MAMA KWA UBUNIFU HUU WENYE TIJA KWA NCHI YETU. UTAKUMBUKWA KWA VIZAZI NA VIZAZI NDANI NA NJE YA RAIFA LETU.
 
Back
Top Bottom