Namna 'Royal Tour' ilivyoikoa sekta ya utalii kutoka ICU

Hiyo elevetion ya mlima ndivyo inavyopatikana ndg msomi?

Elimu ya shule gani hii?
 
Bajeti yao kutangaza mlima ni kiasi gani kwa mwaka?

Na wana tqngazia wapi ndugu mtaalamu?
 
[emoji23] Africa bwana. Utalii wa asili unajitangaza wenyewe ila leo mtu anajitokeza kuforce hapa.
Nakuuliza maswali haya !
Mlima mkubwa hupo wapi africa!
ina maana dunia nzima kwa karne hii atangaze mtu mmoja ndio utalii unaongezeka
Acha wivu, watangulizi wote hawakuweza hili alilofanya Dr Samia, "mlima everest upo katika safu ya milima himalaya, lakini juhudi zinatakiwa ili kunivutia niende" unabakia kusema, utalii wa ashili unajitangasha wenyewe, watu wengine mnastahiki kupigiwa mambata ili akili ziamke.
 
Kenya ambao hawajafanya ROYAL tuwa kasi ya ukuaji wa utalii wao ikoje, Vipi kuhusu ukuaji wa utalii wa EGYPT ambao hawajafanya ROYAL tuwa?

GUINEA je, utalii wao umekuwaje. Kweli wewe ndugu umefanya comparison analysis katika kujadili hoja yako?
Kwa kile nilichokusudia kuandika, sikuwa na ulazima wa kufanya comparison analysis. Lengo langu liko wazi kabisa, kuonesha tu Royal Tour imeleta mafanikio gani kwenye sekta ya utalii nchini.

Kuonesha comparison ni study mpya kabisa ambayo naweza kufanya hivyo siku nyingine, ila kwa hilo ambalo mimi nimeandika, ni kuonesha tu impact ya Royal Tour basi.

Naamini tumeelewana, kutokakufanya comparison analyisis haifanyi taarifa yangu kuwa invalid. Kukiwa na ufafanuzi zaidi niite, sitochoka.
 
Wewe ndiyo juzi ulikuwa unasema vijana wanasiasa uwezo wao wa kujenga hoja ni mdogo,sasa wewe hapa unafanya nini?

Unasema inasadikika ongezeko la watalii walimechangiwa na filamu ya royal tour!!how?

Ni lini ilifanyika assessment ya filamu ya Royal Tour ili tujue kuwa watalii wamepata taarifa ya vivutio vyetu kutokana na filamu husika?

Mtaalamu wa kujenga hoja unaleta hadithi za kusadikika jukwaani[emoji1787][emoji1787]
 
Weka assessment report ya impact ya Royal Tour Film tuione.
 
Kama mambo yote ni bam bam kwanini bado tulia na kutoka machozi ya damu ?

 
Royal Tour haikuwa kutangaza nchi bali mtawala..., Just a Promo like any other Promo hilo ni moja mbaya zaidi tunaendelea kutumia rasilimali kuintangaza hiyo Royal Tour badala ya Utalii wenyewe....

Tangazo la Tangazo linatangazwa zaidi ya Tangazo Lenyewe....
 
Sijui anatuonaje,yaani kukusanya secondary data za NBS,eti ndiyo kafanya utafiti[emoji1787][emoji1787][emoji1787].Sasa yeye na NBS nani kafanya utafiti!!
Makada wa mbogamboga wana matatizo sana!
 
Hii hoja yako imeweka uchi kabisa itikadi yako na pia hisia zako juu ya Rais Samia Suluhu. Ila tukiachana na hayo, naomba niende moja kwa moja kwenye kutoa majibu kwenye hoja zako pasi na kutaka kuingia ndani kwenye itikadi wala hisia zako, hayo yako nje ya uwezo wangu, ila kwa baadhi ya hoja zako, nakujibu kama ifuatavyo.

1. NBS ndio taasisi ya juu zaidi nchi mwetu inayohusika na masuala ya takwimu, na NBS ina uwezo wa kuomba data kutoka entry points zote za migrations nchini kwa minajili ya kuchakata taarifa zake. Wageni waingiapo nchi huja kwa sababu mbalimbali, hii inabainishwa hasa kwenye VISA zao. Yaani, wapo wanoomba VISA za biashara, matembezi na kazi, na wapo wanaosema wanakuja kwa ajili ya utalii. Hapa NBS inapata taarifa za watu hawa kirahisi kabisa. Sasa kama unataka kupingana na data za NBS itakupasa uje na data zako, ufanye utafiti wako ili uweze kuwa objective, otherwise itakuwa unapiga tu kelele kama ulivyofanya hapo juu.

2. Royal Tour haikufeli, Royal Tour imefanya vizuri sana. Kutokuwaweka hao Mweka na taasisi zingine za utalii haifanyi Royal Tour kutofanya vizuri, ndani ya mwezi mmoja, tayari ilishatazamwa mara milioni zaidi ya 50 pekee kwenye mtandao wa Amazon. Niseme tu, Royal Tour ilikwenda kama ilivyopangwa, na kama mpango ulienda sahihi, basi hayo ni mafanikio. Sasa kama imefeli kwa mtazamo wako, tuanza kuangalia tasfiri yako ya mafanikio, pengine haikufanikiwa, ila kwa mawazo yako, ila sio ya kwao.

3. Mbuga kuwa na barabara mbovu sio shida, of couse mbuga zinapaswa kuwa katika hali yake ya uhalisia, unataka serikali iweke lami mbugani au? Haya, kama barabara zetu ni mbovu, why bado Tanzania inangia kati ya nchi bora za kutembea duniani kila mwaka na inapata tuzo kwa kuwa na vivutio bora vya utalii kila mwaka.

4. Watalii hufa kila sehemu, nikisoma wanaopanda Mlima Evarest wanakufa wengine, ukiangalia wanaotembelea victoria falls wanakufa wengine, ukitazama wanaotembelea Kruger Afrika Kusinia wanakufa wengine. Kufa kwa watalii sio suala la Serikali, serikali inajitahidi kadiri iwezavyo kulinda maisha ya watalii, ila suala la kifo liko nje ya uwezo wa serikali yoyote. So I suggest tafuta namna nyingine ya kukosa, au suggest njia ya kuzuia vifo kama unayo.
 
Nimeisoma hoja yako imejaa hisia tu, haina fact hata moja. Mimi nimeandika baada ya kusoma ripoti ya NBS, itafute kwenye website yao uisome na wewe next time uache kuandika kwa mihemko. Tuambie kati ya watalii milioni 1.1 walioingia Tanzania kati ya Jan - Oct 2022, ni wangapi walibook kabla ya Kovid-19? Wengi humu kwa sababu tu wanafanya kazi kwenye kampuni ya utalii wamejipa mamlaka ya kuzungumzia sekta ya utalii hata kama hawa facts za msingi za kutetea hoja zao. Ujinga sana.
 
Akili za watu kama wewe ndo hatari sana...Dubai wanatumia dollars milioni zaidi ya 50 kila mwaka kuitangaza nchi .. unafikiri wao wajinga? Si kila mtu anaijua Dubai?

unakosea sana.Dubai wanatumia pesa nyingi kuijenga na kuvutia wawekezaji sababu ni jangwa.
hapa kwako kuna jangwa mpaka kuforce
 

NBS wanaangalia border za kuingilia watalii, fact zao zinatoka huko

ila sasa kuna watu ambao wao ndio wanakaa na wageni au wageni wanafanya reservation kupitia wao, so wanajua in details hao wageni walipanga lini kuja so hapo usiwe mbishi

royo tour movies ingefanya vizuri then wageni kutoka US wangekuwa ni wengi zaid coz hata tuliamua kuizindua US ni kupata so la Marekani

but angalia wageni wengi ambao wamekuja ni wa wapi?

Ulaya, Russia, Israel na US kidogo sasa una fact gani ya Uhalisia kusema Royo Tour Documentary imefanya vizuri?

nilishiriki kwenye Royo Tour so najua naongea nn
 
2019 kulikuwa na Idadi kubwa ya Watalii
 
unakosea sana.Dubai wanatumia pesa nyingi kuijenga na kuvutia wawekezaji sababu ni jangwa.
hapa kwako kuna jangwa mpaka kuforce
Kwenye mambo ambayo hamna utaalam nayo muwe mnanyamaza kimya na kujifunza...
Hiko kipindi cha Royal tour ndo kimesababisha Rwanda wapate watalii Wengi kuliko Zanzibar..


Mnafikiri Rwanda wapumbavu kulipa hela PSG na Arsenal kuitangaza nchi Yao?...
Rais wa Tz Samia Hakukurupuka kuandaa hiko kipindi ..kashauriwa na wataalam wanaojua biashara ya utalii...muwe mnapinga vitu ambavyo mna uelewa navyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…