Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali inayotokea hapa Jamii forum, kuhusu kutoonekana hadharani kwa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli kwa muda wa wiki mbili sasa toka Feb 27, 2021.
Mijadala hiyo imekuwa inanisikitisha, hasa kutoka kwa wapinzani wa serikali. Kinachonisikitisha, ni kuona wapinzani wa serikali ya JPM wanajiona wamesoma lakini, JPM anawachezesha ngoma ya mdundiko pasipo wao kujitambua. Kwanza nataka niwambie, ndugu zangu JPM yupo vizuri sana kiakili.
Ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa akili. Hii issue ameamua kuifanya kama issue ya kiongozi wa Korea Kusini,kwamba haonekani hadharani, lakini baadae ataonekana, na ataendelea na kazi kama kawaida.
Kinachosikitisha, ni kuona wapinzani kina Lissu wanakimbia na unspecified, rumors na speculation huku na huku. Oh, yupo Nairobi hospital. Oh sasa wanataka kumpeleka India. Yaan mnajishushia heshima Kabisa. Mnachezeshwa mdundiko bila nyie kujitambua. Yaan Lissu umejishushia heshima Kabisa.