Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Chumvi ya mawe kwa urahisi kabisa inapatikana kwenye maduka ya dawa za asili .
Miongoni mwa faida kuu ya chumvi ya mawe ni kukuondolea uchawi uliopo mwilini mwako, husuda na kama kuna milango ya ridhiki ilifungwa basi ukitumia chumvi ya mawe itakusaidia sana kufungua kifungo.
Cha kufanya loweka chumvi ya mawe kwenye ndoo unayokwenda kuogea , hakikisha ni usiku wa manane haswa kuanzia saa 7 usiku na kuendelea.
Hakikisha unaoga sehemu ya wazi (Usioge chooni) ,
Kabla ya kuoga nuia mambo yako , kama kuna husda yoyote uliyofanyiwa iondoke, uongeze mvuto wa kinyota /kiroho.
Oga kwa siku 7 mfululizo usiku wa manane.
Pia unaweza kutumia maji yenye chumvi ya mawe kudekia sehemu unapolala na kiasi kidogo cha chumvi ya mawe kumwagia mwagia kwenye kingo za nyumba yako.
Chumvi ya mawe inasaidia pia hata kwenye shughuli yako, ukitaka shughuli yako iondokane na nuksi ya aina yoyote basi mwagia chumvi ya mawe, pia unaweza ukaimwagia jikoni unapopikia chakula maana kuna watu wanaroga chakula kisiive ili kukuharibia shughuli.
Hili ni zindiko kubwa sana kiroho.
Unaweza kuongezea pia na dawa inaitwa Mzizima , hii itaenda kuzima uchawi wote uliofanyiwa mwilini mwako.
Mzizima unaweza kuogea muda wowote na pia unaweza kuchanganya na uji ukanywa pia.