Namna ya kupunguza upweke nyumbani

Namna ya kupunguza upweke nyumbani

Binadamu yeyote anahitaji kuwa na furaha, pamoja na kuzungukwa na watu mbali mbali ambao watamfanya achangamke na kuondoa au kupunguza tatizo la msongo wa mawazo.

Hii imekuwa ikitokea kwa baadhi ya familia, baada ya kukuza watoto wao na kwenda kujitegemea, na hatimaye kuwaacha wazazi wao wakiwa wapweke huku wakizungukwa na majengo au vyumba visivyokuwa na watu.

Njia ninazoweza kuwashauri jamii ya namna hii, kugawa kiwanja au jengo katika sehemu tatu; sehemu ya kwanza inaweza kutumiwa kama karakana ya kutengeneza vitu fulani n.k.

Sehemu ya pili itakuwa makazi ya familia, na sehemu ya tatu unaweza kuweka biashara yoyote iwe ni ya vinywaji n.k

Hii itasaidia kuwa na mzunguko mkubwa wa watu, na itapunguza uwezo wa mtu kukaa pekee yake pamoja na kuwepo kwa msongo wa mawazo.

Karibuni kwa hoja
Huu mwaka umegonga miaka mingapi kwani?
 
Mimi nyumbani kwangu eneo kubwa zaidi nimelitenga la viumbe hai (Nyumba imechukua robo ya eneo na the rest ni mimea na wanyama na ndege)
Kuna nyasi, migomba, miti ya matunda, miti ya vivuli, bustani za mboga na maua nimeanza kujenga mabanda mazuri kabisa ya kuku, bata, bata mzinga, sungura (hawa tayari wapo), mbwa tayari wapo pia, kuna kitenga vya kasuku pia na maboxi ya njiwa.
Mji wa aina hii bado ukiwa mpweke we tena basi!
Mana kuanzia asbh naamka ninatoka banda hili, naingia lile, naenda mgomba huu mara mpera ule.
Sijawahi hisi upweke nikiwa nyumbani!
 
Back
Top Bottom