Mimi nyumbani kwangu eneo kubwa zaidi nimelitenga la viumbe hai (Nyumba imechukua robo ya eneo na the rest ni mimea na wanyama na ndege)
Kuna nyasi, migomba, miti ya matunda, miti ya vivuli, bustani za mboga na maua nimeanza kujenga mabanda mazuri kabisa ya kuku, bata, bata mzinga, sungura (hawa tayari wapo), mbwa tayari wapo pia, kuna kitenga vya kasuku pia na maboxi ya njiwa.
Mji wa aina hii bado ukiwa mpweke we tena basi!
Mana kuanzia asbh naamka ninatoka banda hili, naingia lile, naenda mgomba huu mara mpera ule.
Sijawahi hisi upweke nikiwa nyumbani!