Namna ya kupunguza upweke nyumbani

Itakua una familia! Ukiwa na familia huwezi kua mpweke, changamoto ni sisi wazee wa chumba & sebule afu upo mwenyewe
Watoto nao wakianza kujitegemea acha tu...Mi nikistaafu naenda uswahili huko kweny vigege vya kahawa kukaa.
 
Watoto nao wakianza kujitegemea acha tu...Mi nikistaafu naenda uswahili huko kweny vigege vya kahawa kukaa.
Unaenda eneo ambalo mji haujakua sana unatengeneza sehemu nzuri unauza kahawa watu wanakunywa huku mnaaangalia bunge😁hapo hutakaa uwe mpweke
 
Safiii anza kumanifest hii sasa hivi.
Mimi nilianza kupanda miti siku ya kwanza nimenunua eneo.
By the time naanza kujenga(two years later) ile miti ilishakuwa mirefu kabisa.
eneo la garden nililikata kabla kuchimba msingi.
Watu hawakunielewa, so nimeanza kujenga nikaanza na bustani ya maua mbele ya nyumba, mpk sasa ni kama tumeishi hapo miaka 5 , wakati March mwaka huu ndo tunakamilisha mwaka.
tunakula ndizi,mikomamanga miti imeshaweka vivuli vikubwa kabisa

So anza the very day umelipia eneo lako.
set mahala pa mazao mafupi, miti mirefu, bustani, mabanda ya mifugo na eneo la nyumba!
 
Kwa bahati mbaya sana mkuu bado sijapata eneo la kumiliki ambalo litanitisha kwa hayo yote.

I Hope miaka ya mbele nitapata eneo kama hilo.

Nimekosa basi iwe japo robo tatu hekari ama hekari moja.

Nataka niwe mtu wa shamba yaani kila bidhaa ipo hapo nyumbani.
 
Unaenda eneo ambalo mji haujakua sana unatengeneza sehemu nzuri unauza kahawa watu wanakunywa huku mnaaangalia bunge😁hapo hutakaa uwe mpweke
Nimegundua upweke ni tatizo kubwa hapa duniani sio ulaya tu pekee.

KUna haja ya kuishi kama ambavyo tuliishi utotoni yaani marafiki na kuwa na bize nyingi za hapa na pale.
 
Me ukitaka uone kweli nipo mpweke ni pale flow ya hela inaposuasua ila kuhusu watu huwa natamani hata niwahamishe dunia nyingine hii nikae mwenyewe.
 
Binafsi yangu nikikaa vijiweni au sehemu yoyote ambayo watu wanaongelea sana maisha ya watu negatively lazma nipate loniliness kubwa kuliko nikiwa peke yangu.

Loniliness ingine ni nikiwa sina hela 😁😁 hapo inazidi mara dufu
 
Me ukitaka uone kweli nipo mpweke ni pale flow ya hela inaposuasua ila kuhusu watu huwa natamani hata niwahamishe dunia nyingine hii nikae mwenyewe.
Hata mili niliangalia kuna pattern za maisha nikaja kugundua. Nikiwa sina pesa nakuwa miserable

Ila kama miamala inasoma na nipo busy kwa kufanya kitu nachokipenda. Loniliness ni ngumu sana kunipata
 
Hata mili niliangalia kuna pattern za maisha nikaja kugundua. Nikiwa sina pesa nakuwa miserable

Ila kama miamala inasoma na nipo busy kwa kufanya kitu nachokipenda. Loniliness ni ngumu sana kunipata
Yah mkuu hata mimi nimeona.

Ndio maana husemwa kwamba pesa na maendeleo ni moja ya sababu ya upweke hapa duniani
 
Kwenye kila familia kuna watoto huwa wanakuwa kama walezi wa wazazi ,wao wanakusanya maokoto kutoka kwa mabrothers na masisters wake...wanakaa tu home kwao.
 
Manifest.
Tamka unalo na kisha utaona kila unachofanya unakielekeza kwenye dream yako.
wala usipunguze ukubwa.
Sema nina heka 1 yenye mifugo na makazi na mimea.
Utaishi ukiimeza hii na kila senti utajikuta unaielekeza kwenye mrija utakakaokupatia unachotamani!

Hebu soma 365 Manifestation Power + Workbook
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…