Namna ya kutambua kama umeokoka au wewe ni Mkristo

Wasikilize watumishi na manabii utagundua hilo,Kuna mmoja anasema mfalme Suleiman yupo kuzim!

Labda ndio maana anahusishwa kuwa Baba was wajenzi huru hao Freemasons!!!!

We wasikilize utajua tu!!
Kwa hiyo niamini maneno tu ya hao wanaojiita manabii ? Yani niamini tu hivyo hivyo ?🤔🤔🤔
 
Kwanini wasiwepo nyakati hizi ila wawepo nyakati zilizopita?🤔🤔🤔🤔 najifunza.
Nakupa sifa moja ya mitume: ni watu waliopewa kazi ya kuweka misingi ya kanisa na ukristo, hao walimwona Yesu Kristo akiwa hapa duniani kwa macho yao.

Manabii kazi yao kubwa ilikuwa ni kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu wakati ambapo hatukuwa na Biblia.

Kazi za mitume na manabii ndizo zilizotupa Biblia.

Manabii na mitume walishamaliza kazi zao.

Wametupa Biblia ambayo ndio Neno la kuaminiwa na la kutegemewa.

Hawa wote unaowasikia siku hizi ni self-proclaimed na ni wafanyabiashara.
 
Kuokoka ni kuamini kuwa kuna Mungu mmoja tu na kumkiri mwanae wa pekee Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi wa ulimwengu aliye na mamlaka Duniani na Mbinguni, kubatizwa kwa maji mengi na kuishi kwa maisha yenye kuzitii na kutozivunja amri 10 za Mungu (hili ni la muhimu sana maana amri 10 za Mungu zilitoka kwake mwenyewe)

Wengi wameokoka kutokea dhambini hivyo wanamkiri Yesu huku bado wanavutwa na shetani ndio maana utakuta kuna baadhi ya vitu wanaviacha na vingine vinawashinda japo taratibu wanajitahidi kufanya hivyo

Imani hujengwa taratibu ndio maana wanasisitizwa kutoliacha kanisa na kujibidiisha katika kulisoma neno lake na kujumuika na wenzao katika ibada ili kuijenga imani na ujasiri wa kiroho kuishinda nguvu ya shetani, hii haijawahi kuwa rahisi lakini ukiweka nia baada ya muda unafanikiwa.

Bwana Yesu asifiwe
 
Mtaadhibiwa kwa kupotosha watu.
 
Tuta amini vip hao manabii walikuwepo kwel na walitumwa na Mungu na hawakuwa wafanya biashara?

Kama issue ni kuamini tu kwa nini hata hawa wa sasa tusi waamini tu ??? Najifunza[emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…