Namna ya kutambua simu unayonunua kama ni Brand new au Refurbished

Namna ya kutambua simu unayonunua kama ni Brand new au Refurbished

Mnao nunua samsung za kitonga mnapewa zenye kioo namba mbili, kilia kitu ni org ila kioo chenga hizi zimejaa kariako, kioo namba mbili kinakuwa rangi yake kama imepauka flani hivi, pia Wanao taka camera, ukiona timu spes za camera hazima haina telephto na optical zoom usiguse
 
Kuna Post Mdau kauliza Duka gani lina reputation nzuri ya kuuza SIMU ZA SAMSUNG ORIGINAL NA SIO REFURBISHED?

Nimeona nijibu kama Post Mpya kwa Faida ya wengi, kwa miaka mingi niliyouza Simu,nimeona maduka makubwa wakiuza vitu FAKE,used kwa bei ya kitu KIPYA, wateja wengi hawajui na hawana muda,
Ni ngumu sana kujua simu mpya na refurbished kwa macho.

Huwezi kuamini hadi iPhone 16 zinauzwa kama mpya ila zishazingua..kuna duka ni authorized seller wa samsung wanauza simu nyingine zishatumika,nikiwa kama ex winga nitaandika mbinu chache za kujua simu mpya,

Kwa Samsung, angalia Imei number zilizopo kwenye mfuniko wa nyuma na za ndani ya simu zinaendana? Na kama zinaendana, waambie wakupe box, je imei number za kwenye box la simu zinaendana na za kwenye simu?

Software:ukiingia kwenye settings za Samsung, angalia status ya software,wakiandika OFFICIAL means simu haija chezewa,ila wakiandika CUSTOM kimbia

Mbinu nyingine kwa Samsung andika codes hizi kwenye uwanja wa kupiga simu ##786#

Hii inaitwa RTN SCREEN juu kwenye option click VIEW..status ikionesha YES means simu ni REFURBISHED, ikionesha NO means simu ni brand New..

Kwenye iPhone simple,ukiingia kwenye settings za iPhone nenda kwenye settings, nenda kwenye general,then about phone..kuna maneno haya hapa na maana zake

M -simu mpyaaaaa(brand new)

N -Simu ilikua mpya ila imezingua ikarekebishwa na kurudishwa dukani,ila sio USED

F – Simu ni refurbished

Be aware wahindi matapeli.

Hii ni balaa tupu huko sokoni
 
Mkuu ukiachana na hizi brand 2 ulizozitolea ufafanuzi...... vipi kuhsu hizi nyengine au ndo waliosoma Cuba ndio tayari washaelewa.........??
 
Sio kazi unazima simu kisha una hold volumes button halafu Unachomeka usb cable ambayo ipo connected zinaingia download mode.

Inategemea na simu na simu simu za zamani inaweza kuwa na combination nyengine, unagoogle model husika online.
kuna muuzaji atayekuruhusu ufanye haya yote kabla hujalipia hyo smu?
 
Back
Top Bottom