Namna ya uwasilishaji ya Chalamila kuhusu Dart Simu 2000, je viongozi wakumbushwe kuwa wananchi ni maboss wao?

Namna ya uwasilishaji ya Chalamila kuhusu Dart Simu 2000, je viongozi wakumbushwe kuwa wananchi ni maboss wao?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Viongozi wanapoongea na wananchi wanatakiwa kukumbuka kuwa kwenye taifa lenye utawala bora na utawala wa kidemokrasia MWANANCHI ndiye mwenye mamlaka na ameyakasimisha kwa SERIKALI ili imhudumie. Rejea tafasiri ya demokrasia.

Nikiona kiongozi anawafokea wananchi huwa najiuliza je, yeye ni bora Sana kuliko wananchi wanaotoa kero zao? Nimesikia akitumia maneno makali mpaka nikaogopa.

Viongozi wa dini msiposimama kwenye zamu yenu, mtatukosea Sana waumini. Kwa nini msiige mfano mzuri wa kiongozi Kama Mzee Mipango au Biteko. Mh Rais aliwahi kumwambia Chalambila "akue " naona bado hajaweza kubadilika.

Ifikie wakati wakuu wa mikoa nao wapigiwe kura, tuone Kama kweli watachaguliwa.

Wakumbushwe kuwa hawatakaa milele kwenye viti Hivyo REJEA SABAYA!

Kuhusu DART kujenga karakana Simu 2000,sijui Kama zoezi hilo limekusanya maoni ya wananchi? Na kama waliridhia je kwanini walalamike?

PIA SOMA

- RC Chalamila: Wafanyabiashara Wadogo wa Simu2000 wafahamu kuwa eneo walilopo ni la Serikali, lazima liendelezwe
 
Viongozi wanapoongea na wananchi wanatakiwa kukumbuka kuwa kwenye taifa lenye utawala bora na utawala wa kidemokrasia MWANANCHI ndiye mwenye mamlaka na ameyakasimisha kwa SERIKALI ili imhudumie. Rejea tafasiri ya demokrasia....

KUNA SIKU GEN Z TUTALIKOMBOA TAIFA LETU KUTOKA KWA VIONGOZI WASIO NA UWEREDI NA WAROHO WA MADALAKA KAMA AWO NA WENGINE KIBAO NDANI YA TANZANIA
 
Aje tuna maelezo ya kutosha na mustakabali otherwise asiwafokee.

Na wananchi wasigome bila kufata utaratibu, watanzania wanakosea sana hapo.

Strikes and lock outs bongo zina sheria zake.

Cha mwisho, serikali inamiliki ardhi bongo.

Nilikua na ardhi tangibovu barabarani kabisa. Ila alinivamia mwanajeshi, akaichukua, serikali ikanipokonya na kumpa yule bwana, ikanipa ardhi pemba mnazi. 6kms kutoka pemba mnazi centre. Yaani iliammua tu.

Wakasema raisi ameamua kutatua mgogoro hivo. Bongo😥. Namalizia process niondoke maazima.so jamaa wafate tu njia nzuri.

Asante
 
Back
Top Bottom