Namna ya Waislamu kufanya mijadala ya kidini na wasio kuwa Waislamu

Huwa unakuaga na hoja dhaifu sana, ukisoma unachoandika huwa unaona unetumia kabisa akili?
 
Hakuna baya alilolinena mleta mada.
Na ushauri mwingine ni kwamba waislam ni vema wakaacha kuiongelea Biblia, ambayo haiwahusu. Watumie muda wao kuiongelea Quran, ndiyo kitabu chao. Wajue kuwa hakuna muislam anayeijua biblia vizuri zaidi ya mkristo mwenyewe. Waislam kujifanya wanaweza kuwafundisha wakristo kuhusu Biblia, ni kupoteza muda wao, na kufungua ukurasa wa quran yao kushambuliwa na wasioiamini.

Siku zote dini huenezwa kwa ushawishi wa mema na siyo chuki. Ushawishi kwa njia ya wema ndio uliowafanya waislam kubadilika na kuwa wakristo. Wapo waislam walienda shule za kanisa, wakasoma bila kubaguliwa, wakatendewa hata ambayo hawakuyatarajia, baadhi mpaka kupewa scholarships kwenda kusoma nje, wakigharimiwa na Kanisa. Kwa hiari yao, baada ya kuushuhudia upendo wa kweli, waliamua kuwa wakristo, na wengine walienda mbali zaidi na kufanikiwa kuwa mapadre, hata kuwa maaskofu. Mfano mmojawapo ni aliyekuwa Askofu Mkuu Mario Abdallah Mgulunde.

NB: Una nafasi nzuri sana ya kumshawishi mtu kwa kumwonesha upendo, kuliko chuki
 
It feels good to polish Islam by beautiful verses and polite narrations; however to understand Islam you have to listen to some former extremists and unapologetic muslims.

BTW if you have a chance listen to Isa El-Buba testimony to know the dark side of the Islam Cult. Listen to the testimony of the former Head of Sheikhs of Kigoma region Dr. Hussein Mubarak (Holder of PHD in Islamic Sharia) for you to well understand your god Allah. Listen to the Former Arab Muslim "Christian Prince" debating the Islam apologetics with the facts your Imam will never speak of.

I advice you to listen to the people who was born, lived and breathed Islam so as yo can well understand what Islam is.
 
Inaonekana katika uislamu dhambi zinapitakana kirahisi na kiholela au rejareja sana.
Niliwahi kusikia eti hadi kuna namna na mguu wa kuingilia chooni!
And don't call us your people.
I find it very condescending every time you start a thread with "my people", my people, my people, my people my people.......
 
Kama vipi rudi tena barabarani safari hatukukosi mgalatia


 
pole sana neno my people litakuwepo sana,kama linakukera hizo ni shida zako deal with it

Uislamu una adabu Zake,miongoni mwa adabu ni dua,chooni kuna viumbe vichafu vinaishi mle kwahiyo huwa kabla ya kuingia tunaomba dua tukingwe na viumbe wabaya,miongoni mwa dua ni
ewe Allah najilinda kwako kutokana na shetani wa kike na shetani wa kiume

vile vile miongoni mwa adabu ni kuingia na mguu wa kushoto na ukitoka na mguu wa kulia,na kuna dua miongoni mwa dua ewe Mola wangu nakushukuru kwa kuniwezesha kutoa uchafu na kunipa afya njema

Ngoja tuwafundishe kitu,kila neno binadamu analotamka linaandikwa liwe kubwa au dogo,kila mtu au binadamu ana Malaika wawili ambao wanamchunga 24/7 ,anayeandika mambo ya kheri yupo kulia kwako na anayeandika maovu yupo kushoto kwako,haya mtayajulia wapi? Ndio maana huwa tunawalingania muijue haki

Siku ya kiama au hukumu kuna mizani ya haki itapima vitendo vyako vyema na viovu,ikiwemo na maneno yako unayoyatamka,upuuzi utapimwa na maneno mazuri yatapimwa pia,ni jambo gumu kulielewa hili lakini haki lazima isemwe,kwahiyo kama unasubiri kukombolewa na damu ya Yesu imekula kwako,chunga matendo yako,tabia zako na jitahidi uwe na muamala mzuri na Mola wako
 
Wtf shetani wa kike na shetani wa kiume!
 
Makafir maana yake nini na je siyo lugha ya maudhi dhidi ya wasio Waislamu?
Neno kafir (كافر) katika Uislamu linamaanisha mtu anayekataa au kufunika ukweli baada ya kufikiwa na ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Asili ya neno: Linatokana na kitenzi cha Kiarabu “kafara” chenye maana ya kufunika, kuficha au kukataa. Waarabu wa kale walilitumia hata kwa mkulima anayefunika mbegu ardhini.

Katika muktadha wa Kiislamu: Ni mtu asiyemuamini Allah na ujumbe wa Mitume Wake, hasa Mtume Muhammad ﷺ, baada ya ujumbe kufika kwake kwa namna inayofahamika.

Muhimu kufahamu:

Sio neno la matusi bali ni istilahi ya kidini.
Uislamu unahimiza heshima, haki na mazungumzo ya hekima kwa watu wote bila kujali imani zao.

Kifupi: Kafir = mtu asiyeamini ujumbe wa Uislamu baada ya kufikiwa nao.
 
Upo sahihi kabisa,dini ya uislamu ndio inavyoelekeza hivyo kama mada ilivyo dadavua

Ngoja nikupe kisa kimoja juu ya upole na ulaini wa Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wasalam,kulikuwa na mtu mmoja ana mchukia sana Mtume,kiasi kwamba kila siku alfajir alikuwa anaenda kibarazani kwake na kumwaga kinyesi,hali hiyo ikaendelea kwa muda mrefu

Siku moja Mtume anaamka asaubuhi hakukuta kinyesi,akajiuliza leo mbona jirani yangu hakuja hapa na si kawaida yake,akasema bilashaka atakuwa anaumwa

Akaenda kumuona na kumpa pole,akamwambia leo sijaona habar zako nikajua tu utakuwa na shida,jirani akatahayari,alijua hakujulikana,ndio akajiuliza duh kumbe Muhammad rehema na amani ziwe juu yake anajua namwaga uchafu siku zote na hakuja kunigasigasi,aliona haya sana na akasea kweli wewe ni Mtume wa Mungu,baadae akasilimu

Kuna mlevi mmoja alikutwa anakojoa msikitini enzi za uhai wa Mtume,waislamu wakataka kumpiga,Mtume akawaambia wamuache Amalizie kukojoa kisha wamwagie maji,Mtume alikuwa laini sana kwa watu,na upole na mkarimu
 
Kifupi: Kafir = mtu asiyeamini ujumbe wa Uislamu baada ya kufikiwa nao.
Hapa nimekupata. Sasa, je, utakubaliana na mimi kwamba kumwita mtu "Kafir" stranger ambaye hujamuhubiria Uislamu akaukataa ni kumkashifu? Nauliza hivi kwasababu naona kuna watu, hata hapa ndani ya huu uzi yupo mmoja, wanawaita wapinzani wao kiitikadi "makafiri". Years ago nilishawahi kuulizwa "wewe ni mwenzetu au ni kafiri" na Mzanzibari ambaye nilikua ndo nimekutana naye kwa mara ya kwanza ktk maisha yangu. Yaani ilikua kama ndo salamu yake kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…