Nampenda lakini simwamini kabisa, nifanyeje?

Kupitia haya maelezo yako; unatakiwa kuchagua mambo mawili tu!

La kwanza ni kuondoka kwa huyo mpuuzi wako unaye muendekeza, ili uishi maisha marefu hapa duniani!

Au uendelee kubakia naye hapo mnapoishi kienyeji, ili ndani ya miaka michache tu kuanzia sasa akuue na hivyo kwenda kuishia kuliwa na finyi kaburini.

NB: ogopa kuishi na mtu wa aina hiyo katika maisha yako yote kuanzia sasa. Maana mapenzi hayako hivyo mdogo wangu. Sisi wakubwa zako mpaka leo tunadunda, ni kwa sababu hatukuwahi kuwa na wapenzi wa aina hiyo. Usiendelee kuishi na mwendawazimu! Atakuua.

Ukishasema wewe Tate Mkuu Mimi Sina la kuongeza

Hony huu ushauri hapa ukiudharau tutakuja kukusoma mitandaoni kwa huzuni kama ile ya gunia2 za mkaa.
Mashetani NI watu na malaika NI watu pia. Bahati mbaya wewe umekutana na SHETANI mzimamzima kwenye mwili wa binadamu.
 
Kama Alikidanganya vyotr Hivyp mpaka kuhusu mali lengo ilikuwa ni Akumiliki sasa leo unataka kumkimbia kiboyaaa tuu aisee kifatacho ATAKUUA KWELI MAANA HANA CHA KUPOTEZA..!! HANA MAISHA HAWEZI KUKUSHAWISHI UBAKI NAE.

Ushauri..
Nguo sio mali kitu labda kama kwenu ulifukuzwaaa ondoka hata na ulizovaaa uhai wako una thamani sana achana na huyo ashachanganyikiwa dada puuza siku utaombwa msamaha ukiwa KABURINI
 
Binti acha ufala huyo ni kichaa atakuja kukuua kimbia.
Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya Mambo ya kipuuzi namna hiyo.

Mpenzi wako ana matatizo ya akili na wenda anafanya hayo mambo akiwa ajitambui nini anafanya.
 
mama D karibu Dodoma siku ya kuapishwa Tulia. Baadhi ya makada wa chama tutakuwa na jambo letu pale Morena Hotel.

Ukifika getini mwambie mlinzi wewe ni Mgeni wa yule Babu mweupe kutoka Lushoto. Muda ni kuanzia saa nne usiku. Tafadhali uje peke yako.

Asante kwa mwaliko Tate Mkuu
Sasa inabidi tuwaalike kule kwetu Lushoto kina Suluhu, Mpango, Majaliwa na Tulia tuwape cheo Cha TateMkuu
 
Najua we ni mgeni hapa, huenda mwanzo ulikua kama msomaji tu,ukaona ujiunge rasmi ili uombe ushauri, hivyo nawaomba Wana Jf wasikulaumu kutokana na uandishi wako, ispokua wakushauri juu ya matatizo yanayo kukabili.

Hapo ukiendelea kukaa utakua na tatizo la kisaikolojia, yaani mara nyingi utakua unajawa na hofu, hata presha inaweza kukushika kutokana na matendo ya huyo mtu wako.

Pia anaweza kukudhuru, kuna hisia na uhalisia, kihisia unaona bado unampenda, ila kiuhalisia ni lazma umuache uende zako kwa faida ya furaha ya maisha yako na amani ya kweli, hutakaa ufurahie hayo maisha, tena ukisha mzalia ndo kabisa utakua umefunga pingu na matatizo.

Lakufanya: Ondoka bila kumtaarifu, kisha ukishafika kwenu mtumie ujumbe kua wazazi wako wamekuja kukuchukua hivyo asihangaike kukutafuta aendelee na maisha yake, vunja line, badili namba, baada ya mda utarudi na kuimarika tena.
Atakutana na mkono wa sheria mkononi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni ushauri,

Mimi ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana wapenzi wengi t, kanidangany mpaka level yake ya elimu n.k,

Siku yaliponkfika shingoni nikamwambia ukweli na nikamuaga naenda sehemu nikapitie vitu vyangu kisha nielekee nyumbani nikawasalimie, kiukweli nisiwe mnafiki nilikuwa nasepa mazima. Alikubali lkn imefika usiku wa kuamkia siku ambayo naondoka akanibadilikia na tulikuwa tunacheka kabisa, ghafla akaanza kucheka akanishikia kisu usoni akabadilika kabisa lkn anacheka sana, aliniwekea tumboni akasema bora aniue tu maana ananipenda lkn nataka niache Dah kiukweli nilijitetea mpk nilichanganyikiwa, hatimaye baada ya masaa takriban mawili aliniacha akasema nikirudia atanimaliza kabisa.

Siku moja kanikuta na simu nipo instagram naangalia comments nikawa nacheka lkn limekuwa ni tatizo kwake (hili ni la muda mrefu hataki nishike simu, hajawahi kunikuta naongea na mwanaume wala kunasa msg na yeye anajua sina hiyo tabia, nikishika simu nafanya application za kazi nikichoka naingia kujiburudisha mtandaoni sasa kinamuuma sana mm kufanya hivo), hiyo siku akaanza kunigombeza, kwa kuwa ni tabia yake siku hiyo nikamwambia laivu nimechoka na hii tabia, ghafla kaanz kunipiga anasema ko imechoka kuishi na mimi, akaniumiza sana akaona haitoshi kakimbilia kisu dah! Nilipiga kelele watu wakaja ndio akaniachia.

Asubuhi kulipokicha akanifata nilipolala akaanza kulia sana ananiomba msamaha, alijutia alichokifanya mpk leo namuona hayupo sawa, nilimwambia nimemsamehe lkn aliendelea kulia baadae akanyamaz lkn anajuta hadi leo. Tangu siku anipige na kunishikia kisu namuogopa sana, simwamini tena nikimuona nawaza kuna siku ataniua, tunaweza kuwa tunacheka kabisa ghafla hali ya hofu inanitawala, nabadilika kabisa mpaka anaanza kulia tena, hio hali inanisumbua sana, akinikumbatia nakuwa na furaha ghafla tena nashikwa hofu hapohapo,namwambia aniachie, akiniletea zawadi ananiambia fumba macho ili anipe, nafumba ghafla naanza kupiga kelele nafumbua macho!

Dah of course inamuuma Sana akiniona na hali hiyo lkn akili yangu najaribu kuirudisha upya imegoma kabisa, nawaza kutoroka tuu muda wowote na inaniuma kuondoka bila kumuaga nifanye je?nisaidiwe nn cha kufanya? Halafu amenihofia je nikitoroka akaninasa njian? Maana ananiwinda sana. Nampenda lakini nipo tayr kujisacrify kumuacha, nitumie njia ipi?
Ondoka haraka sana.. otherwise…….
 
Kimbia kifo kitakukuta hapo
 
Ila Kuna watu wanajiendekeza sana
Mtu keshakudanganya yote Hayo wewe bado upo tuuuuu

Watu tunatofautiana lakini kiukweli kwa mtu mzima mwenye akili kuna vitu hata havihitaji kuomba ushauri....
Bado nischana 24 ...ndo maana kaomba ushauri.

Ila kama wee hapo, aahh mapema, ushaamua vyakumuamua.
 
Una mchumba wako halafu mnaishi pamoja...wanawake siku hizi mnajirahisisha kweli

Kuna uwezekano unaishi na mwanaume ambaye ana dissociative identity disorder au aina nyingine ya magonjwa ya akili au mtu mgomvi...

Wewe tuambie tu ukishauawa tukusafirishe au tukuzike hapahapa?
 
Back
Top Bottom