Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ambacho nakiona, ni kuwa, kuna siku kisu kitaingia mwilini mwako.Naombeni ushauri,
Mimi ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana wapenzi wengi t, kanidangany
Mkuu toa tu msaada na wengine wafaidike, msaada wako ukiwa mzuri wengi watakufuata uko uko kwa msaada zaidi.Njoo PM nimesadia watu wengi tuu wenye matatizo kama yako
Kwani uandishi wake umeuona una matatizo gani?Najua we ni mgeni hapa, huenda mwanzo ulikua kama msomaji tu,ukaona ujiunge rasmi ili uombe ushauri, hivyo nawaomba Wana Jf wasikulaumu kutokana na uandishi wako, ispokua wakushauri juu ya matatizo yanayo kukabili.
Anza kuandaa kaburi lako,kifo kifo kifo hakina hurumaNaombeni ushauri,
Mimi ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata,
KweliMapenzi gani haya mbona bado mdogo hivyo ebu toka hapo dear achana na huyo mwanaume hana cha kuchanganyikiwa chochote ni usanii tu anakufanyia
Mkuu nakubaliana na wewe, huyu jamaa hundred percent ni psychopath...Kama sio unaishi na mgonjwa wa akili bhasi huyo ni psychopath...na atakuua kweli kishaa aanze kujutia wewe ukiwa maiti..ondoka haraka,au huna pa kwenda?
You are living with a psychopathy.Naombeni ushauri,
Mimi ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana wapenzi wengi t, kanidangany mpaka level yake ya elimu n.k,
Siku yaliponkfika shingoni nikamwambia ukweli na nikamuaga naenda sehemu nikapitie vitu vyangu kisha nielekee nyumbani nikawasalimie, kiukweli nisiwe mnafiki nilikuwa nasepa mazima. Alikubali lkn imefika usiku wa kuamkia siku ambayo naondoka akanibadilikia na tulikuwa tunacheka kabisa, ghafla akaanza kucheka akanishikia kisu usoni akabadilika kabisa lkn anacheka sana, aliniwekea tumboni akasema bora aniue tu maana ananipenda lkn nataka niache Dah kiukweli nilijitetea mpk nilichanganyikiwa, hatimaye baada ya masaa takriban mawili aliniacha akasema nikirudia atanimaliza kabisa.
Siku moja kanikuta na simu nipo instagram naangalia comments nikawa nacheka lkn limekuwa ni tatizo kwake (hili ni la muda mrefu hataki nishike simu, hajawahi kunikuta naongea na mwanaume wala kunasa msg na yeye anajua sina hiyo tabia, nikishika simu nafanya application za kazi nikichoka naingia kujiburudisha mtandaoni sasa kinamuuma sana mm kufanya hivo), hiyo siku akaanza kunigombeza, kwa kuwa ni tabia yake siku hiyo nikamwambia laivu nimechoka na hii tabia, ghafla kaanz kunipiga anasema ko imechoka kuishi na mimi, akaniumiza sana akaona haitoshi kakimbilia kisu dah! Nilipiga kelele watu wakaja ndio akaniachia.
Asubuhi kulipokicha akanifata nilipolala akaanza kulia sana ananiomba msamaha, alijutia alichokifanya mpk leo namuona hayupo sawa, nilimwambia nimemsamehe lakini aliendelea kulia baadae akanyamaz lkn anajuta hadi leo. Tangu siku anipige na kunishikia kisu namuogopa sana, simwamini tena nikimuona nawaza kuna siku ataniua, tunaweza kuwa tunacheka kabisa ghafla hali ya hofu inanitawala, nabadilika kabisa mpaka anaanza kulia tena, hio hali inanisumbua sana, akinikumbatia nakuwa na furaha ghafla tena nashikwa hofu hapohapo,namwambia aniachie, akiniletea zawadi ananiambia fumba macho ili anipe, nafumba ghafla naanza kupiga kelele nafumbua macho!
Dah of course inamuuma sana akiniona na hali hiyo lkn akili yangu najaribu kuirudisha upya imegoma kabisa, nawaza kutoroka tuu muda wowote na inaniuma kuondoka bila kumuaga nifanye je?nisaidiwe nn cha kufanya? Halafu amenihofia je nikitoroka akaninasa njian? Maana ananiwinda sana. Nampenda lakini nipo tayr kujisacrify kumuacha, nitumie njia ipi?