Nampenda sana ila kwa hili naombeni maoni

Okay ushaeleweka kuwa wewe ni mtu wa fashion (wakisasa) na dress code anazopiga binti ni kama huzielewi

Ushawahi mtoa out siku moja aukasema bibie leo pesa hii hapa ebu vunja kabati chukua hii na hii?

Au ushawahi mletea zawadi ya nguo zile ambazo wewe unafikiri ndio zinazo weza kuku turn on ukiwa naye?
 
Ipo shida mahali, umempenda Kwa vitu temporary na sio permanent, utajuta in ur next chapter, someone who doesn't fit you in God's perspectives muache sio wako huyo. Wewe ni WA mataifa yeye ni mwana low profile. Utajuta tafuta wa aina yako
 
Nimeona upo 20s nikaona nikusamehe kwani bado una mengi ya kujifunza; Kuhusu mavazi sio issue kubwa kwani bado unanafasi ya kumbadilisha ukitaka. Unaonaje ukampeleka shopping ukamnunulia nguo mbili tatu unazozipenda uone kama hatazivaa? Akizivaa akapendeza mwelekeze kuwa unapenda design hizo...
Hawa viumbe muda mwingine hufundishwa kwa action (na ndicho wanapenda)
 
Mtatuprovoke asubuhi asubuhi...
Ulishajaribu kuwaza labda inawezekana amekuzidi maarifa fulani na hivyo hapo anakupotezea muda au mnapotezeana muda kuna sehemu anaenda hapo anapita
 
Ww kama mpenzi wake ni jukumu lako kumnunulia nguo unazoona zinampendeza ,hilo swala ndogo sana ,ingekua tabia kama ulevi, kukojoa kitandani ,matusi,...ningeona ni tatizo
 
Mpeleke shopping ukamnunulie unachotaka avae halafu uone. Hilo eneo sasa ni kazi yako kumbadilisha.
 
Wakati mwanaume flani anahangaika kumpata 'wife material' wenye tabia njema, heshima, utii na nk, kuna wengine wanahangaika na mavazi mabovu ya mwanamke huyo. Kijana, hebu kuwa makini kidogo, tafuta sababu zingine za kukufanya ukereke na sio mavazi.
 
Yaani jambo dogo kama kuvaa ndio unalileta huku?
Si umshauri avaaje

Aiseee.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Unataka akiwa na wewe au mkiwa mnatembea awe anavaa hivi? Hujui km mmezaliwa na familia na malezi tofauti? Hujui kwamba alichofunzwa na wazazi wake sicho ulichofunzwa na wazazi wako?
 
Sasa wewe unashindwaje kumchagulia na kumnunulia nguo nzuri ili apendeze unavyotaka wewe?

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, fanya kuni PM namba za binti ili nimuelekeze namna gani anatakiwa kuvaa. Mimi ni fashonisti na mtu wa massaji kwa ujumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…