MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.
Ninaandika nikiwa na furaha kubwa sana kuhusu vikao vinavyoendelea kati ya Mama Samia na viongozi wa Chama Cha Mbowe. Kama mnavyokumbuka kabla ya Mama kukutana na viongozi wa CHADEMA tayari alishafanya vikao viwili na mwenye chama Mh Mbowe. Vile vikao viwili vya mwanzo vilikuwa muhimu sana kuweka mambo sawa. Ukishamweka sawa mmiliki wa chama basi hawa wengine lazima waufyate.
Mwenyekiti wa CHADEMA kafanya vyema sana kuwashirikisha viongozi wa chini yake mazungumzo ya ikulu ili kusitokee mvutano usio wa lazima. Hawa wafuasi wa mitandaoni hawana athari zozote kwa chama zaidi ya kupiga tu makelele yasiyosaidia. Kina Mdude, Hilda, Yeriko na wafuasi wengine maarufu mtandaoni sio lazima sana kuwashirikisha maongezi nyeti kama hayo. Hata wanachama wengine wanatakiwa wajue tu mlienda ikulu hakuna haja ya kujieleza. CHADEMA ni imani na asiyeamini akatafute chama kingine.
Ila lazima Mbowe awafikirie watu wawili. Lema na Lissu. Hawa wana ushawishi mkubwa kwahiyo hata wao ni muhimu walambishwe "asali" ili kuleta utulivu. Ila kama asali ni kidogo amlambishe Lema tu maana yule ni mtoto wa nyumbabi tofauti na huyo mwingine aliyekuja baadae. Ikumbukwe hakuna mtoto wa nyumbani aliyewahi kufukuzwa kwenye chama. Hivyo malalamiko ya Lema kwamba hajalambishwa asali ni rahisi kumfikia baba mkwe ikawa shida.
Namaliza kwa kumpongeza Mama Samia kwa kucheza kete zake vizuri.