Nampongeza mwananchi kwa kunipa ushirikiano wa kusambaratisha ndoa ya Mwanafunzi wa Darasa la 6 Kata ya Mambali Nzega, Tabora

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
1,710
Reaction score
8,690
Wasaalam.

KISA; Tarehe 6 Julai, 2025 Jumapili, jioni majira ya saa 9 nilipokea taarifa ya ujumbe wa simu (sms) kutoka kwa mwananchi mzalendo kutoka huko Tabora, Nzega, kuwa: kuna mwanafunzi wa darasa la 6 kaozeshwa kwa nguvu na wazazi wake na kuna juhudi za kuficha hizi taarifa. Aidha, mwananchi alisema, wanaofanyiwa hivyo wakikataa wanafukuzwa makwao.

HATUA NILIZOCHUKUA; kuwapa taarifa mamlaka ya mkoa husika ili Sheria ya mtoto ifanye kazi yake.

MATOKEO; Mwananchi mzalendo mtoa taarifa amenitumia ujumbe kuipongeza Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, tayari mtoto aliyeolewa ametafutwa na amepatikana kutoka huko alikofichwa pia, waliohusika wametiwa nguvuni kwa maelezo na hatua zaidi. Taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika.

FUNZO; Ndugu Wananchi, mawasiliano ya kidigitali ni msaada mkubwa kwenye ulimwengu wa leo katika kuelimisha umma, kupokea na kupeleka taarifa na kuchukua hatua kwa gharama nafuu kabisa hivyo, tuendelee kushirikiana zaidi kupitia hii fursa kwani, tunafikika hadi vijijini.

HITIMISHO; Binti atarejea shuleni na waliohusika watapambana na sheria. Aidha, Nakemea Waoaji na Waozaji wa Watoto/ Wanafunzi. Nawataka jamii iache kuoa na kuoza Wanafunzi maana, utaratibu huo umepitwa na wakati. Hivi sasa, wananchi wako macho na taarifa zinasafiri kwa kasi.

MIKAKATI ZAIDI; Tutawafikia waharibifu wa watoto popote walipo. Wote mliowaoa wanafunzi, warejesheni shuleni mara moja kabla hatujawafikia. Timu yangu na mimi binafsi, tutaendelea kupokea sms za wananchi kuhusu masuala ya wizara hii na kuchukua hatua na kutoa mrejesho ili, kuwatia moyo zaidi wananchi.

MWISHO; Ndugu Wananchi, naomba sambazeni mawasiliano yetu, washeni moto wa FAECHA: FAHAMU ELIMIKA CHUKUA HATUA 💪🏼✍🏼,

🇹🇿Maendeleo na Ustawi wa Watoto Tanzania, Inawezekana.

@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @ofisi_ya_mkuu_wa_mkoa_tabora_ @rcpaulchacha Mhe. RC Tabora, PONGEZI KWA KAZI NZURI✅️✍️
@maendeleoyajamii Ofisi ya Rais - Tamisemi
IMG-20250710-WA0006.jpg
IMG-20250710-WA0006.jpg

Pia soma ~ Waziri Gwajima, sikia kilio cha Watoto wanaofanyiwa ukatili, Ubakaji, mimba, ndoa za Utotoni Uyui (Tabora)
 
Mheshimiwa waziri hongera sana kwa kazi iliyotukuka ,ila hujaweka mawasiliano ili nasi tukipata changamoto kama hiyo tukujulishe
Jamani, miaka yote mi5 natangaza namba zetu na yangu binafsi wewe bado kumbe hujawahi ona hadi niko finishing line? Duuu, nchi kubwa👇 yangu ipo bango la tatu 0765 345777 unatuma sms tafadhali nitasoma. Shukrani kwa ushirikiano wako.
 
Attachments

  • IMG-20250708-WA0028(1).jpg
    IMG-20250708-WA0028(1).jpg
    151.2 KB · Views: 23
  • IMG-20250708-WA0027(1).jpg
    IMG-20250708-WA0027(1).jpg
    186.1 KB · Views: 26
  • IMG-20250510-WA0045(17).jpg
    IMG-20250510-WA0045(17).jpg
    115.6 KB · Views: 32
Mh Waziri nipe ushauri Nini nifanye
Leo asubuhi nimebahatika kuzuia utoroshwaji wa mtoto wa kike wa kidato Cha pili ambaye alitakiwa kusafirishwa kupelekwa mkoani Arusha kufanya kazi za ndani make tayari alishavuka Wilaya Moja ndo nikabahatika kumkatamata na nilipompekua nilimkuta na namba za simu za mtu aliyekuwa anawasiliana nae kupitia simu za kuomba
Sasa sijuhi Kuna hatua zaidi za kisheria natakiwa kuzifuata? Kupitia hii namba niliyomkuta nayo ameandika kwenye karatasi?
 
Wasaalam.

KISA; Tarehe 6 Julai, 2025 Jumapili, jioni majira ya saa 9 nilipokea taarifa ya ujumbe wa simu (sms) kutoka kwa mwananchi mzalendo kutoka huko Tabora, Nzega, kuwa: kuna mwanafunzi wa darasa la 6 kaozeshwa kwa nguvu na wazazi wake na kuna juhudi za kuficha hizi taarifa. Aidha, mwananchi alisema, wanaofanyiwa hivyo wakikataa wanafukuzwa makwao.

HATUA NILIZOCHUKUA; kuwapa taarifa mamlaka ya mkoa husika ili Sheria ya mtoto ifanye kazi yake.

MATOKEO; Mwananchi mzalendo mtoa taarifa amenitumia ujumbe kuipongeza Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, tayari mtoto aliyeolewa ametafutwa na amepatikana kutoka huko alikofichwa pia, waliohusika wametiwa nguvuni kwa maelezo na hatua zaidi. Taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika.

FUNZO; Ndugu Wananchi, mawasiliano ya kidigitali ni msaada mkubwa kwenye ulimwengu wa leo katika kuelimisha umma, kupokea na kupeleka taarifa na kuchukua hatua kwa gharama nafuu kabisa hivyo, tuendelee kushirikiana zaidi kupitia hii fursa kwani, tunafikika hadi vijijini.

HITIMISHO; Binti atarejea shuleni na waliohusika watapambana na sheria. Aidha, Nakemea Waoaji na Waozaji wa Watoto/ Wanafunzi. Nawataka jamii iache kuoa na kuoza Wanafunzi maana, utaratibu huo umepitwa na wakati. Hivi sasa, wananchi wako macho na taarifa zinasafiri kwa kasi.

MIKAKATI ZAIDI; Tutawafikia waharibifu wa watoto popote walipo. Wote mliowaoa wanafunzi, warejesheni shuleni mara moja kabla hatujawafikia. Timu yangu na mimi binafsi, tutaendelea kupokea sms za wananchi kuhusu masuala ya wizara hii na kuchukua hatua na kutoa mrejesho ili, kuwatia moyo zaidi wananchi.

MWISHO; Ndugu Wananchi, naomba sambazeni mawasiliano yetu, washeni moto wa FAECHA: FAHAMU ELIMIKA CHUKUA HATUA 💪🏼✍🏼,

🇹🇿Maendeleo na Ustawi wa Watoto Tanzania, Inawezekana.

@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @ofisi_ya_mkuu_wa_mkoa_tabora_ @rcpaulchacha Mhe. RC Tabora, PONGEZI KWA KAZI NZURI✅️✍️
@maendeleoyajamii Ofisi ya Rais - TamisemiView attachment 3400053View attachment 3400054

Hivi mtoto kama huyu hatima yake ya Malezi inakuwaje ?
 
Back
Top Bottom