Unaposema wananchi hawafaidi matunda ya uhuru isipokuwa viongozi na familia zao umesahau kuwa kabla ya uhuru wananchi haohao walikosa haya yafuatayo:
1)Kuishi baadhi ya maeneo ya nchi yao.....mfano kule KICHANGA CHUI(MASAKI YA LEO)...daraja la selander lilikuwa mpaka wao na watu weupe.
2)Wananchi haohao hawakuwa na ACCESS ya kupata huduma za afya....hospitali zilikuwa kwa ajili ya weupe tu....mpaka akajitokeza "TAJIRI MMOJA MZALENDO...tajiri huyu mwenye asili ya kihindi akafungua ZAHANATI kwa ajili ya wazawa pale ilipo STESHENI POSTA.....
Baadaye akaja ndugu SEWA HAJI na kuendelea kutoa nafasi ya kutibiwa wazawa......
Je hospitali ,vituo vya afya na zahanati zilizoko SASA ZINAFANANA na zilizokuwa kipindi cha AWAMU YA KWANZA?je hakuna hatua za MAENDELEO makubwa kufikia sasa ?!!
3)Mkoloni aliacha barabara moja tu.....mikoa haijaunganishwa?!! Si faida kwetu wananchi wa kawaida?!!!
4)Baba zetu walikula UNGA WA YANGA na kuvaa ndala ,je Leo hakuna mabadiliko?!!
5)Mkoloni hakuacha CHUO KIKUU hata kimoja....Uganda alikijenga.......je leo hatuna vyuo vikuu mpaka "vichochoroni"?!
We jamaa mtambo kweli sio kidogo tena chenga kweli.
Ivi hasikii au kuona migogoro ya ardhi kila siku juzi wananchi huko morogoro wamechoma magari na vitu vingine vya watu toka wizara ya ardhi au wewe hauko nchi hii
Hizo huduma unazozungumzia ambazo hakuna wataalamu na vifaa pia hata maslahi ya watumiaji huko ni duni kupelekea kukosa motisha hata huduma ni bora liende ndio maana vigogo na wenye nazo wanatibiwa kwenye hospitali binafsi,kuna vituo vya afya vimejegwa ila mtumishi mmoja, juzi hospitali ya bugando ilikua haina mitungi ya gasi na ile ndio hospitali ya rufaa je huko kwengine inakuwaje
Kuhusu suala la barabara acha kabisa maeneo ya uzalishaji yana hali mbaya ndio maana hata gharama za maisha ziko juu hizo unazozungumzia za mikoa wamejenga kwa sababu ya kufanikisha mambo yao ila sio kwa lengo la kuboresha maisha mfano juzi tumeona huko mlimba mbunge anaenda kuzindua daraja la 31m ambalo ni la mbao kwa karne hii
Leo hii watu wanakosa chakula kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi, mfumuko wa bei za bidhaa na chakula pia upungufu wa ajira licha ya uwepo wa rasilimali mali nyingi,mwekezaji anakuja na watu wake kila sehemu na sisi tunabaki kuwa vibarua kwenye hiyo miradi kwaiyo wimbi kubwa halina ajira inayopelekea mzunguko hafifu wa uchumi
Acha uongo hayo majengo mengi ambayo ni vyuo vikuu Sasa yalijengwa wakati wa ukoloni IDM,UDSM lakini pia kuwa na vyuo vikuu vingi sio kipimo Cha maendeleo na je hao wahitimu wanachangia vipi kama katika uwekezaji kwenye rasilimali wawekezaji wanakuja na watu wao vijana wa kitanzania wanaambiwa wajiajiri
Nikwambie tu ndugu yangu nchi yetu hii wanaofaidika ni wachache Sana ukilinganisha watu na rasilimali. Tatizo mnaleta mahaba kwenye vitu vya msingi, migogoro tuliyoiona kwa wenzetu mingi ilitokana na mfumo mbovu Kama huu kwa sababu kuna kundi la watu wachache wanaokula mema ya nchi ambayo inasababisha kuwa na pengo kubwa kati ya masikini na matajiri