Uchaguzi 2020 Namshauri Lissu asifanye kampeni, panakaribia kucha

Mnataka kuleta zile habri za Tumuachie Mungu
 
Hamna chochote kitakachofanyika hamna serikali unaweza beba risk Kama hiyo kwa Hali ya kisiasa ilivyo Tanzania
 
Hakuna injustice yoyote anayofanyiwa Lissu ni upumbavu wake tu anajijaza kiburi kulata sifa.

Vitabu vya dini vimeagiza kuziheshimu mamlaka. Ukitaka kujua hafai kuwa kiongozi ni kauli aliyosema akishindwa uchaguzi hatakubali, hii maana yake ni nini? anafahamu wangapi watampigia kura? Achana na akili uliyoenda shule, tumia ile kabla hujaenda shule wanaitaga aKili ya kuzaliwa utaona wazi Lissu amekuja kigomvi. Na sio bure wazungu wake wamemdanganya akianzisha vurugu watapaza sauti kuomba serikali ya makubaliano kwamba waziri mkuu au kiongozi mkubwa yeyote atoke upinzani. Tundu Lissu yupo tayari kuanzisha vita Tanzania na ikitokea yeye anaenda zake ubeligiji kujigijigi anawaacha mnapambana wenyewe na njaa zenu.
 
Hapana, asimame ili joto lipoe? No way, Uchaguzi hauwezi kuendeshwa kwa maelekezo ya Magufuli, No way
Nakubaliana na wewe! Pia ngamia ukimuachia aingize kichwa bandani mwako, atataka aingize na nundu yake!

Kwa kifupi watazoea...
 
Angalau wewe unanaoneka una mapenzi ya kweli, wengine wanamtumtumia tundu kama msukulule tu, lkn mwisho wa siku hawajali chochote kuhusu tundu, ...
Umesahau kwamba tulitaka kusoma dua mlipotaka kumuua mkakataz?
Umesahau tulichangia matibabu YAke pia?
Umesahau watu huko Kenya walichangia damu zao?
 
Wewe utakuwa wa kwanza kukatwa masikio
 
Kwa dhati kabisa leo nakupongeza kwa hii post🙏
 
Napinga Ushauri wako ili kulinda Katiba ya nchi na kanuni za uchaguzi
 
Kutokana na onyo la NEC la kusimama siku saba, nashauri kamati kuu imshauri atii Kwa hili hata kama kaonewa. Waswahili husema Kula na kipofu usimshike mkono.

Ujeuri wake na ukurupukaji unaweza kumponza hata kile kidogo cha kupata wabunge wengi atakikosa. Sio kila Jambo ni nguvu. Ukiheshimiwa kidogo na wewe onesha heshima pia.

Kumbuka watanzania ni waoga usitegemee nguvu ya umma kukuingiza Ikulu. Wengi wanakushangilia lakini ukiwaambia wakusindikize mahali hawatoki. Pia kumbuka wengi wanaokusapport hawatapiga Kura Kwa sababu tofauti.

Tafakari ndugu wanakamati najua mnajua mengi.

Huu ni sauti ya Unabii.
 
Kutokana na onyo la NEC la kusimama siku saba, nashauri kamati kuu imshauri atii Kwa hili hata kama kaonewa. Waswahili husema Kula na kipofu usimshike mkono...
Hakuna ujinga yaani aonewe alafu akubali
 
Niliposema Lissu anadharau 'machinery' za nchi yetu hamkunielewa mwanzoni. Taratibu mtanielewa!
 
Nak Naungana na Wewe moja kwa moja ! Mimi ni CCM . Nimuombe Sana , Sana Mheshimiwa Tundu Lissu awe mvulivu kwa muda huo wa one Week . Kwanza atakuwa amepata muda wa kutosha wa kupumzika ! Kampeni ya kuzunguka nchi nzima sio Mchezo !! Ni kazi kweli , kweli ! Na ndiyo maana hata Rais Magufuli naye amejipa muda wa kupumzika ! Awe mvumilivu Tundu Lissu .
 
Ccm kwa kijificha kwenye kivuli cha amani,wananchi sasa wanataka HAKI.
 
Bora afanye kampeni na wajaribu kumzuia ili dunia ione na ikusanye vizuri ushahidi juu ya hawa wauaji na watu wenye roho mbaya

Ingawa hili tu la kumzuia kufanya kampeni kwa siku 7 ni ushahidi tosha
Dunia itawafanyia nini? Kwa sasa kila mtu yupo kwenye ujisaidie mwenyewe mode........zaidi watatoa tu maneno yao yakupeana moyo ndo imekwisha hio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…