Ni kweli mkuu nikuunge mkono Moja kwa Moja tatizo uongozi unaangalia Hali ya Leo na sio ya kesho ,bei ya chakula imekuwa tishio na serikali sidhani kama wamefanya namna yakuagiza stock maana wakulima wengi walikimbilia kuuza mazao kukabiliana na Hali ya maisha ,kwaiyo mkulima mwenyewe ndio wakwanza kuumia ,pia tumejiachia kulalamika mvua hamna wakati tumezungukwa na maziwa ,mito,na bahari na maeneo yakilimo ila hatuna hata mifereji yakudumu kwaajili ya kilimo Cha umwagiliaji ,kwa ufupi ni umaskini wa ajabu kulalamika njaa ,shida kubwa imekuwa elimu na uzembe ambao unatulazimu tuwe na wawekezaji kwenye sekta ambazo ni Bora tukasomeshe wanafunzi nje huko waje waanzishe kilimo chenye tija hapa bongo kuliko kutegemea wataalamu kutoka SUA ambao hawana maono zaidi yakukaa ofisini,huko wakishindwa kuandaa project muhimu za utatuzi wa kudumu