Namshukuru Mungu zoezi langu la kutoa pesa kwenye simu limeenda salama

Namshukuru Mungu zoezi langu la kutoa pesa kwenye simu limeenda salama

Umetoa 500,000.00 Tsh. Kwa wakala: ***** *******.Makato Tsh 12,200.00( Ada Tsh 7,000.00 + Kodi Tsh 5,200.00).Salio Jipya Tsh 172,968.00. Muamala No: CO210730.1759.D******

Ni hatari !!!!!!
Mkuu bado una kipengere cha kukatwa 6100
 
Yaani nusu nusu nikajinyonge
Mungu awalaani hawa madhalimu wameamua kutupora hata kiduchu nimetoa 230000 wamechukua elf 8700 yote bila hata chenji.
Pesa usaka kwa tabu wao wanaenda kununua v8.
 
Ndo
Kusema k
Zimeshuka
Thamani
Hadi
Ziwe bei
Ya nyanya
K hazijawahi kupanda bei mkuu ni wewe jinsi unavyobargain na mmiliki wa K,

Ukimset fresh unapiga ata bure
 
Hatimae leo nimefanikiwa kutoa pesa iliyokuwa kwenye simu yangu kwa Uchungu mkubwa.

Kabla ya makato ya serikali nilikuwa na mazoea ya kuweka pesa yangu ya akiba kidogo kwenye simu na nyingine cash kwenye kibubu,
siku moja kabla ya ongezeko nilitumiwa meseji kuhusu makato nilijua yatakuwa madogo sana kwa sababu ni ya, serikali hivyo niliamua kuacha pesa kwa simu bila hofu.

Nilikuja kushituka usiku nilipokuja kuona mkeka wa makato unavyosoma na ndio zoezi limeanza nilishindwa kuwaza nifanye nini zaidi ya kuamua kuiacha

Ni pesa Ndogo lakini kwangu ni kubwa ilikuwa tu 150k (laki na nusu)

Imekaa humo mpaka leo nilipoamua tu ngoja nikatoe niitiage kwenye kibubu ichanganyikane na wenzake

Siwafichi haya makato yanauma sana, ni kama kisu basi yanakata mpaka kwenye mfupa

150k hapo nimekatwa 6k (elfu sita), fikiria ni laki na nusu tu lakini makato elfu 6

Sahani 3 za kiepe yai, au sahani 4 nne za kiepe kavu

Elfu 6 hiyo, papuchi mbili pale kwenye vyumba vya hapo Buguruni, au mbili za chap chap hapo Chako ni Chako Dodoma,

Wakati wa makato nimeweweseka kwa kweli mpaka mikono ikawa inatetemeka

Na kukumbuka juzi nimeshindwa kuitafuna papuchi ya jirani yangu kisa tu aliniomba elfu 5 na kutaka kunitunuku nikasema sina, ila leo nimekatwa 6k na serikari bila kunifanyia kazi yeyote, sawa kikubwa namshukuru Mungu zoezi langu la kutoa pesa limeenda salama na hivi sasa naendelea vizuri.

Mimi kuja kuweka tena pesa kwenye simu mimi!


Cc Zero IQ
Nimetoa laki moja tu, na nimekatwa hivyohivyo elfu sita kama wewe, kumbe kheri ya wewe umehurumiwa!! Hata hivyo inahuzunisha sana vile wanavyoorodhesha jinsi walivyozinyofoa...
 
Hivi Bi. Mkubwa hayumo humu tum-tag aone masikitiko ya mwanae?🤣
 
Umetoa 144,000.00 Tsh. Kwa wakala: JULIAS MASAWE.Makato Tsh 6,130.00( Ada Tsh 3,600.00 + Kodi Tsh 2,530.00).Salio Jipya Tsh 504.00. Muamala No: CO210730.1304.E58770


Wacha kabisa mkuu
Yaani umebakiwa na 504 kwenye Account???
 
jana nimeweka elfu 20 kwenye simu yangu nikataka kutuma kwa ndugu yangu..basi nikaambulia hivi;
nikatuma elfu 18...(nikakatwa 1160)
naye akaenda kuitoa akakatwa 2160
jumla makato 3320 nimelilia moyoni tu

akanipigia simu kunijuza nikamwambia bora usingesema maana nilivyoipata kwa shida unazidi kunihuzunisha moyo wangu bado nahitaji kuishi..msiniambie maumivu bora mkaushie tu. Serikali inatujaza hasira, inatutia huzuni, inatuongezea msongo wa mawazo, inatusukumiza kwenye kifo bila hata sababu.
Ila tuache utani Mwigulu ana ROHO MBAYA SANA
 
Back
Top Bottom