Namtafuta mwanaume atakayekuwa tayari kumuoa dada yangu

Kweli bado.Twasubiri ajitokeze mwenye nia nzuri.
Maalim tuyajenge.

Huu ni utaratibu mzuri nilishawahi kufanya hilo kwa binamu yangu.

Nami nilishawahi kumtafutia dadangu wa bibamu mume, nilichofanya nilikwenda kumshika rafiki na ndugu wa ndugu yangu, Nikamwambia napenda umuoe binamu yangu.

Nikafanya mchakato na huyu rafiki yangu kwanza amuone tu kwa sura ili kwanza aridhike. Kama asingeridhia na binamu yangu kutojua huwa haimpetei madhara yyt

Alipomuona nikamuuliza rafiki yangi kama karidhia. Akasema ndio.
Baada ya rafiki yangu kuondoka nikamfata binamu yangu nikamwambia yule uliyemtengea chai asubui ni rafiki na ndugu ya ndugu zangu na anataka kukuposa na nitakwenda kuwaambia wazazi wako. Na atakuja rasmi kwenu kukuona, mtaongea.

Napoongea hapa sasa wana miaka minne ktk ndoa na wana watoto wawili.

Muhimu atakaejitokexa kwako umuulize imam wa msikiti anaoswali. Na wewe utueleze imam was msikiti ambao huduma za kidini mnapata kutoka msikiti huo.

Pamoja na kuwa Nina fikra za kuongeza make mwenye sifa kama za huyo ukhti. Lkn kwa sasa nipo likizo ya muda mrefu. Sina kazi, sina biashara. Siku inavyopita mungu mwenyewe ndie anaejua.
 
Kama mtakua tayari niwaoe wote wawili basi tuanzeni mchakato
 
Allah atufanyie wepesi katika mazito yetu
 
Nimependa sana mchango wako na umenifurahisha kwa hitimisho lako.
Inaonekana wewe ni mtu mzuri.Siwezi kujua mawazo ya dada lakini kama maamuzi ya mwisho ni ya kwangu ningekuozesha kwa mahari kidogo sana.
 
Mimi nimeomba wewe uwe wa nyongeza
Utaomba vipi nyongeza kabla hujapokea cha mwanzo.Tungependa tukujue kama ni mwenzao au ni mwenzangu.Tukijua ni kama dada tutakutafutia dawa yako.
 
Kweli bado.Twasubiri ajitokeze mwenye nia nzuri.
Mkuu unamaana gan unaposema nia nzuri? Mimi ni miongoni mwa watu waliojitokeza pm yako na nikaweka sifa zangu lukuki ili maswali yasiwe mengi na baada kama wiki moja mhusika (dada yako) alinipigia simu wakati huo mimi nilikua kazini tena nilikua bize mno hivyo nilimkatisha bila ya kujua kama ni dada yako na kumwambia nitakucheki baadae nipo bize mno.

Lakini nilisahau kuirudia tena ile namba baada ya siku kama tatu alinipigia tena na kuanza kujitambulisha nami nilimpa ushirikiano wa kujitambulisha ila baada ya kuuliza kazi ninayofanya sikutaka kujivunga nikamwambia ukweli aiseee hapo maswali yalikua mengi sana na mwishowe aliahidi atarejea kunitafuta lakini hakunitafuta tena aliingia mitini

Jinsi inavyoonekana dada yako hamtafuti mtu mwenye sifa tajwa bali anamtafuta bwanyenye mwenye kazi nzuri na pesa zake na kama ataendelea hivyo sijui kama atafikia malengo simuombei mabaya huu ni mtazamo wangu tu kwa jinsi alivyonihoji nimejifunza kitu kutoka kwake

Bahati nzuri baada ya wiki moja nimeitwa kwenye kazi inayoendana na taaluma yangu.
VIJANA TUTAFUTE PESA KUOA MWANAMKE ALIYEKUZIDI KIPATO/MALI NI HATARI KWA AFYA YAKO.
 
Utaomba vipi nyongeza kabla hujapokea cha mwanzo.Tungependa tukujue kama ni mwenzao au ni mwenzangu.Tukijua ni kama dada tutakutafutia dawa yako.
Ewaa, hapo sasa ndiyo unakuja vizuri. Tutafutane basi Ami ake ili tuweze kuondoa doubts
 
Nimekusikia.Kwanza nashukuru kwa maelezo yako kila mmoja aliyewasiliana nasi ameona usalama na amejua ukweli halisi.Na nimefurahi inaonekana kwa mfumo wa JF majina yanayokuja kule kama ni tofauti na haya yanayojitokeza hapa kwa sababu wala sikuona jina lako hili ijapokuwa taarifa zako alinieleza dada.
Kuhusu kwamba dada anatafuta bwanyenye wala si sahihi.Anachotafuta ni stara yake na anatamani watoto katika umri wake huu.Kikwazo chake kingine hapendelei kuhamishwa kwenye mji wake.Anapenda kama mume si wa huku basi awe tayari kuhamishia shughuli zake waishi pamoja huku hata ikiwa si kwenye nyumba yake.Kwa sharti hili nimeshamuonya asiling'ang'anie na anaweza akawa amenielewa.
 
Ewaa, hapo sasa ndiyo unakuja vizuri. Tutafutane basi Ami ake ili tuweze kuondoa doubts
Wenzako wamejitokeza kwa dada.Wewe wataka utafutwe wapi.Hapo sasa ndio unaanza kueleweka jinsia yako.
 
Wenzako wamejitokeza kwa dada.Wewe wataka utafutwe wapi.Hapo sasa ndio unaanza kueleweka jinsia yako.
Mimi na wewe twende hivihivi mdogomdogo, The picture tutalijua huko mbele ya safari. Kwa sasa una rulsa ya kuongea yote😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…