Namtetea Mbowe, Chadema, Hakuna Ubaya Wowote, Mtu, Chama Kusaidiwa na Kupokea Fedha Zozote Toka Popote na Kwa Yeyote!. Sio Kila Pesa ni Rushwa!

Hapa ndiyo umeuvaa uccm wako barabara,maana maccm wote wanaomtetea Mbowe siyo kama wanampenda, na ni hao hao waliokuwa wanamng'ong'a kwa kuendekeza usultani,lakini baada ya kuona ni nani anajiandaa kuchukua kijiti cha uenyekiti ghafla wote mumekuwa watetezi wa Mbowe kwani mlitegemea angeingia mtu ambaye mtamfanya kama mlivyomfanya Mbowe. Turudi kwenye suala la hela inayolalamikiwa,suala siyo hela bali madhumini ya hiyo hela jee inaingizwa Chadema na kwa wanachadema ili ifanye nini. Nafikiri wewe mwenyewe unaona madhara yaliyoletwa na hiyo hela haihitaji miwani kuona hili tifu linaloendelea Chadema kuhusiana na hela ya Abdul na Mama yake. Au Paschal hujaona kuwa lengo la hela ya Abdul limefikiwa kwa 75% hadi sasa?
 
Huna na wala hujawahi kuwa na lolote
 
Mkuu ni wewe uliyeandika hivi?
Unatakatisha fedha ambazo kila kitu saiv kipo uwanjani Tundu lisu amefafanua? Unamjibia mbowe kwenda Ikulu baada kutoka jela kwamba alienda kumshukuru mama na kumsalimia wakati mwenyewe hajaeleza hivyo hadi jana Lissu katoboa? rushwa hata uipake rangi na kuinukisha harufu nzuri kwa kiwango unadhan itabadilika?

Mwache mwenyewe mtuhumiwa mbowe aueleze umma kwanini alienda ikulu break ya mwanzo alipotoka jela kabla hata kuonana na mama watoto wake. hili jambo lipo mezani lakini pia afafanue kuhusu ile tuzo ya bawacha na vitenge kumbe haikua ajenda ya chama

unataka kumtilia Lissu maneno mdomoni kwamba hakutakiwa kupewa burungutu ili anyamaze?
 
Bro, katika maisha unaweza ukawa umeachive vitu vingi sana ikiwa pamoja na elimu ila kama ukikosa msimamo, wewe ni FAILURE katika maisha.

Ifike mahali Mzee Paskali amua moja hata wanaoamini vitabu wanasema mungu hapendi mtu KINYONGA. Mzee PASKALI wewe unakosa hata TEUZI kwakuwa u wavuguvugu unauma na kupuliza.Hakuna anayekuamini, wanafiki siku zote ni WASALITI. Na hakuna anayetaka kuwa karibu na MSALITI.

Ukiamua kula kula, ukiamua kufunga kula funga kula.Usitake uonekane mzuri kwa kila mtu.Huu ni UNAFIKI katika kilele chake.

Waswahili wanasema mtaka yote,mkosa yote!!!


# wewe mzee jiheshimu,kaa chini ujitafakari. Unazidi kujishushia heshima na kufanya hata hiyo elimu yako idharaulike.
 
Mimi ni chadema roho na kweli. Lisu anachokifanya cha kuwanaga wenzake si chema...
sikiliza clip hii nimeweka uzi kabisa juu yake

View: https://youtu.be/rTWpnMO7kto?si=54k-QsjtgmlxtnQw
Kuunga mkono maridhiano haihalalishi kwamba hata maridhiano yasipo tekelezwa basii usiyakatae , maridhiano nikteka na kuuwa wanachama wa upinzani ? Mnataka aendelee kukubaliana na maridhiano ya aina hivyo?
 
kama wewe unavyojishushia heshima, umeandika nini sasa ? Jibu hoja za pascal
 
Nakumbuka nikiwa kwenye utumishi kule, kwanza ukipokea zawadi yoyote lazima ukaiandikishe kwa mkuu kuwa nimepewa zawadi hii.

Lakini pia, kama zawadi hiyo thamani yake inazidi 50k ilikuwa lazima ukaikabidhi zawadi hiyo ofisi kuu wao ndio wataamua wafanye nini na hiyo zawadi.

Sababu ilikuwa moja, bila kujali malengo ya mtoa zawadi, kitendo cha wewe kupokea zawadi tayari unakuwa compromised. Yaani subconsciously utakuwa unawiwa kulipa fadhila kwa mtu huyo.

Hivyo basi, kama Mbowe na CDM wamepokea zawadi yoyote, walipaswa kuisema kwa wanachama wao, wamepokea kutoka kwa nani na malengo yake ni yapi.

Kisha 'zawadi' hiyo iingizwe kwenye mfuko wa chama na kupangiwa matumizi na chama. Tena ikiwezekana wale waliohusika kuipokea basi wasishiriki kwenye kupanga matumizi.

Mbowe amepungukiwa uadilifu. Lissu amepungukiwa hekima lakini ni bora mara 100 kuliko Mbowe. Upinzani utafika mbali chini ya Lissu kuliko ndumilakuwili Mbowe.
 
Paskali you are so cheap, hivi hujui hata sheria inayokataza kutakatisha pesa? Unahalalisha pesa kwa sababu aliyetoa pesa amekujaa moyoni uko tayari kuharibu credibility yako sababu utetee rushwa iliyosemekana kutoka kwa mama Abdul?

Hela yeyote chafu kwenye taasisi kama CHADEMA sababu inahisiwa kutoka CCM ni sawa?

Umejenga heshima yako jf kwa muda mrefu sasa unaiharibu haraka sababu ya uchawa, it's a pity.
 
Shida siyo kupewa fedha, shida ni dhumuni la fedha unazopewa. Sasa mtu unaambiwa nakupa fedha ili usiiseme serikali! Hiyo ni fedha halali?
 
Ni pale mwana CCM anapojitokeza kutetea mambo asiyoyajua,hayamuhusu na hajaulizwa lakini yupo bize haswa!
 
Paskal umeanza kunifanya nifikirie zaidi juu kauli yako kuhusu pesa,yaani mtu akupe tu pesa,hakuna pesa inayotolewa kwa mtu kama zawadi,pesa haikuwahi kuwa zawadi,pesa ya namna hii ni rushwa na pia kuna vitu vikitolewa kwenye mazingira fulani ni rushwa tu what connect between chadema and ccm people?
ccm wamekuwa hodari sana kwa kuhonga vyama,wenyeviti wa vyama ili kuviuwa vyama,so Lissu kwa sasa ni threat kwa ccm,Mbowe amekuwa msuruhishi zaidi kuliko kuwa mpinzani so hawa watu wanatoa pesa kumbakisha mbowe
 
Wewe Mzee kichwa kimeganda tembelea mbuga kipindi hiki ili uwe sawa maana vitu vingine unavyotetea ni hatari kwako na Taifa..
 
MKuu Blaza Jei, brazaj , asante kwa bandiko hili Hongera Tundu Antipas Lissu kwa kutambua usalama wako unawajibika nao wewe mwenyewe, wengine wote hawaaminiki!
Japp naunga mkono hatua zozote mtu yeyote anazozichukua kulinda usalama wake,kwa mtu kuwa security conscious,ndio maana niliwalaumu kutochukua hatua madhubuti kulinda viongozi wake,Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?

Lakini kauli hiyo ni moja ya kauli zake ropo ropo zinazomuonyesha alivyo na upungufu wa busara kumchafua Mbowe kuwa ni muuaji anaweza kumuua kwa sumu!。

Japo Mbowe aliishia Form IV na alipata ile divisheni ya vijana,lakini Mbowe sio kilaza,sio kichaa,sio mwendawazimu,hata kama kweli ni muuaji wa kichini chini, hawezi kufanya ujinga wa kupanga kumuua lissu,amualike nyumbani kwake, amuandalie chakula halafu akitilie sumu ampe Lissu sumu nyumbani kwake!。 Nasema big no!。
Hata ile siku anarudisha fomu,kitendo cha kwenda huku amevaa bullet proof ni mockery kwa Chadema wasije kumuua!。

Anachofanya Lissu ni utovu wa shukrani kwa Mbowe kwa jinsi alivyomtesekea kuokoa maisha yake。

Japo mimii ni supporter mkubwa Lissu humu jf
Lissu apunguze u ropo ropo, asimchafue Mbowe ili angalau aweze kupata japo kura
mbili!, vinginevyo...
Na Mbowe akionewa pia namtetea Namtetea Mbowe, Chadema, Hakuna Ubaya Wowote, Mtu, Chama Kusaidiwa na Kupokea Fedha Zozote Toka Popote na Kwa Yeyote!. Sio Kila Pesa ni Rushwa!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…