Namtumbo: Wazazi waacha kupeleka Watoto Shuleni wakiaminishwa Yesu Kristo anakaribia kurudi

Kweli huwa mnaeenda kusomea ujinga, mnatutia aibu Tanzania hii
Bora nimtoe mtoto shule nimpeleke msumbiji akajishughulishe, kuliko kumtoa amsubiri tapeli mmoja alipaa na ungo
 
Labda akikuta watoto wako shule atakasirika sana manake walipenda awakute nyumbani wanamsubiri hata km ni miaka 800.
Atakua yesu wa mchongo mwanza toka apewe dozi hajaridi kila akisoma mchezo naaona ntakufa tena
 
Mtu kama huyu hastahili kuachwa hivihivi. Sijui aelimishwe kwa namna gani.

View attachment 2875334
Imani ni shambulio la akili
 
"....DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi"
Nashauri: Hao wakapumzishwe pale Kingolwira miezi 6 wakati msako una endelea, halafu ndo baadaye hayo mahojiano yaendelee.
 
Mfuasi wa Kibwetele huyo.

DINI ZINA WAPUMBAZA WATU WENGI SANA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
...Wale waliohamia pale Uwanja wa Ndege Dar wakiaminidhwa na Kiongozi Wao kwamba Watakwenda sijui Jerusalem bila kuhitaji Pasipoti Miaka ya Tisini na wakaanza kuchafua Uwanja Wetu wa Ndege Kwa Vinyesi Hadi wakatimuliwa na Polisi, kumbe nao walikuwa Dini Gani ??? [emoji848][emoji848][emoji848]

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Ila Wasabato bhana [emoji23][emoji23][emoji23]
Huyu jamaa alikua Msabato alikua anasali Nyegezi akahasi akafukuzwa kwa taratibu za Kanisa..Hivyo sio Mwadventista tena. ieleweke hivo kuwa sio Msabato na Wasabato wanahimiza watoto kwenda shule tena kwa mtaala wa sasa somo la dini ni la lazima kwa wanafunzi wote.
Somo linaitwa Sport Culture and Religion.
Huyo n muuni TU aliyechanganyikiwa
 
Huyo jamaa alishahasi Kanisa akafukuzwa alikua Msabato kwa Sasa sio Msabato tena
 
Biblia yenyewe inasisitiza watoto wapewe elimu yeye hayo ya Yesu kurudi na watoto kutokwenda shule kayatoa wapi?

Akamatwe akanyee ndoo huko jela kwa kosa la kupotosha raia
 
Another Mackenzie in town. Na bado kuna wajinga wamemwamini.
 
Mhubiri apewe adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine. Imani nyingine ni ",kichefuchefu "
 
Wanafunzi kadhaa wa secondary na msingi, wametolewa shule na Mchungaji na Muinjilisti Erick Manyanya, pamoja na wazazi wao, wakiwa kanisani, wakimsubiri Yesu arudi, huko Namtumbo.
 
Dini zingine ni majanga kwa jamii na taifa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…