Namungo FC yazuiwa Uwanja wa Ndege Angola

Timu ya Namungo kutoka Lindi Tanzania imexuiwa kuingia nchini Angola ikidaiwa wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana maambukizi ya Corona.

Timu hiyo imeamliwa kurejea ilikotoka na mamlaka za Angola.

Maendeleo hayana vyama!
 
Tatizo na mashaka na vipimo vyetu kama wanapima au wanachukuwa pesa tu na ku save chem za kupimia wakiandika negative tu. ndio maana hata Dubai Tanzania wako katika list hata kama umeonesha umepima ukifika ni lazima upime tena ni kama vile hatuamini.
Sas kama mkuu ashasema tz hamna korona hata wakipima wakakukuta nayo hawawezi kukuambia unayo.
 
Wawarudishe wanamichezo wetu waendelee na VPL, sasa wakikaa Karantini hiyo mechi itachezwa lini? Bora warudi maisha yaendelee.
 
Nashauri vilabu vinavyoshiriki mechi za kimataifa kuwapima na kuwafungia kambini wachezaji kabla ya kuondoka kwenda nje kwa ajili ya mechi...ili tujue kama kweli kinachofanyika ni figisu ama la. Kinyume na hapo hatuna haki ya kulalamikia figisu as hatuna uhakika kama ni kweli au la.
 
Tatizo na mashaka na vipimo vyetu kama wanapima au wanachukuwa pesa tu na ku save chem za kupimia wakiandika negative tu. ndio maana hata Dubai Tanzania wako katika list hata kama umeonesha umepima ukifika ni lazima upime tena ni kama vile hatuamini.
We nae jiongeze hizo ni figisu, hawa jamaa ata kaizer chief waliwafanyia figisu hizo.

Why hao wanne waliokutwa nao watengwe then wengine waruhusiwe wachezi mechi.

Ila na wao si watakuja humu tusubiri
 
JF
Namungo FC imezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.

Mpaka wakati wa kuandika taarifa hii timu ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uende karantini.

Namungo ipo Angola kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya kombe la shirikisho.

Taarifa zaidi zitafuata.

===========

NAMUNGO YAZUILIWA UWANJA WA NDEGE

Kikosi cha wachezaji wa Namungo fc wamezuiliwa uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola baada ya maafisa nchini humo kudai kuwa wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virus vya Corona.

Maafisa hao wamesema kuwa Namungo watatakiwa kufanya moja kati ya kurudi Tanzania au waende Quarantine.

Klabu hiyo yenye maskani yake huko Lindi iliondoka kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Primeiro De Agosto mchezo ambao utachezwa tarehe 14 Februari.

Namungo chini ya kocha wake Hemed Morocco inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 21 na kucheza michezo 16.

De Agosto iliingia kwenye kombe la shirikisho baada ya kushuka kutoka michuano ya klabu bingwa barani Afrika, baada ya kufungwa na Kaiser chiefs ya Afrika kusini.

Ni moja kati ya michezo miwili ya hatua ya mtoano ambapo mshindi wa matokeo ya ujumla kwamaana ya Nyumbani na Ugenini atafuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
 
Sijapenda lugha uliyotumia, HUKO LINDI, je ingekuwa Namungo inatoka Arusha, Mwanza, au Mbeya ungetumia hilo neno, Ifike sehemu muache huu ujinga , kwani ulikuwa unaripoti kutoka Luanda?
 
Mbona hata sisi tulizuia wachezaji karibia 5 wa Platinum wasicheze kwa sababu za covid? Waliopatokana na covid wakae pembeni mbungi ipigwe kama kawaida.
 
Timu ya Namungo kutoka Lindi Tanzania imexuiwa kuingia nchini Angola ikidaiwa wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana maambukizi ya Corona.

Timu hiyo imeamliwa kurejea ilikotoka na mamlaka za Angola.

Maendeleo hayana vyama!
Hii sawa mkuu, kitoka Lindi Tanzania, siyo kutoka huko Lindi.
 
Tanzania hamna Corona, tulimuomba Mungu maombi ya siku tatu ikaisha chini ya jemedari John Pombe Joseph Magufuli.

Angola wasitujaribu.
COVID 19Hakuna Hapa Tanzania
Angola Watajuta Kwenye Hili Jambo
Ambassador Wetu, Alifanyie Kazi Hili Jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…