Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Hello people.

Ndugu zanguni nina hali fulani hivi siielewi.

Nampenda sana shemeji yenu na kwa jinsi alivyo nimejikuta namuheshimu sana ila nahisi kama heshima imezidi hadi imegeuka woga hivi.

Japo huwa ananisaidiaga financially akijisikia ila nahisi ninamzidi kipato na simtegemei ila sijui kwanin sauti yake imekua na mamlaka sana kwangu,yaan nikisikia tu sauti yake sijui kwanini hata tone yangu inabadilika na kuwa ya upole na unyenyekevu mkubwa na huwa nalipima neno kabla ya kumwambia.

Kuna siku alinikasirisha sana na sikutaka tena kuendelea na mahusiano nae akawa akipiga sipokei then kwa hasira nikapanga akipiga nipokee then nimfokee nimjibu mbovu then nikate nimblock lakini cha ajabu nilivyopokea na kusikia sauti yake tu sikuweza tena kuongea nae kwa sauti ya ukali kama nilivyopanga na maneno makali niliyokua namwambia kwenye sms ukiniambia nimwambie kwa mdomo siwezi so nikaishia kuwa mpole kama mwanakondoo tu.

Sio mkatili wala sijalogwa ila nikimzingua ni mkali sana ila anajali na anajitahidi sana kunionesha upendo lakini sijui kwanini namuogopa hadi nakosa ujasiri wa kutoa madukuduku yangu kwake.

Mimi ni mwanamke.
Ukijitahidi kutokumheshimu mwanaume, utaachana nae na utampata mshenzi zaidi yake, na by the way anabeba mamlaka ya kiMUNGU aliyopewa kama mwanaume, tatizo ni moja tu kwamba utandawazi umewaharibu sana wanawake,yuko mtu anamhudumia mwanamke, anamlipia Kodi na pesa ya chakula, lakini huyo mwanamke ni mbabe mbabe mwenye kauli mbovu pale anapoulizwa hata tu mbona hajapokea simu zaidi ya masaa matatu, anakuja juu, anakata simu, anajifanya mjuaji na hana ujuaji wowote, anatoka familia masikini, hana kazi ya kueleweka, yaani ni mshenzi mshenzi sana, wanawake wengi wanaposemaga kua ntamblock mwanaume hua ni kiburi tu Cha kwamba wanaume wako wengi na anatongozwa kila siku, sasa utakua na wanaume wote? Heshimu wanaume mnaokua nao na aachecheni ujinga na ulimbukeni wa "NINA KAZI YANGU" sijui mala "NIMESOMA ASINIBABAISHE" mmejaa ujinga ujinga tu
 
Sijaona sababu ya wewe kuanzisha huu uzi
Mbona Uzi unaenda vizuri ujue alikuwa na sababu na ndo content zinazofurahiwa humu( halafu kwa ushauri usipende kukatisha wenzio ameandika ili kuona Kama yupo Sahihi wewe eti hujaona sababu
 
Ukijitahidi kutokumheshimu mwanaume, utaachana nae na utampata mshenzi zaidi yake, na by the way anabeba mamlaka ya kiMUNGU aliyopewa kama mwanaume, tatizo ni moja tu kwamba utandawazi umewaharibu sana wanawake,yuko mtu anamhudumia mwanamke, anamlipia Kodi na pesa ya chakula, lakini huyo mwanamke ni mbabe mbabe mwenye kauli mbovu pale anapoulizwa hata tu mbona hajapokea simu zaidi ya masaa matatu, anakuja juu, anakata simu, anajifanya mjuaji na hana ujuaji wowote, anatoka familia masikini, hana kazi ya kueleweka, yaani ni mshenzi mshenzi sana, wanawake wengi wanaposemaga kua ntamblock mwanaume hua ni kiburi tu Cha kwamba wanaume wako wengi na anatongozwa kila siku, sasa utakua na wanaume wote? Heshimu wanaume mnaokua nao na aachecheni ujinga na ulimbukeni wa "NINA KAZI YANGU" sijui mala "NIMESIMA ASINIBABAISHE" mmejaa ujinga ujinga tu
Umeongea kwa hisia mkuu.
Nimekuelewa.šŸ™
Kumuheshimu ni wajibu wangu.
Sitaacha

Kwa upande wangu block sio kiburi bali nakua nimechoka mauzauza mkuu.
 
Hawezi kuwa na michepuko.
Ananipenda sana.
Namuamini.
Na kama kumtii mwanaume wangu ni undondocha haina shida dini yangu imenifundisha kuwatii wanaume na ndio maana naogopa hata kumjibu vibaya
Na wewe muongo Sasa Kama kwa sms unaweza mjibu what the difference
 
Mbona Uzi unaenda vizuri ujue alikuwa na sababu na ndo content zinazofurahiwa humu( halafu kwa ushauri usipende kukatisha wenzio ameandika ili kuona Kama yupo Sahihi wewe eti hujaona sababu
Hajui kuwa sometimes mtu unaomba ushauri ukiwa tayari unajua jibu ila unataka tu kusikia mitazamo ya wengine ili kupata uhakika wa ambacho tayari unajua ila huna uhakika nacho
 
Na wewe muongo Sasa Kama kwa sms unaweza mjibu what the difference
There is a difference mkuu!
Niko huru kwenye text kuliko kwenye kuongea kwa sauti.
Ila sio kama namtext matusi au maneno machafu.
 
Hello people.

Ndugu zanguni nina hali fulani hivi siielewi.

Nampenda sana shemeji yenu na kwa jinsi alivyo nimejikuta namuheshimu sana ila nahisi kama heshima imezidi hadi imegeuka woga hivi.

Japo huwa ananisaidiaga financially akijisikia ila nahisi ninamzidi kipato na simtegemei ila sijui kwanin sauti yake imekua na mamlaka sana kwangu,yaan nikisikia tu sauti yake sijui kwanini hata tone yangu inabadilika na kuwa ya upole na unyenyekevu mkubwa na huwa nalipima neno kabla ya kumwambia.

Kuna siku alinikasirisha sana na sikutaka tena kuendelea na mahusiano nae akawa akipiga sipokei then kwa hasira nikapanga akipiga nipokee then nimfokee nimjibu mbovu then nikate nimblock lakini cha ajabu nilivyopokea na kusikia sauti yake tu sikuweza tena kuongea nae kwa sauti ya ukali kama nilivyopanga na maneno makali niliyokua namwambia kwenye sms ukiniambia nimwambie kwa mdomo siwezi so nikaishia kuwa mpole kama mwanakondoo tu.

Sio mkatili wala sijalogwa ila nikimzingua ni mkali sana ila anajali na anajitahidi sana kunionesha upendo lakini sijui kwanini namuogopa hadi nakosa ujasiri wa kutoa madukuduku yangu kwake.

Mimi ni mwanamke.
Eti sio mkatili wala sijalogwa,umejuaje kama hajakuloga,na kama sii mkatili unaogopa nini?inaonekana umempenda sana kwahiyo hujielewi...
 
Eti sio mkatili wala sijalogwa,umejuaje kama hajakuloga,na kama sii mkatili unaogopa nini?inaonekana umempenda sana kwahiyo hujielewi...
Yawezekana ni kweli nimempenda hadi sijielewi ila unataka niseme ni katili wakat sio?
Na ningekua nimelogwa nisingekua nafikiria kusepa.
Mim mtu akizingua mawazo ya kumuacha ni dk 1 tu na nikibaki ninakua nimeamua tu kuvumilia nikiwa na akil zangu
 
Eti sio mkatili wala sijalogwa,umejuaje kama hajakuloga,na kama sii mkatili unaogopa nini?inaonekana umempenda sana kwahiyo hujielewi...
Yawezekana ni kweli nimempenda hadi sijielewi ila unataka niseme ni katili wakat sio?
Na ningekua nimelogwa nisingekua nafikiria kusepa.
Mim mtu akizingua mawazo ya kumuacha ni dk 1 tu na nikibaki ninakua nimeamua tu kuvumilia nikiwa na akili zangu.
 
Umeongea kwa hisia mkuu.
Nimekuelewa.[emoji120]
Kumuheshimu ni wajibu wangu.
Sitaacha

Kwa upande wangu block sio kiburi bali nakua nimechoka mauzauza mkuu.
Basi katafute Dunia yako ya kuishi ili usikutane na unacho kutana nacho maana hakikwepeki hapa Duniani iwe kwa huyo au Kwa mwingine
 
Kuna jambo ambalo ulilifanya ukijuwa kwamba siyo sawa lakini ukalifanya bila yeye kujuwa hivyo unapomsikia unapata huna nguvu ya nafsi kwa sababu kuna jambo umelificha.
 
Basi katafute Dunia yako ya kuishi ili usikutane na unacho kutana nacho maana hakikwepeki hapa Duniani iwe kwa huyo au Kwa mwingine
Si bora mtu akublock kuliko maugomvi na matusi juu ndo ujue kakuchoka?

Mimi mwanaume akishanivua nguo ntaendelea kumuheshimu hata tukiachana so ni bora block kuliko wale wanaochana vibaya kwa matusi na kashfa.
 
Kuna jambo ambalo ulilifanya ukijuwa kwamba siyo sawa lakini ukalifanya bila yeye kujuwa hivyo unapomsikia unapata huna nguvu ya nafsi kwa sababu kuna jambo umelificha.
Sina lolote baya nimewahi mfanyia mkuu.
Im a very loyal woman.
Nikipenda huwa sitizami pembeni
 
Back
Top Bottom