Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Mchizi mwenyewe sasa

FB_IMG_1675375753319.jpg
 
Ndo inavotakiwa kuwa ww ulitaka uwe mkali umekuwa mwanaume
Kwa hiyo sina kasoro mkuu?

Lakin si inashauriwa kwenye mahusiano pakiwa na shida mkae muyaongee?Sasa mim nabakia kulia tu au kuitikia tu,hata kumbishia siwezi au hata kumkatisha akiwa anaongea siwezi hata kama nina hasira na unakuta nina vitu nataka kusema.

Nikikabwa sana nakimbilia kumuandikia sms kwa mdomo siwez kumwambia.Na akikasirika ni mkali hata ukilia hajali
 
Hello people.

Ndugu zanguni nina hali fulani hivi siielewi.
Nampenda sana shemeji yenu na kwa jinsi alivyo nimejikuta namuheshimu sana ila nahisi kama heshima imezidi hadi imegeuka woga hivi.

Japo huwa ananisaidiaga financially akijisikia ila nahisi ninamzidi kipato na simtegemei ila sijui kwanin sauti yake imekua na mamlaka sana kwangu,yaan nikisikia tu sauti yake sijui kwanini hata tone yangu inabadilika na kuwa ya upole na unyenyekevu mkubwa na huwa nalipima neno kabla ya kumwambia.

Kuna siku alinikasirisha sana na sikutaka tena kuendelea na mahusiano nae.Akawa akipiga sipokei then kwa hasira nikapanga akipiga nipokee then nimfokee nimjibu mbovu then nikate nimblock lakini cha ajabu nilivyopokea na kusikia sauti yake tu sikuweza tena kuongea nae kwa sauti ya ukali kama nilivyopanga na maneno makali niliyokua namwambia kwenye sms ukiniambia nimwambie kwa mdomo siwezi so nikaishia kuwa mpole kama mwanakondoo tu.

Sio mkatili wala sijalogwa ila nikimzingua ni mkali sana ila anajali na anajitahidi sana kunionesha upendo lakini sijui kwanini namuogopa hadi nakosa ujasiri wa kutoa madukuduku yangu kwake.

Mimi ni mwanamke.
Wanawake kama wewe huwa wanaitwa vindondocha. Huwa kazi yao ni kutii kila anachoambiwa na mumewe halafu mapenzi na waume zao huwa hayanogi kitu kinachofanya wanaume kupenda mchepuko zaidi na kuwaacha wake zao kama vyombo vya kuzaa.
 
Back
Top Bottom