Huu ndiyo ukweli kwenye ulimwengu wa sasa suala la binti kuolewa au kutokuolewa inabidi lichukuliwe kuwa jambo la kawaida tu tena kama bahati tu.
Maana ukitaka kuliweka kama kipaumbele kwako au kwa mwanao huchelewi kujiua au kujidhuru na pia kumsababishia mwanao msongo wa mawazo.
Hebu acha suala la ndoa libaki kwa wale watakaobahatika na kama hakupata mume au mke basi mtu asinyanyapaliwe kama siyo kutafutiwa mume au mke ulimwengu umebadilika lazima tuendane nao.