Mkuu so kwamba sijaelewa interview ila kama anaona top 5 hafit angesema tu so kudanganya na hapa town ana nyimbo 6
Sio kwamba anadanganya ila alichokifanya Kwenye muziki majigambo ni kitu cha kwaida kabisa isitoshe ukiweka list ya wasnii wanaopiga shows nyingi Nandy huwezi acha kumtaja
:::::::::::::::::::::;:::::
Nandy ataja kinachompa pesa tofauti na muziki
FRIDAY , 24TH FEB , 2017
Msanii muziki wa bongo fleva mwanadada Nandy amebainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii nchini Tanzania wanaoingiza kipato cha juu bila ya kutegemea muziki.
Mrembo huyo amesema kuwa amefungua kampuni yake binafsi inayojihusisha na utengenezaji wa nguo za kitenge, mikoba, nguo za harusi pamoja na mavazi mengine ya utamaduni inayojulikana kwa jina la Nandy African Print.
"Nilianza ujasiriamali tokea nipo chuo kabla masuala ya muziki hayajachanganya vizuri nilikuwa naenda kununua nguo Kariakoo halafu ninazipamba vizuri kwa kutumia vitu vya asili".Alisema Nandy
Aidha msanii huyo amesema mpaka sasa ameweza kutoa ajira kwa watu watano ambao ni mafundi wanajishughulisha na utengenezaji wa nguo za asili yaani mafundi cherehani.
"Sijakurupuka kufungua kampuni yangu kwani nilijipanga muda mrefu tokea kipindi ninashiriki mashindano ya muziki nchini 'Nigeria' nikasema nikishinda lazima nitimize lengo langu la muda mrefu, nilianzia na mtaji wa milioni 10 kwa ajili ya kununulia vifaa pamoja na kulipia kodi".Alisema msanii huyo
Kwa upande mwingine msanii huyo alisema malengo ya kampuni yake ni kuhudumia ndani na nje ya nchi kwa kutoa mavazi ya asili yenye ubora zaidi."
unaweza sema kwa biashara hii anayofanya Ni bado hastahili kuwa top 4 Ni kweli lakini jiulize anmishe gani zingine anazopiga kimyakimya bila kuzitangaza au kujulikana?
kina Diamond/Allikiba nawengine ulowataja hapo juu unadhani pesa walizonazo zinatoka kwenye shows /matangazo na muziki pekee fatilia watu kama jay moe. Nyandu tozz jux na wengineo sio watu wanao tegemea muziki pekee wanaharakati zao zingine tofauti kabisa na wanapiga money ya kutosha