Mwanamuziki Nandy amevunja ukimya baada ya kukutana na walezi wa sanaa BASATA kufuatia mjadala mkubwa wa vazi alilovaa kwenye fainali za Miss Universe.
Nandy amefafanua kuwa hakuwa utupu kama wengi walivyodhani, bali vazi hilo lilitengenezwa kwa kitambaa kinachofanana na rangi ya ngozi yake.
Amesema alienda BASATA akiwa na nguo hiyo kuionyesha, na amelishukuru baraza hilo kwa mazungumzo ya kujenga.
"Mimi ni binti wa Kitanzania siwezi kukaa utupu wa kiasi kile, ni ubunifu tu! Siku nyingine msistukee," amemalizia Nandy huku akiwatoa hofu mashabiki zake waliopata taharuki.
#Nandy #BASATA #Burudani #Mitindo #Tanzania