Nani alitudanganya sisi wamatumbi kuwa AZUMA , ni dawa ya U.T.I?

View attachment 3676092
Kuna thread fulani tuliwahi kuzungumzia kwa uchache kuhusu hili...

Tatizo kubwa watu wana kukariri ujinga,
Ungenitag Mkuu.
Kuna wakati nilikuwa na UTI kali sana ikanitibu chap, na imenitibu mara nyingi sana siyo mara moja tu.
. Sasa kama siyo dawa ya UTI ni dawa ya nini?

Nachojua hii dawa ni Antibiotic, kwamba inaua bacteria. Na ukiangalia UTI ina sababishwa na bacteria walio kwenye utumbo mkubwa waitwao Escherchia Colli (E. Colli), sasa kwanini mtu useme kwamba hii dawa haitibu??
 
Mkimaliza kwenye tiba ya UTI mje kwenye upimaji wenyewe wa UTI, huko ndiko tatizo linakoanzia.
Kama siyo dawa ya UTI inatibu nini?
Mimi ninachojua ni kwamba imenitibu UTI mara nyingi sana.
Kwa hapa Tanzania, hospital zinazo pima U. T. I, haziwezi kufika hospital hata 20.. 🤝 🤝.
 
Azuma sio dawa sahihi ya UTI sawa tumeelewa ila mnaulizwa dawa sahihi ni ipi? hamtaki kujibu.
 
Azuma sio dawa sahihi ya UTI sawa tumeelewa ila mnaulizwa dawa sahihi ni ipi? hamtaki kujibu.
Dawa zipo nyingi kutegemea na hali ya mgonjwa na pia kutegemea na aina ya bakteria aliyesababisha hiyo UTI.
 
Dawa ni kile kinachokuponya, mengine ni mbwembwe za madaktari tu. Nakukumbusha tu kuwa dawa maarufu ya tumbo ni fragyl😀
 
Hao watumiaji ni wajanja kuliko uwajuavyo. Wao wanaenda famasi kununua AZUMA wakisema wanaumwa UTI lakini kiukweli wagonjwa hao na wafamasia wote wawili wanakuwa wanajua huyo mgonjwa anaumwa nini! Ahahahahaha!!
Cheza na Mbongo weweee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…