Nani alitudanganya sisi wamatumbi kuwa AZUMA , ni dawa ya U.T.I?

Nani alitudanganya sisi wamatumbi kuwa AZUMA , ni dawa ya U.T.I?

waache kuchamba kuelekea mbele (hasa wanawake)wachambe kurudi nyuma kutatua tatizo kwanza kujua chanzo cha tatizo. na waache ile michezo na wakifanya wasiwe wana badili cd ovyo katikati ya wimbo kama dj ni hatari

pia wazingatie usafi binafsi na aina ya material za nguo wanazotumia hasa za ndani kiujumla
Kwa kuongezea wanywe maji mengi kabla na baada ya tendo , wamalize mkojo wanapoenda kujisaidia haja ndogo.
 
Hivi huwa nashangaa mbona UTI wanaumwa wanawake na km kisa ni kufirana, mbona mashoga hawaumwi UTI?
nature au lugha nyingine female anatomy ni tofauti na mwanaume ivyo Ecoli(ambaye huishi kwenye ule uchafu )huathiri urethra pindi mwanamke akikubali kubadilisha cd katikati ya mziki. au akiwa ananawa kuanzia nyuma kwenda mbele hubeba chembechembe nakuzizogezea pali zikiwa na huto mdudu huleta hayo madhara.

pia kutumia mate kama lubricant humweka kwenye risk mana hudhoofisha wale bacteria rafiki kwake tofauti na shoga.
 
Kwa kuongezea wanywe maji mengi kabla na baada ya tendo , wamalize mkojo wanapoenda kujisaidia haja ndogo.
hii hufanya kazi kwa wepesi sana kwa mwanaume ila mwana mke huchukua muda sababa ya ile anatomy yake ilivyo kaa kumbuka njia ya mkojo na unapoingia huwa ni tofauti ingawa wengi hawalijui hili😃
 
Mkimaliza kwenye tiba ya UTI mje kwenye upimaji wenyewe wa UTI, huko ndiko tatizo linakoanzia.
Hapo kuna shida mbili.
1) Mpimaji akiwa na colour blindness

2) Kutozingatia muda wa kipimo.

Mwingine anasoma kipimo muda ambao sio sahihi, utakuta anasoma kipimo dakika zimeshapita za kutosha, wengine zinafika mpaka dakika 15 .

Kiuhalisia kipimo cha uti majibu yake inabidi yatolewe ndani ya dakika 2, zikizidi dakika 2 majibu yatakayotolewa yatakuwa false results.
 
Hivi kumbe ni kweli Azuma sio dawa ya UTI, kuna mtu ni Dr. Alikua ananieleza hiki kitu, sikua naamini, ila sasa wengi ndio wanajua na hadi hao Watoa huduma za Afya, wanafanya hivyo.
Tatizo watu wanachanganya UTI na magonjwa ya ngono,kuna baadhi ya magonjwa ya ngono mfano Chlamydia mgonjwa anaweza kupewa Azuma lakini yeye kwa kutojua kutofautisha Chlamydia na UTI ataenda kusema nimepewa Azuma kwa sababu nilikuwa naumwa UTI ilihali hakuwa anaumwa UTI. Shida ipo hapa kwenye wagonjwa kudogodesha magonjwa ya ngono kwa kuyaita UTI.
 
Hivi huwa nashangaa mbona UTI wanaumwa wanawake na km kisa ni kufirana, mbona mashoga hawaumwi UTI?
UTI wanaumwa wote wanawake na wanaume ila wanawake wanaumwa zaidi kwa sababu sehemu ya mkojo ya mwanamke ipo karibu na sehemu ya haja kubwa kwahiyo ni rahisi bacteria wanaosababisha UTI kuhama kutoka kwenye njia ya haja kubwa na kufika kwenye njia ya mkojo na kuleta maambukizi. Kwa mwanaume hadi bakteria atoke kwenye njia ya haja kubwa na afike kwenye njia ya mkojo sio rahisi lakini inawezekana. Ndio maana watu wanaambiwa wajisafishe kutoka mbele kwenda nyuma na sio kutoka nyuma kwenda mbele.
 
Tatizo watu wanachanganya UTI na magonjwa ya ngono,kuna baadhi ya magonjwa ya ngono mfano Chlamydia mgonjwa anaweza kupewa Azuma lakini yeye kwa kutojua kutofautisha Chlamydia na UTI ataenda kusema nimepewa Azuma kwa sababu nilikuwa naumwa UTI ilihali hakuwa anaumwa UTI. Shida ipo hapa kwenye wagonjwa kudogodesha magonjwa ya ngono kwa kuyaita UTI.

Hii ni sawasawa mkuu ni Claymidia ipo sana kuliko hiyo UTI yenyewe, inakuwa asymptomatic sometime hasa kwa wanawake ndio maana wakitumia Azithromycin wanapona na kwa sababu mtaalam kamwambia una UTI hajataka kueleza ni ugonjwa wa zinaa basi wanabaki na uelewa kuwa Azithromycin inatibu UTI.
 
Kumekua na wimbi la wadanganyika wakiamini kuwa AZUMA ( Azithromycin ) ni dawa za kutibu UTI .


Hii kitu imesambaa sana kiasi cha wimbi kubwa la watu wakizibugia kama pipi , huku wakiamini watapona UTI.

Sijui maamlaka zipo wapi , au labda na mimi ni mlevi na mjinga tu , sijui kama Azithromyicin almaarufu kama AZUMA kuwa ni dawa za kutibu bacteria wa UTI🤔

Ngoja wajuzi wa mambo waje🍺
130258.jpg

Kuna thread fulani tuliwahi kuzungumzia kwa uchache kuhusu hili...

Tatizo kubwa watu wana kukariri ujinga,
 
Kumekua na wimbi la wadanganyika wakiamini kuwa AZUMA ( Azithromycin ) ni dawa za kutibu UTI .


Hii kitu imesambaa sana kiasi cha wimbi kubwa la watu wakizibugia kama pipi , huku wakiamini watapona UTI.

Sijui maamlaka zipo wapi , au labda na mimi ni mlevi na mjinga tu , sijui kama Azithromyicin almaarufu kama AZUMA kuwa ni dawa za kutibu bacteria wa UTI🤔

Ngoja wajuzi wa mambo waje🍺
Kama siyo dawa ya UTI inatibu nini?
Mimi ninachojua ni kwamba imenitibu UTI mara nyingi sana.
 
Back
Top Bottom