H r n
JF-Expert Member
- Oct 3, 2019
- 1,100
- 2,079
Habari wakuu,
Kuna jambo nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwenye jamii yetu. Watu wengi huamini kwamba kuhama nyumba ni jambo linalopaswa kufanyika usiku, kiasi kwamba mtu akihama mchana huonekana kama amefanya kitu kisicho cha kawaida.
Binafsi najiuliza, hii dhana ilianzia wapi? Je, kuna sababu za msingi zinazofanya watu wahame usiku zaidi kuliko mchana, au ni mazoea tu yaliyojengeka kwenye jamii?
Kwa mtazamo wangu, kuhama ni kuhama tu, iwe mchana au usiku. Kila muda una faida na changamoto zake. Lakini bado wengi wanaonekana kuhusisha kuhama usiku na usiri, uchumi wa gharama, au hata imani fulani za kijamii.
Je, wewe unaonaje? Umewahi kuhama mchana au usiku? Unafikiri kwa nini watu wengi hupendelea kuhama usiku?
Karibuni kwa maoni na uzoefu wenu.