Nani alitufundisha kwamba kuhama nyumba ni usiku pekee?

Habari wakuu,

Kuna jambo nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwenye jamii yetu. Watu wengi huamini kwamba kuhama nyumba ni jambo linalopaswa kufanyika usiku, kiasi kwamba mtu akihama mchana huonekana kama amefanya kitu kisicho cha kawaida.

Binafsi najiuliza, hii dhana ilianzia wapi? Je, kuna sababu za msingi zinazofanya watu wahame usiku zaidi kuliko mchana, au ni mazoea tu yaliyojengeka kwenye jamii?

Kwa mtazamo wangu, kuhama ni kuhama tu, iwe mchana au usiku. Kila muda una faida na changamoto zake. Lakini bado wengi wanaonekana kuhusisha kuhama usiku na usiri, uchumi wa gharama, au hata imani fulani za kijamii.

Je, wewe unaonaje? Umewahi kuhama mchana au usiku? Unafikiri kwa nini watu wengi hupendelea kuhama usiku?

Karibuni kwa maoni na uzoefu wenu.
Braza Meni shame mchana Godoro ulimi wa Mbwa?
 
aiseee 😁😅😅
Direct_ConvertGif_1781184582735.gif

Sasa familia inahama na vitu vyote vimeenea kwenye bodaboda pamoja na family members, Kwann tusihame usiku 😂
 
Na ukiwa na pesa Huwez kuhamia sehemu ya kichovu hvy hutokuwa na presha ya kukimbizana kuhama usiku ety watu wasione mali zangu waje kuiba 😂
Hahaha wakiona tv yangu ya nchi 75 itakuwaje so ukiona hivyo mtu anahamia uswahili masaki huko hawana mambo hayo😃
 
Mm mwnyw baadhi ya vitu vyangu nilivibeba kwenye boda mana sikuwa na haraka ya kuhama, mana nilihamisha Vitu mdogo mdogo, Sasa unahamisha labla TV pekee yake utaiweka kwenye gari au kwenye boda
Issue ni tutafute pesa hata mchana unahama
 
Habari wakuu,

Kuna jambo nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwenye jamii yetu. Watu wengi huamini kwamba kuhama nyumba ni jambo linalopaswa kufanyika usiku, kiasi kwamba mtu akihama mchana huonekana kama amefanya kitu kisicho cha kawaida.

Binafsi najiuliza, hii dhana ilianzia wapi? Je, kuna sababu za msingi zinazofanya watu wahame usiku zaidi kuliko mchana, au ni mazoea tu yaliyojengeka kwenye jamii?

Kwa mtazamo wangu, kuhama ni kuhama tu, iwe mchana au usiku. Kila muda una faida na changamoto zake. Lakini bado wengi wanaonekana kuhusisha kuhama usiku na usiri, uchumi wa gharama, au hata imani fulani za kijamii.

Je, wewe unaonaje? Umewahi kuhama mchana au usiku? Unafikiri kwa nini watu wengi hupendelea kuhama usiku?

Karibuni kwa maoni na uzoefu wenu.
Mara nyingi huwa ni privacy! Unakuta mtu ana masufuria, magodo au furniture chakavu au hata vitu vya thamani ambavyo wezi wanaweza kuvutika. Kwa kifupi watu wanakwepa jamii kujua undani wa wanavyomiliki. Pia sehemu unayohama au kuhamia, kuna wengi tu ahawataki ku-attract attention ya mtaa mzima.
 
So wanaosema sijui wezi sijui usiri sijui usalama ni balabala tu issue ni hela
Hy pia n sababu ila sio sababu kubwa.
Mtu unaenda kuishi uswahilini kwa watu waliochoka automatically Huwez kuwa na mali zitakazowavutia wezi, Ukiona Una mali Za kuwavutia wezi bc tafuta mtaa wa kuendana na hali ya uchumi wako.
 
Mara nyingi huwa ni privacy! Unakuta mtu ana masufuria, magodo au furniture chakavu au hata vitu vya thamani ambavyo wezi wanaweza kuvutika. Kwa kifupi watu wanakwepa jamii kujua undani wa wanavyomiliki. Pia sehemu unayohama au kuhamia, kuna wengi tu ahawataki ku-attract attention ya mtaa mzima.
Kwa hii point yako ishu sio privacy, bali ni umasikini tuu
 
Back
Top Bottom