Nani alitufundisha kwamba kuhama nyumba ni usiku pekee?

Nani alitufundisha kwamba kuhama nyumba ni usiku pekee?

1. Kunaepusha husda na uchawi miongoni mwa majirani na maadui wa familia. 2. Ni utamaduni tu uliojengeka tangu kale,hata wanyama mfano paka wana tabia za kuhama usiku 3. Kuepusha aibu, imagine mtaani ulikuwa unasimulia wewe huwezi kulalia godoro inchi 1 wakati unahama unahama na sandarusi iliyojazwa pamba.
Una tatizo mpaka hapo huwezi ukawa unasimulia watu unalalia godoro gani ni ujinga kiwango cha lami huwezi akawa unajieleza kwa watu unamiliki vitu fulani na huna ni utoto
 
Habari wakuu,

Kuna jambo nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwenye jamii yetu. Watu wengi huamini kwamba kuhama nyumba ni jambo linalopaswa kufanyika usiku, kiasi kwamba mtu akihama mchana huonekana kama amefanya kitu kisicho cha kawaida.

Binafsi najiuliza, hii dhana ilianzia wapi? Je, kuna sababu za msingi zinazofanya watu wahame usiku zaidi kuliko mchana, au ni mazoea tu yaliyojengeka kwenye jamii?

Kwa mtazamo wangu, kuhama ni kuhama tu, iwe mchana au usiku. Kila muda una faida na changamoto zake. Lakini bado wengi wanaonekana kuhusisha kuhama usiku na usiri, uchumi wa gharama, au hata imani fulani za kijamii.

Je, wewe unaonaje? Umewahi kuhama mchana au usiku? Unafikiri kwa nini watu wengi hupendelea kuhama usiku?

Karibuni kwa maoni na uzoefu wenu.
Hao wanaohama usiku ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine mkuu. Ni sawa na baadhi ya watu ukimpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto anakuona mshirikina. Sasa kama mkono wa kushoto ni mkono wa laana kwanini Mungu aliamua kuitenganisha? Si angeweka tu mikono yote miwili mkono wa kulia?

Mimi sijawahi kuhama usiku. Nahama mchana kweupe mkuu. Kuhama usiku ni uzezeta. Ni zaidi ya wauza duka mazezeta amabao hawauzi sindano au chumvi usiku. Watanzania wamejaa mawazo ya kishirikina na kilofa.
 
Ngoja waje, ila nadhani ni kwa sababu wengi hutumia magari ya wazi kwenye usafirishaji, jambo ambalo siyo salama...


Cc: Mahondaw
 
Mk
Hao wanaohama usiku ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine mkuu. Ni sawa na baadhi ya watu ukimpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto anakuona mshirikina. Sasa kama mkono wa kushoto ni mkono wa laana kwanini Mungu aliamua kuitenganisha? Si angeweka tu mikono yote miwili mkono wa kulia?

Mimi sijawahi kuhama usiku. Nahama mchana kweupe mkuu. Kuhama usiku ni uzezeta. Ni zaidi ya wauza duka mazezeta amabao hawauzi sindano au chumvi usiku. Watanzania wamejaa mawazo ya kishirikina na kilofa.
Mkuu umewasimanga kwa uchungu mno wanakuja
 
Kama mizigo yako haifungwi kwenye ma box maalumu, jua mambo yako bado makorokoro lazma yaamishwe usiku😆😆
 
Back
Top Bottom