The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Inawezekana kabisa kwamba magufuli alikuwa na madhaifu yake, na inaweza isiwe dhambi kumsema vibaya. Ila kwa watu wenye malengo ya kutafuta kura Kwa wananchi wa kawaida walipaswa kupotezea kabisa habari za magufuli.
Kuna baadhi ya mambo ambayo hata Magufuli angekuwepo naamini asingebadili chochote lakini alishawaaminisha watu Imani ambayo ni ngumu kufutika katika kizazi kilichowahi kuyaona na kuyasikia maamuzi yake.
Ukweli ni kwamba kumsema vibaya Magufuli ukiondoa kujipoza machungu na kuwapoza machungu wahanga wachache wa utawala wake hakuna tija yoyote linapohusika suala la kuongeza kura.
Magufuli mwenyewe alizoea kuwasema vibaya watangulizi wake lakini alitenda jambo lililowaaminisha watu kuwa inawezekana ni kweli watangulizi wake walikuwa na shida.
Unapomponda Magufuli huku vitu vinapanda bei, umeme unakatika hovyo rushwa na urasimu na mauzauza mengi serikalini unakua hujui unalotenda.
Licha ya matatizo ya Magufuli lakini sio uongo kwamba bado ana waumini wake wengi pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote wa hivi karibuni hapa nchini. Hivyo hata kama unamchukia kwa kiwango gani Kwa ajili ya kulinda kura ni bora ukapitezea kabisa mada zinazomhusu.