Nani aliwadanganya CHADEMA wamponde Hayati Magufuli majukwaani!!? Hili jambo litawanyima kura miaka elfu

Nani aliwadanganya CHADEMA wamponde Hayati Magufuli majukwaani!!? Hili jambo litawanyima kura miaka elfu

Lini Tanzania haijawahi kuwa na Matatizo?

Kama ni ufisadi kwani kipindi cha Magufuli haukuwepo?- Si ni Magufuli alitutangazia Kangi Lugola na Andengenye wamepiga dili kwenye kandarasi ya polisi, akawatumbua, kisha hakuwafikisha mahakamani na huyo Andengenye akamfanya mkuu wa mkoa wa Kigoama. Hapo kuna kupambana na ufisadi hapo?
Hoja yangu ni kwamba tuzungumzie matatizo yaliyopo tuache kupaza sauti kuhusu mtu ambaye hatunae lkni namna tunavyomuongelea sanasana tunaisaidia ccm izidi kuwa comfortable
 
Uongozi wa Chadema nadhani hawaitaji kura za Wananchi wa Tanzania ili waendelee kuwemo kwenye ulingo wa Siasa. Ni fikra fikirishi hii usiipuuze!!!
 
Hata ungekuwa wewe, yale Magufuli aliwatendea CHADEMA wacha wateme nyongo!
Ukiwa na viongozi wanaowaza kutema nyongo basi utakuwa na viongozi wabovu sana katika kizazi hiki hawa chadema wangekuwa Mandela si wangeongea hadi siku wanaingia kaburini?
Ukiwa na kaliba ya mkombozi huwa unapotezea haraka sana yaliyokupata na kujenga dalaja la ukombozi
 
Wewe una hoja ila hata kama wafuasi wa magufuli wasingekuwa na chaguo chadema wangekuwa kwenye position nzuri sana kujaza hilo gap walipaswa kuja na majibu yanayopwaya sasa na si kumsengenya magufuli. Kwa akili yangu ya kawaida tu naamini Kwamba kwenye kampeni za 2025 ingawa amekufa bado atakuwa kiini kikuu cha mijadala mingi miongoni mwa wagombea
Utakuwa na matatizo ya afya ya akili watu wanaosema hadharani uovu wa Magufuli we unasema wanamsengenya? Sukumagang mnapwaya Magufuli hana na hatokuwa na influence yeyote kwenye uchaguzi wa 2025.

Rais Samia ni mjuzi wa siasa ingawa katoka chama kikongwe chakavu, kawashtukia sukumagang na upuuzi wenu kaamua heri awe na ukaribu na CHADEMA kuliko wapuuzi sukumagang ndani ya CCM.

Kama Magufuli alikuwa na ushawishi uchaguzi wa 2020 asingeuiba uchaguzi mzima mzima, kama akiwa hai alishindwa kusimama na CHADEMA kwenye uchaguzi huru na haki akaamua kuupora, kuua, kuwakamata wagombea wa CHADEMA kuwafungulia kesi na kuwaibia kivuli chake akiwa kaburini kitawatesa?

You are deluded umechanganyikiwa
 
Nyie wapumbv na wajinga huyo mjinga Mapombe aliharibu nchi akaua watu ,akapiga risasi so mlikuwa hamuoni wajinga nyie huyo Jamaa yenu

Aliharibu na matundu ya baadhi yenu sio nchi peke yake.
 
Mimi ni CHADEMA lakini kwa suala hili chama kinazingua sana, kuna haja gani ya kuhangaika na mtu aliyetangulia kwa Mungu?
CHADEMA haijawahi na haitokuwa na wafuasi wajinga kiasi hiki, Fascist Hitler, Stalin, Idi Amin na wengineo wamekufa miaka mingi lakini bado wanasemwa kwa maovu yao, wew ni chizi siyo CHADEMA
 
Hoja yangu ni kwamba tuzungumzie matatizo yaliyopo tuache kupaza sauti kuhusu mtu ambaye hatunae lkni namna tunavyomuongelea sanasana tunaisaidia ccm izidi kuwa comfortable
Hakuna mwenye time na mwendazake, ila tuna time na kuusema udhalimu wake ili tusirudie makosa kuwapa dhamana watu kama yeye au kuyanormalize makosa hayo.

Tusipokemea mambo ya wasiojulikana, kupora pesa za wafanyabiashara, kuvunja katiba na kuonea watu vitajirudia
 
Hicho ni chama cha hovyo sana Si bure mpaka sasa hakina hata ofisi na si bure miaka yote inaisgia kuwa failure kwenye chaguzi, Hivi unaanzaje kumuongelea vibaya Magufuli mbele ya watanzania na utegemee watakuelewa? Hapo ndipo walipofeli, Wananchi hawana umeme, maji mgao n.k laiti kama wangejikita kuongelea hayo na kuchukua yale mazuri ya JPM wangeshinda kwa kishindo.
Sukumagang utawajua kwa hoja zao za kipumbavu, chama cha hovyo serikali ingekubali kukaa nao na kufikia maridhiano? Magufuli anayependwa na watanzania kwa nini hakukubali uchaguzi huru na haki?

Wanaomsifia ni sukumagang na wagonjwa wa akili
 
Kwa kweli wanatuangusha sana sie tunao acha shughuri zetu na kwenda kuwasikiliza.
 
Inawezekana kabisa kwamba magufuli alikuwa na madhaifu yake, na inaweza isiwe dhambi kumsema vibaya. Ila kwa watu wenye malengo ya kutafuta kura Kwa wananchi wa kawaida walipaswa kupotezea kabisa habari za magufuli.

Kuna baadhi ya mambo ambayo hata magufuli angekuwepo naamini asingebadili chochote lakini alishawaaminisha watu Imani ambayo ni ngumu kufutika katika kizazi kilichowahi kuyaona na kuyasikia maamuzi yake.

Ukweli ni kwamba kumsema vibaya magufuli ukiondoa kujipoza machungu na kuwapoza machungu wahanga wachache wa utawala wake hakuna tija yoyote linapohusika suala la kuongeza kura.

Magufuli mwenyewe alizoea kuwasema vibaya watangulizi wake lakini alitenda jambo lililowaaminisha watu kuwa inawezekana ni kweli watangulizi wake walikuwa na shida.

Unapomponda magufuli huku vitu vinapanda bei, umeme unakatika hovyo rushwa na urasimu na mauzauza mengi serikalini unakua hujui unalotenda.

Licha ya matatizo ya magufuli lakini sio uongo kwamba bado ana waumini wake wengi pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote wa hivi karibuni hapa nchini. Hivyo hata kama unamchukia Kwa kiwango gani Kwa ajili ya kulinda kura ni bora ukapitezea kabisa mada zinazomhusu.
Mimi na familia yangu,wapangaji wangu,Majirani zangu na wote wanaokuja nyumbani kuchota Maji ni waumini wa kuu wa huyu Mzee,kuna vijana hapa mtaani kwangu wanatimu inaitwa JPM na ni team yenye Mashabiki wengi mtaani kwetu na inadhaminiwa na wazee wa jeshi walistaafu.
 
Watu wamesahau jinsi akina Dr Slaa walivyounanga utawala wa Mkapa baada ya kutoka madarakani mwaka 2006 hadi 2010, ishu za buzwagi, kagoda, ndege ya rais, Meremeta etc

Watu wanataka maovu ya utawala wa Magufuli yasisemwe kisa kafa, kafa yeye nchi haijafa!
 
Inawezekana kabisa kwamba magufuli alikuwa na madhaifu yake, na inaweza isiwe dhambi kumsema vibaya. Ila kwa watu wenye malengo ya kutafuta kura Kwa wananchi wa kawaida walipaswa kupotezea kabisa habari za magufuli.

Kuna baadhi ya mambo ambayo hata magufuli angekuwepo naamini asingebadili chochote lakini alishawaaminisha watu Imani ambayo ni ngumu kufutika katika kizazi kilichowahi kuyaona na kuyasikia maamuzi yake.

Ukweli ni kwamba kumsema vibaya magufuli ukiondoa kujipoza machungu na kuwapoza machungu wahanga wachache wa utawala wake hakuna tija yoyote linapohusika suala la kuongeza kura.

Magufuli mwenyewe alizoea kuwasema vibaya watangulizi wake lakini alitenda jambo lililowaaminisha watu kuwa inawezekana ni kweli watangulizi wake walikuwa na shida.

Unapomponda magufuli huku vitu vinapanda bei, umeme unakatika hovyo rushwa na urasimu na mauzauza mengi serikalini unakua hujui unalotenda.

Licha ya matatizo ya magufuli lakini sio uongo kwamba bado ana waumini wake wengi pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote wa hivi karibuni hapa nchini. Hivyo hata kama unamchukia Kwa kiwango gani Kwa ajili ya kulinda kura ni bora ukapitezea kabisa mada zinazomhusu.
Nakupinga vibaya sana ! Shetani ana wafuasi wengi kuliko Magufuli lakini anapingwa siku zote na ataendelea kupingwa tu
 
Nadhani wamepewa hayo masharti. Wanashindwa ongelea kupanda kwa gharama za maisha, tatizo la ajira, ufisadi na matumiz mabya ya pesa za umma. Wanashindana na marehem
 
Back
Top Bottom