Inawezekana kabisa kwamba magufuli alikuwa na madhaifu yake, na inaweza isiwe dhambi kumsema vibaya. Ila kwa watu wenye malengo ya kutafuta kura Kwa wananchi wa kawaida walipaswa kupotezea kabisa habari za magufuli.
Kuna baadhi ya mambo ambayo hata magufuli angekuwepo naamini asingebadili chochote lakini alishawaaminisha watu Imani ambayo ni ngumu kufutika katika kizazi kilichowahi kuyaona na kuyasikia maamuzi yake.
Ukweli ni kwamba kumsema vibaya magufuli ukiondoa kujipoza machungu na kuwapoza machungu wahanga wachache wa utawala wake hakuna tija yoyote linapohusika suala la kuongeza kura.
Magufuli mwenyewe alizoea kuwasema vibaya watangulizi wake lakini alitenda jambo lililowaaminisha watu kuwa inawezekana ni kweli watangulizi wake walikuwa na shida.
Unapomponda magufuli huku vitu vinapanda bei, umeme unakatika hovyo rushwa na urasimu na mauzauza mengi serikalini unakua hujui unalotenda.
Licha ya matatizo ya magufuli lakini sio uongo kwamba bado ana waumini wake wengi pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote wa hivi karibuni hapa nchini. Hivyo hata kama unamchukia Kwa kiwango gani Kwa ajili ya kulinda kura ni bora ukapitezea kabisa mada zinazomhusu.
Jambo hili halifanyiki kwa bahati mbaya,kwa sababu wale wanaoyafanya haya.tunawajua na tunawaelewa historia zao.Ni ushirika ulioundwa makusudi ili kutimiza malengo yao upya.
Ndio hao wanaogawana keki ya nchi hii kama ilivyokuwa mazowea kabla ya 2015.
Wengine wakijiita walamba asali.
Kuanzia EPA,RICHMOND MEREMETA, SYMBION POWER na ma uozo lukuki yaliykuwa yameichungulisha kaburi "CCM."
Ikiwemo na ile HOME SHOPPING CENTER ambayo sasa ndio SILENT OCEAN. Ambayo Mzee Asali Junior aliwauxia kiwanja cha CCM.kinyemela wakati akiwa K/M CCM asali ilee!
Ambapo sasa ndio makao makuu yao hao "Bahari kimya".
Pale alipoingia Magufuli na kuanza kuusafisha huu uozo.
Na ndipo CCM na wafuasi wake walipopata nguvu mpya ya kukijenga upya chama.
Hadi leo wanapopata nafasi ya kumsimanga wakati akiwa hayupo tena mbele za familia yake!
*Magufuli kafa na kuacha...
*IKULU mpya ya Chamwino.
*ATCL mpya.
*SGR Mpya.
*Nyumba mpya za Magomeni.
*Mabweni Mapya UDSM.
*Daraja jipya la Tanzanite.
*Daraja jipya la Wami.
*Bwawa jipya la umeme JNHP.
*Stendi kuu za mabasi za kisasa Dodoma,Morogoro na Mwanza.
*Meli mpya Ziwa Victoria na ukarabati wa Mv Victoria.
*Meli Mpya ziwa Nyassa.
*Ndege na Helikopta mpya jeshini.
Pia kanunua Rada mpya nne nchini na kuondoa utegemezi wa Rada za Kenya.
Akafhibiti utoroshaji madini Mererani kwa kujenga ukuta na akaanzisha madoko huru ya madini nchi nzima.
Akazuia utoroshaji wa fedha kupitia utitiri wa Bureau de change mitaani.
Akarudisha nidhamu kwa watumishi sekta ya Umma na hakusita kutumbua mtu kwa uzembe hata kama alikuwa rafiki yake kama Charles Kitwanga.
Akaondoa vyeti feki na mushahara hewa nchi nzima.
Amekufa na kuiacha Tanzania ikiwa uchumi wa kati tukiwa kasi ya ukuaji ya 7.1%.
Yote haya ameyafanya ndani ya miaka mitano.halafu wajinga fulani wanajikusanya na kudhani wanaweza kuja kuizima legacy ya mtu kama huyu kwa kusjiri wajinga fulani mitandaini ili kumtukana?
Itakuwa ngumu sana hilo kutokea na labda mkabomowe hiyo miradi na kuwauwa wale wote wanamkubali na kumkumbuka Magufuli.