Nani aliwadanganya Watanzania kuwa maziwa ni tiba ya mtu aliyemeza sumu?

Nani aliwadanganya Watanzania kuwa maziwa ni tiba ya mtu aliyemeza sumu?

Jamaa alichokisema ni kweli kabisa.
Maziwa kwenye swala la sumu hayana utofauti na maji ya kunywa. Vyote kazi yake ni kudilute sumu.

Na ndio maana hata kwenye matibabu ya sumu zilizomezwa hakuna tiba ya kumpa maziwa.

Ila activated Charcoal inatumika
 
Sayansi ndogo.....Adsorption.
Activated carbon ita attract cations zije kwenye Surface yake.
Najua ni useful kwenye water and waste water treatment.
Kwenye Sumu sijui, ila kama ina cations zinazoweza kuvutika Might work.
Ila lazima ina side effect kwenye mwili.
 
Sayansi ndogo.....Adsorption.
Activated carbon ita attract cations zije kwenye Surface yake.
Najua ni useful kwenye water and waste water treatment.
Kwenye Sumu sijui, ila kama ina cations zinazoweza kuvutika Might work.
Ila lazima ina side effect kwenye mwili.
Hata carbon ya kukamatia dhahabu inafanya kazi namna hiyo.
 
Tuwekane sawa kwanza.

Maziwa yanasaidia kwenye sumu ingawa sio moja kwa moja.

Maziwa yana protini na ndani ya protini kuna amino acid.

Baadhi ya kazi za protini ni ukuaji, kurekebisha seli za mwili.

Pia protini inahusika katika chembe seli nyekundu za damu ambazo zinaunda haemoglobin yenye kazi kubwa ya kusafirisha oksijeni.

Kuna aina mbalimbali za sumu na hutegemea kiwango au dozi pamoja na mahali inapoweza kudhuru au kuleta madhara katika mwili.

Sumu huweza kuleta madhara katika seli, tishu, ogani, mfumo au kudhuru kiumbe moja kwa moja.

Kwa sababu sumu ina athari inapoingia katika mwili hivyo basi njia moja wapo ya kusaidia mwili au seli ni matumizi ya protini kama virutubisho ambavyo vinapatikana katika maziwa pia.

Kwa hiyo inatarajiwa mtu anapotumia sumu ni muhimu pia kupata virutubisho vya protini.

Ingawa nakubaliana na wewe kuwa dhana ya maziwa kutumika kama antidote/kigeuza - sumu au kikata - sumu imekuwepo muda mrefu sana.

Mwisho tunaishi katika dunia iliyozungukwa na sumu sumu sumu kuanzia tunavyotumia, kunywa na kula hata hewa tunayovuta.

Pia ikumbukwe kuwa maziwa yana placebo effect ambayo ni chanya na inasaidia kuleta utulivu wa akili na mwili kwa muhanga aliyekunywa sumu kwa kuondoa hofu hasa katika huduma ya kwanza.
 
Back
Top Bottom