Nani aliwahi kuhoji haya kipindi cha Magufuli?

Nani aliwahi kuhoji haya kipindi cha Magufuli?

Bondpost

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2011
Posts
7,019
Reaction score
10,455
Ndugu zangu watanzania, wakati tunaendelea kujadili siasa za nchi yetu ni vema tuangalie serikali zilizopita na ya sasa kwa kuangalia namna ambavyo kumekuwa na tofauti katika utendaji wake wa mambo mbalimbali.


Leo hii napenda kuwauliza wenzetu wanaopenda kuweka ulimganyo wa utendaji wa serikali ya Magufuli n Samia. Labda tujiulize yafuatayo kuhusu serikali ya Magufuli ili tuilinganishe na hii iliyopo especially kwenye masuala ya mikopo inayolalamikiwa na mikataba;

Nani amewahi kuona mkataba wowote unajadiliwa Bungeni?

📑Nani amewahi kuona mkataba wa mkopo?

📑Nani amewahi kuona mkataba wa Stiegler’s Gorge, SGR, Bandari ya Bagamoyo?

📑Nani ameuona mkataba wa manunuzi ya Ndege?

📃Lini ripoti ya CAG imeongelea mikopo?

Tujihoji huku tukiangalia uwazi ambao umekuwepo sasa wakati wa kusainiwa hii mikataba.

I submit.
 
Jibu ni hakuna..!
Namna hiyo basi tulikuwa kwenye hatari kubwa sana mtu mmoja kujiamulia bila hata kutaka ushauri wa mihimili mingine ya kikatiba iliyopewa jukumu Hilo la kushauri kabla ya kutenda.

Ni vema sasa tupitie Ile mikataba Kama ambavyo nae alipitia mikataba ya gesi na bandari ya Bagamoyo ili tupate ushauri wa kitaalamu zaidi maana yawezekana tunalipishwa madeni ambayo sio halisi.
 
Magufuli hayupo Hata mumchukie vipi Hayupo
Chukizenu hazita wasaidia Kitu
Mtatafuta kila Baya dhidi yake
lakini Yule Alikuwa Zaidi ya Rais kwa Tanzania muacheni Apumzike
Bado haujajadili hoja bwana mzee, hapa Kuna hoja na viroja. Kuhusu mikataba unasema alikuwa zaidi ya Rais naelewa wengine mlimuita Mungu nk hicho ni koroja.

Kuhusu kumuacha hapana tutamjadili matendo yake maana hata wanaomsapoti wanalilia legacy yake iendelee kuwepo otherwise wasingeililia legacy.

So no heri ujibu hoja au ukae kimya tu kwakuwa unaweza kukuta umegutuka .
 
Ninacho kumbuka ni mwanzoni mwa utawala wa magufuli alitowahi kutoa maelekezo mikataba yote ya madini iende bungeni. Ilipofika bungeni serikali ikavuliwa na akina Lisu na Mnyika na mbowe na kina Zito akaona kumbe aliingia cha kuruhusu mikataba bungeni. Hapo sasa ndio iliundwa timu ya wasiojulikana kupiga shaba watu kama nguruwe, kuteka kumpoteza kila aliyekosoa. Nilikuja kumchukia na kumdharau sana mwendazake kwa ujinga mkubwa kiasi kile
 
Wakati wa shetani yule nani angejadili chochote kwa vile yeye alikuwa ameiteka nyara nchi. Alikuwa anafanya anachopanga na kuamua yeye. Bunge lilikuwa la kwake,serikali ndo usiseme kwa maneno yake mwenyewe alisema ni mhimili uliokuwa umejichimbia chini zaidi na mahakama nayo alishaiteka JM alikuwa anamtetemekea kama muungu. Kwa kifupi taifa lilikuwa chini ya vyombo. Katika mazingira hayo nani angejadili mikatababa ambayo hata ilikuwa haijulikani jinsi ilivyokuwa inaingiwa?
 
Mikataba na mikopo haijawahi kuwa wazi kwa wananchi na kujadiliwa kwa upana, toka enzi za Nyerere. Magufuli asihukumiwe kwa hilo. Kwani sasa hivi mikataba iko wazi? Inajadiliwa na kuchambuliwa kwa uwazi? La msingi tujiulize pia, kwa nini viongozi wanakwepa jambo hilo?
 
Naamini mama anayafatilia kimya kimya huko. Nna imani sana na mama, anaupiga mwingi. Juzi karuhusu muswada wa kuwazuia polisi wasikamate mtuhumiwa kama hawajakamilisha upelelezi. Sijui ataisaini lini ili ianze kutumika rasmi.
 
katika awamu hii ya 6 uwazi umeongezeka sana. ila kuna kama dalili kama vile Mchwa/kupe/wpigaji/wabadhirifu/mafisadi wameanza kujipenyeza tayari kwa mashambulizi.
ni muhimu udhibiti uwe ule ule uliotumika ktk kipindi cha Hayati JPM.

JPM alidhibiti sana Mchwa/kupe/wapigaji/wabadhirifu/mafisadi.
kundi hili ni htari sn kwa ustawi wa Taifa letu, kundi hilo ndio hurudisha maendeleo ya wananchi nyuma, yaani ukiwatizama usoni ni kama watu lkn ndani ya mioyo yao ni htari zaidi ya wanyama.

Kwenye Udhiti hakuna budi njia aliyo itumia Hayati JPM itumike ipasavyo.
 
Kwan kwa sasahivi ni mikataba ipi ipo wazi. Au mkishaambiwa tumekopa USD kadhaa kwa riba nafuu ndio mkataba ushakuwa wazi huo. Haijawahi tokea mikataba ikawekwa wazi kwa wananchi tokea Tz izaliwe
Mkuu hivi ni kwa nini mikataba haiwekwi wazi? Na kwa nini hao wenye wajibu wa kupitia hiyo mikataba haiwekwi wazi? Wameshindwa kutimiza wajibu wao? Nini kinawatatiza kutowajibika ipasavyo? Au wanakrimiwa vyakutosja na muhusika wa mikataba? Ebu enyi wenye elimu, ufahamu na ujuzi TUJUZENI tujie.
 
Nani amewahi kuona mkataba wa mkopo?

📑Nani amewahi kuona mkataba wa Stiegler’s Gorge, SGR, Bandari ya Bagamoyo?

📑Nani ameuona mkataba wa manunuzi ya Ndege?

📃Lini ripoti ya CAG imeongelea mikopo?
Yaani kwa miaka takribani sita report ya CAG Haikuwahi kuonyesha deni la taifa yaani mkopo wa taifa una hali gani!!?

Yaani Shughuli zote za ujenzi wa Stiegler's Gorge, SGR hatukuambiwa chochote kuhusu misingi ya utekelezaji wake!!? Ile kwamba inajengwa kwa fedha za ndani nayo hatukusikia walipaswa wasambaze na BOQ.kama.nakala za rasimu ya katiba😂😂 na kwamba mkataba wa ujenzi wa bagamoyo port una ukakasi pia hatuambiwa eti ndugu yangu?

Alafu ndege nazo hatukuambiwa chochote yaani walisema tu bei na kwamba zimelipwa full kwanini hawakutusambazia risiti tuone na user manual ya bombardier zetu jamn!!?

Tunashukuru uongozi wa awamu ya tano na nusu (5.5) chini ya aliyekuwa makamu wa Raisi kwenye awamu ya tano kamili kwa kuwa na uwazi mkubwa hayo hayapo tena kwakweli mama anaupiga mwingi sana yaani haijawahi kutokea kiongozi wetu jasiri na mbunifu mzalendo wa kweli 🤣🤣🤣
YAANI MIJITU MINGINE NI YA HOVYO HADI INAKERA UNAFIKI TU
Unafiki mbaya sana unakutoa ufahamu na uwezo wa kufiriki kabisa kama huwezi kuuacha at least upunguze
Awamu ya Tano ilifanya mengi sana makubwa na yasiyoweza kudhihakiwa na yeyote mwenye fikra timamu
 
Tofauti ya Magu na marais wengine Huyu Mzee Nchi ameijenga bwana,Halmashauri nyingi zimepata majengo yake binafsi tena majengo smart chini ya uingozi wake.

Mkuu tembea Tanzania hii ujionee maajabu ya Magu mzee.

Ukipita chalinze pale kuna kighorofa cha halmashauri mzee utafikiri kimall flan hivi kumbe jengo la serikali.

Tofauti ya mikataba ya sasa na ya magu ni kuwa mikataba ya Magu uliona majengo mapya mazuri ya serikali yakijengwa ila kwa sasa tegemea nyumba nzuri na za kisasa za watu binafsi zikichipuka kama uyoga.
 
Mkuu hivi ni kwa nini mikataba haiwekwi wazi? Na kwa nini hao wenye wajibu wa kupitia hiyo mikataba haiwekwi wazi? Wameshindwa kutimiza wajibu wao? Nini kinawatatiza kutowajibika ipasavyo? Au wanakrimiwa vyakutosja na muhusika wa mikataba? Ebu enyi wenye elimu, ufahamu na ujuzi TUJUZENI tujie.
Kabla ya kutia sahihi mkataba inatanguliwa majadiliano kwa pande zote zitakazohusika.
Kama kuna mapungufu yanaanzia kwenye majadiliano. Ukiona serikali inatumia nguvu nyingi kutotaka mikataba kuwekwa wazi ni dalili ya mapungufu yaliyomo.
Wakati mwingine yawezekana sio hongo lakini wakashindwa au wakazidiwa ufundi wa kujadili.
Wapo wengine wako inferior kwa mtu mweupe nayo ina impact kubwa.
 
Ndege nane mpya hakuna tuliposogea?. Kupata chetu kwenye madini yetu hakuna tuliposogea?.

Madaraja yanayolipamba jiji la Dar kutokea hewani, hakuna tuliposogea?. SGR na busisi hakuna tuliposogea?.

Unaweza kuwa unamkufuru Mungu kwa kulalamika bila ya hoja za msingi.
Unanunua ndege afu huna vibali vya kurusha long haulage,inakusaidia nini?

Madaraja hayajaanza kujengwa leo na hayatakaa yaishe kujengwa.

Nchi ilikuwa kwenye mkwamo mkubwa kiuchumi miaka yote 6 iliyopita na idadi ya maskini iliongezeka.
 
Ndege nane mpya hakuna tuliposogea?. Kupata chetu kwenye madini yetu hakuna tuliposogea?.

Madaraja yanayolipamba jiji la Dar kutokea hewani, hakuna tuliposogea?. SGR na busisi hakuna tuliposogea?.

Unaweza kuwa unamkufuru Mungu kwa kulalamika bila ya hoja za msingi.
Kwa hiyo ndege ndio kibali cha kuchapa watu shaba?
 
Back
Top Bottom