Nani aliye Msafi ndani ya CCM??

Nani aliye Msafi ndani ya CCM??

Mifumo na itikadi za CCM hazizalishi product ya "wanyanganyi na manyangau wa kuhujumu taifa hili" T
Kama CCM haizalishi watu wa aina hiyo ni kwa nini wametamalaki ndani ya chama hicho??

Taja ufisadi wowote ule wa mali za Umma za watanzania ambao ndani mwake hakuna wana CCM.

Mpaka leo CCM imesema nini kuhusu zile 1.5 ten zilizopoea wakati Magufuli akiwa rais???

Uchafu ndani ya CCM unaendeshwa kimfumo na wala siyo kwa kufuata tabia binafsi ya mtu

Hivi leo CCM inakosa mtu wa kumpa nafasi ya Ukatibu mwenezi wa Taifa mpaka wampe Makonda pamoja na kashfa zote zile alizonazo????
 
Shida ni kipimo kinachotumiwa kupima usafi vipimo vingi vimekuwa vikitoa majibu ya jumla mbaya zaidi hata ukikitumia kujipima mwenyewe majibu ni yaleyale.

Inawezekana sisi wengine tunaonekana ni wasafi kwasababu hatujapewa nafasi ya kufanya kazi kwenye hizo fursa.

Kuna siku Dada mmoja alikuwa anatafuta nafuu kutokana na kutotendewa haki kuanzia mwenyekiti wa kijiji,Polisi,Mahakama,Mkuu wa wilaya na Mkuu wa MKOA washauri asilimia tisini wamemwelekeza kwenda kwa Makonda! Mimi nimebakia na swali kichwani hivi kumbe Makonda anaaminika kwamba ndiyo suluhisho la dhuluma hapa nchini? Basi kama ndivyo tupate wengine angalau kumi watusaidie kuondoa uozo katika huduma za mwananchi mnyonge.
 
Nani ndani ya CCM anaona kutumia ghiliba,dhuluma, wizi au rushwa kupata ushindi kwenye chaguzi ni jambo baya??

Nani aliye msafi ndani ya CCM???
CCM watu safi, wamo wa kumwaga!. Mimi namfahamu jamaa mmoja aligombea Kawe, hakutoa hata senti moja kwa yeyote na matokeo yake alipata kura 1!.

Hivyo wasafi wa type hiyo CCM wapo wengi tuu.
P
 
Usafi unazuia uchawa...

Huyo jamaa yako unayemsema ni chawa balaa na huwa hajali anasema nini ili mradi tu kama anachosema kinawafurahisha mabosi wake wa CCM.
 
Kama CCM haizalishi watu wa aina hiyo ni kwa nini wametamalaki ndani ya chama hicho??

Taja ufisadi wowote ule wa mali za Umma za watanzania ambao ndani mwake hakuna wana CCM.

Mpaka leo CCM imesema nini kuhusu zile 1.5 ten zilizopoea wakati Magufuli akiwa rais???

Uchafu ndani ya CCM unaendeshwa kimfumo na wala siyo kwa kufuata tabia binafsi ya mtu

Hivi leo CCM inakosa mtu wa kumpa nafasi ya Ukatibu mwenezi wa Taifa mpaka wampe Makonda pamoja na kashfa zote zile alizonazo????
Ndugu Allen unyangau na ulafi wa Mali za umma ni hulka ya mtu, inawezekana wahuni wanatumia nembo ya CCM kama kichaka cha kuficha maovu yao binafsi, Sidhani kama miiko, na miongozo ya CCM inahalalisha "Ufisadi na Uzandiki".
CCM ni ya Wajamaa na Wakulima, endapo wapo wahuni ndani ya Chama ni Jukumu la Chama kuwatambua na kuwaengua, Sio wote wanaojitambulisha kama Wana CCM ni CCM kweli wengineo ni vibaka wasio hata na kadi ya Chama wenye Nia ovu na rasilimali za umma, Suala la Makonda si agenda tena kisiasa, pengine sijui kwanini unataka iwe ni agenda.
 
, inawezekana wahuni wanatumia nembo ya CCM kama kichaka cha kuficha maovu yao binafsi, Sidhani kama miiko, na miongozo ya CCM inahalalisha "Ufisadi na Uzandiki"
Hao CCM wasafi mbona ni kama wao wapo wachache na hao wahuni ndiyo wapo wengi?

Kimantiki walio wengi ndiyo huwa utambulisho wa kundi.
CCM ni ya Wajamaa na Wakulima,
Aisee!!!

Wewe jamaa ulikuwa kwenye koma ndiyo Leo umezinduka???

CCM iliacha kitambo sana kuwa chama cha kijamaa na wakulima. Sasa hivi CCM ni chama cha wapiga Dili.
 
Nani ndani ya CCM hajawahi kutumia cheo chake kwa manufaa yake binafsi??

Nani ndani ya CCM anaona kutumia ghiliba,dhuluma, wizi au rushwa kupata ushindi kwenye chaguzi ni jambo baya??

Nani ndani ya CCM anayesikitika fedha za Umma zinavyokwapuliwa na wajanja wachache waliomo ndani ya Chama hicho??

Ni mwana CCM gani anayesikitika fedha za Umma kuingizwa kwenye miradi isiyo na kichwa Wala Miguu??

Nani aliye msafi ndani ya CCM???
CCM wote ni ukoo wa panya. Hakuna mwenye nafuu hata mmoja.
 
Nani ndani ya CCM hajawahi kutumia cheo chake kwa manufaa yake binafsi??

Nani ndani ya CCM anaona kutumia ghiliba,dhuluma, wizi au rushwa kupata ushindi kwenye chaguzi ni jambo baya??

Nani ndani ya CCM anayesikitika fedha za Umma zinavyokwapuliwa na wajanja wachache waliomo ndani ya Chama hicho??

Ni mwana CCM gani anayesikitika fedha za Umma kuingizwa kwenye miradi isiyo na kichwa Wala Miguu??

Nani aliye msafi ndani ya CCM???
Wasafi waliondoka awamu ya pili. Kwa sasa kuna #wahuni, chambilecho Mh. Polepole.
 
Nani ndani ya CCM hajawahi kutumia cheo chake kwa manufaa yake binafsi??

Nani ndani ya CCM anaona kutumia ghiliba,dhuluma, wizi au rushwa kupata ushindi kwenye chaguzi ni jambo baya??

Nani ndani ya CCM anayesikitika fedha za Umma zinavyokwapuliwa na wajanja wachache waliomo ndani ya Chama hicho??

Ni mwana CCM gani anayesikitika fedha za Umma kuingizwa kwenye miradi isiyo na kichwa Wala Miguu??

Nani aliye msafi ndani ya CCM???
Afanye kama anajikuna ajitenge na wenzie
 
Je, Utampata wapi Malaika kwenye Ngome ya Mashetani?
 
Nani ndani ya CCM hajawahi kutumia cheo chake kwa manufaa yake binafsi??

Nani ndani ya CCM anaona kutumia ghiliba,dhuluma, wizi au rushwa kupata ushindi kwenye chaguzi ni jambo baya??

Nani ndani ya CCM anayesikitika fedha za Umma zinavyokwapuliwa na wajanja wachache waliomo ndani ya Chama hicho??

Ni mwana CCM gani anayesikitika fedha za Umma kuingizwa kwenye miradi isiyo na kichwa Wala Miguu??

Nani aliye msafi ndani ya CCM???
Watakuwaje wasafi wakati hawataki KATIBA??
Na wewe huo usafi utaupimaje wakati hakuna KATIBA??
 
Hao CCM wasafi mbona ni kama wao wapo wachache na hao wahuni ndiyo wapo wengi?

Kimantiki walio wengi ndiyo huwa utambulisho wa kundi.

Aisee!!!

Wewe jamaa ulikuwa kwenye koma ndiyo Leo umezinduka???

CCM iliacha kitambo sana kuwa chama cha kijamaa na wakulima. Sasa hivi CCM ni chama cha wapiga Dili.
Ndugu Allen sipo kwenye koma na sijawai kuwa huko, Mungu epusha mbali, nipo vizuri, " Upigaji upo na upo kweli kweli" lkn sio Manifesto ya Chama, huo ni ugonjwa unaohitaji tiba, Japo zama zimebadilika kiuchumi na kisiasa, lkn bado fikra za kijamaa na Ukulima zinaishi miongoni mwa Watanzania.
 
Usafi unazuia uchawa...

Huyo jamaa yako unayemsema ni chawa balaa na huwa hajali anasema nini ili mradi tu kama anachosema kinawafurahisha mabosi wake wa CCM.
Mtu yoyote makini hawezi kuwa chawa!, huyo jamaa sio chawa na hajawahi kuwa chawa!, jamaa ni very objective, kwenye mazuri anapongeza na kwenye mabaya anakosoa!, chawa kamwe hawezi kukosoa!.
P
 
Back
Top Bottom