Nani aliyemwambia 'Kiboko ya Wachawi' akimbie Nchini baada ya Kanisa lake la Kitapeli Buza Kufungiwa?

Nani aliyemwambia 'Kiboko ya Wachawi' akimbie Nchini baada ya Kanisa lake la Kitapeli Buza Kufungiwa?

Tumelala sana, yani hata pastor aliejichubua anatutapeli.....

Mhuni Promax yule.
Alikuwa Anachamba watu popote hata akiwa madhabahuni.
Anaongea mambo ya chupi na shanga popote.
Yaani kwa kweli tulipatikana.
Iła kwa Hela amejua kuzipiga.
Mamilioni ya Hela.

Sijui yeye na wale vijana wake wavaa macheni walikuwa hawapigi hesabu za mbele kuwa mchezo huu mwisho wake utakuwa lini? Na utakuwaje?
Na Kwamba hawakufikiri kuwa mwisho utakuwa mbaya?
Dhamiri zao zilikufa kiasi cha kushindwa kujua kuwa Hela huwa ni adimu na hupatikana kwenye mazingira magumu na Kwamba hizi tunazowaibia kuna wakati wowote kitanuka?
 
Humu JF tumo wengi na ndugu na jamaa jamaa katupiga Hela ndefu.

Mimi huwa ni mgumu sana na huwa niko very suspicious lakini Huyu jamaa ndio maana nakwambia atakuwa alikuwa na nguvu fulani ya Nuru au ya Giza isiyo ya kawaida na ndio ilikuwa inampa kiburi na jeuri ya namna ile.
 
Itakuwa kuna masharti hakuyazingatia au Mwenyezi Mungu tu kaamua kuingilia kati baada ya kuona vimezidi.
 
Hela hupatikana ktk mazingira magumu ya ku-hustle,
Sasa yeye aliona ni rahisi tu kuwasmbia Lete 500,000/- kidają kalete 2,000,000/- tumalizie tatizo.

Afadhali alivyokimbia labda mkamateni mkewe wazitapike Hela za watu walizotapeli.

Mke aisaidie polisi ili apatikane jamaa aje kujibu tuhuma zake za wizi kwa njia ya ulaghai zinazomkabili.
Iwe fundisho.

Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa Uhunzi.

Mkewe aisaidie polisi jamaa apatikane na lile genge lake.
 
Pesa haipatikani kirahisi kiivyo kaletę laki 5 kisha kalete milioni unaletewa na hustuki kiwa hii ni hatari ni swala la muda tu bomu litalipuka?

vema watu wangepona na kuondokana na shida zao lakini aaah! 🤔
 
Mhuni Promax yule.
Alikuwa Anachamba watu popote hata akiwa madhabahuni.
Anaongea mambo ya chupi na shanga popote.
Yaani kwa kweli tulipatikana.
Iła kwa Hela amejua kuzipiga.
Mamilioni ya Hela.

Sijui yeye na wale vijana wake wavaa macheni walikuwa hawapigi hesabu za mbele kuwa mchezo huu mwisho wake utakuwa lini? Na utakuwaje?
Na Kwamba hawakufikiri kuwa mwisho utakuwa mbaya?
Dhamiri zao zilikufa kiasi cha kushindwa kujua kuwa Hela huwa ni adimu na hupatikana kwenye mazingira magumu na Kwamba hizi tunazowaibia kuna wakati wowote kitanuka?
Alijuwa wale ni wajinga,pesa kawapiga wake za watu wakawala vile vile
Mijitu ni mijinga kabisa

Ova
 
Unajua imani nyingi zililetwa kiujanja ujanja, lengo kuu likiwa ni kutawala watu, pili ilikuwa kupunguza unyama/ukatili uliokuwa ukifanyika miaka hiyo kwa kuwapa imani ya kusadikika.
Ashakum si matusi, hapo unaongelea imani ya kikristo iliyo letwa na wazungu Africa. Hutopata dalili hizo ulizotaja katika dini ya kiislamu, ila tu uwe tayari kuuelewa Uislamu tofauti na ule wanaouongelea wazungu.

Uislamu umeanza (not exactly umeanza) Arabuni sehemu ambayo haikuwa hata na serikali, na wala haijawahi kuwa biashara toka enzi hizo mpaka leo hii, na wala haujawahi kutumika kama nyenzo ya kuwatawala watu, na wala huijawahi kutumia force kusilimisha watu walio chini ya tawala za kiislamu. Contrary na Ukristo wa warumi, na kumbuka kwamba ukristo wote uliopo duniani hivi sasa umetoka kwa warumi, hakuna ukristo unotoa asili yake Israel.

Ila huo Uislamu wa kweli ndo unaoujua? au we unaujua Uislamu wa kigaidi ulioaminishwa dunia na wazungu mwishoni mwa miaka ya tisini?
 
Taarifa za uhakika ni kwamba Kakimbia nchini baada ya kuambiwa kuwa angeweza Kukamatwa hasa baada ya baadhi ya Waumini waliokuwa Wakisali pale Kwake kulalamika kuwa Wametapeliwa nae sana huku Wengine wakitaka Kumshtaki kwa kusababisha Ndoa zao Kuvunjika na Familia zao kuwa katika Uadui na Chuki kubwa kutokana na Mahubiri yake ya Chuki na Fitina.

Na GENTAMYCINE nauliza kwanini System ya nchi haraka sana haikuamua Kumchunga ili asikimbie kama alivyofanya?
Nani amekuambia amekimbia nchi! Alipokuja hakukujulisha na sasa amekwenda kuchukua kikosi kazi kije kiyamalize matatizo, subiri utaona.
 
Ashakum si matusi, hapo unaongelea imani ya kikristo iliyo letwa na wazungu Africa. Hutopata dalili hizo ulizotaja katika dini ya kiislamu, ila tu uwe tayari kuuelewa Uislamu tofauti na ule wanaouongelea wazungu.

Uislamu umeanza (not exactly umeanza) Arabuni sehemu ambayo haikuwa hata na serikali, na wala haijawahi kuwa biashara toka enzi hizo mpaka leo hii, na wala haujawahi kutumika kama nyenzo ya kuwatawala watu, na wala huijawahi kutumia force kusilimisha watu walio chini ya tawala za kiislamu. Contrary na Ukristo wa warumi, na kumbuka kwamba ukristo wote uliopo duniani hivi sasa umetoka kwa warumi, hakuna ukristo unotoa asili yake Israel.

Ila huo Uislamu wa kweli ndo unaoujua? au we unaujua Uislamu wa kigaidi ulioaminishwa dunia na wazungu mwishoni mwa miaka ya tisini?
Biashara ya utumwa ililetwa na nani?
 
Eti nianze kumkimbilia kakobe ana miujiza,wakati kakobe wakati anauza kanda za mziki kko nlikuwa namuona,hyo miujiza aitoe wapi
Kaja mwamposa anafungua kanisa kinondoni alikuwa na wajanja fulani wakatengana akahamia sinza akiwa solo artist naye tunamuona eti ana miujiza
😄
Nchi imejaa wjngaaa wjngaa

Ova
Makanisa yote yamejaa ujanjaujanja tu KKKT wamegawanyika sasa hivi Kuna KKKT ya Afrika Mashariki lakini wanavyoniacha hoi ni yale mashule na vyuo walivyojenga kwa sadaka za waumini masikini lakini watoto wa waumini masikini hawaruhusiwi kusoma bure,hapo huwa nachoka sana.
Dini ni utapeli wa kimfumo ila Wakatoliki, KKKT, Anglican, Orthodox,SDA nk,hawa hawaguswi kwasababu wana mizizi mirefu kuanzia huko kwa mabeberu walioleta dini ila hawa wakina Kiboko ya Wachawi wakizingua wanapigwa pini tu,ukimzingua Rwaich lazima utamsikia Papa anaunguruma huko Vatican!🤣🤣🤣
Hii laana ya kupigwa na makanisa ilianzia kwa Babu zetu huko walidanganywa na wamishonari,wakaingia Kingi, kwaiyo it's a curse ni lazima tuishi nayo tu.
 
Gamanywa sijawahi kumwelewa. Hata anavyofundisha ni kama yeye mwenyewe hajua na anababaisha sana. Ila sasa wafuasi wake huwambii kitu. Yeye na Mzee wa Malango na Mzaliwa wa kwanza ni Bla bla tupu.
Kwani Mapadri ndiyo Wana eleweka basi,wote walewale tu;Padri anasuluhisha kesi za ndoa na yeye hajawai kuoa,sasa kama siyo usanii ni nini??
 
Kwani Mapadri ndiyo Wana eleweka basi,wote walewale tu;Padri anasuluhisha kesi za ndoa na yeye hajawai kuoa,sasa kama siyo usanii ni nini??
Padre naye muulize swali linalohusu Biblia.....utapigwa na butwa majibu atakayo kupa. Utadhani kuna Biblia nyingine yeye anasoma
 
Back
Top Bottom