Mumuogope Mungu, mbona mnayoyaongea mimi mkurya (Mwireghi) wa kijiji cha Itiryo wilaya ya Tarime siyaoni? Unajua asili ya koo katika makabila mengi ya Tanzania? Unajua kwa nini tulikuwa na mapigano ya koo? unadhani ni chuki miongoni mwetu? wakulima na wafugaji wanvyopigana ni kwa sababu ni koo tofauti ndani ya kabila moja? Mbona wanaJF wanaparurana kila siku humu kwa sababu ya itikadi zao za kisiasa tena kwa matusi mazito sana, wangekuwa wanaonana uso kwa uso si ingekuwa balaa. mbona waireghi, watimbaru, wanyabhasi na koo zingine tunaishi vizuri sana, tunaoana, tunafanya biashara pamoja tena kipindi hiki ambako wizi wa mifugo haupo kwani imeisha. Wakati mwingine ni vizuri kuchangia kitu ulicho na hakika nacho, si tu umezaliwa unasikia wakurya wakorofi na wewe unaamini hivyo hivyo, mambo yanabadilika sana. Tatizo la wakurya hawapendi longolongo akipewa ofisi walozoea misheni town wanakiona cha moto, na sisi wabongo wengi tulishazoea dili. Mwisho Wakurya ni miongoni mwa makabila mazuri na rahisi sana kuishi nao ukiacha matatizo machache kama ya domestic violence na haya yanaendela kupungua